HATUPIMI BANDO

29 January 2014

BABA YAKE NI WEWE MUME WANGU

MUME: Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, sura mbaya, shule hataki, yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie, ukweli hautabadili mapenzi yangu kwako.
MKE:(Huku akipiga magoti) Mume wangu najisikia vibaya naomba unisamehe ni kweli huyo mtoto baba yake ni tofauti na wenzie
MUME: (Machozi yakimlengalenga) Dah mke wangu... baba yake ni nani?
MKE: Baba yake ni wewe.

No comments: