HATUPIMI BANDO

31 January 2014

KWANGUA USHINDE ZAWADI NONO


MIKUBWA MIZIMA MNAOGOPA BINDUKI YA KUCHEZEA

Majambazi yaliingia katika nyumba moja kuiba. Mwenye nyumba akaamka na kwa ujasiri mkubwa akachukua bunduki ya kuchezea ya mwanae na kuwatisha majambazi wenyewe wakawa wapole, akawaketisha chini, na kuanza kupigia simu polisi. Wakati mzee anaita polisi huku akiwalenga majambazi kwa ile pisto ambayo wao walidhani ni ya kweli, mtoto wa mwenye nyumba akaamka;
DOGO: Baba nataka kwenda chooni
BABA: Nenda tu mi nimewakamata hawa wezi nangojea polisi waje
DOGO: Haoooo mikubwa mizima mnaogopa binduki yangu ya kuchezea......baba mkojo ukamtoka ghafla

ANAHITAJIKA MSAFISHA KUCHA MWENYE UZOEFU, KESHO HARUSI


29 January 2014

BREAKING NYEUSSSSSIIIIII SURA MPYA MIGUU YA KIZAMANI LAIV

Katika pita pita yake mhariri asiye mkuu wa blogu hii ya divishen 5, si akasikia kuna mtu ana sura ya kisasa miguu ya kizamani, kiherehere cha uandishi uliobobea kikampanda akaanza kusaka hiyo miguu, na hapa katuletea picha akidai hii ni miguu ya kizamani ya muhusika mwenye sura ya kisasa. Mhariri anadai eti alimkuta mwenye miguu akiomba huduma ya kusafishwa kucha katika saluni moja maarufu pale Kinondoni, pale karibu na muuza chips pembeni ya benki fulani, ile saluni anayoendaga Mona, Mona huyu huyu wa kwetu. (Blog hii inakataa kata kata na kujihusisha na habari hii kwa kuwa imejipost)

BABANGU ANAWEZA KULA TAA

DOGO 1: Mi babangu anaweza kula sufuria nzima ya ugali
DOGO 2: Mi babangu anaweza kula kuku mzima peke yake
DOGO 3: Mi baba yangu anaweza kula taa
DOGO 2: Mwongo wewe anakulaje taa?
DOGO 3: Kila siku namsikia anamwambia mama, 'ZIMA TAA TULE"

HISTORIA YA BOSI WETU

Mimi mwenyewe 'live'

Naitwa John Kitime, nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza ‘bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, maana baada ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto wachanga.Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya kuchekesha, kama vile  watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, na kilabuni, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na vyuo mbalimbali nchini na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na huko nilikutana na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua kuchekesha wakijitahidi kuchekesha , cha kushangaza si nikakuta wengine hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho cha kuchekesha wachekaji.
Katika kiota hiki ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.
Pia mimi ni mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui kucheza, chacha inanichanganya kabisaaa, hii mitindo ya kisasa ndio kabisa siiwezi. Kuna hii inaitwa kiduku, wakati najitahidi kujifunza imeanza kwaito, sijaishika sawasawa imekuja Kibajaji, mara ngololo , sijui skeleu heee jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio mbadili? Halafu kwa kweli huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?

J F K

BABA YAKE NI WEWE MUME WANGU

MUME: Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, sura mbaya, shule hataki, yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie, ukweli hautabadili mapenzi yangu kwako.
MKE:(Huku akipiga magoti) Mume wangu najisikia vibaya naomba unisamehe ni kweli huyo mtoto baba yake ni tofauti na wenzie
MUME: (Machozi yakimlengalenga) Dah mke wangu... baba yake ni nani?
MKE: Baba yake ni wewe.

SIJUI NIMEINGIA MKENGE?

SIJUI NIMEINGIA MKENGE?

PROMO YA CHOO CHA KULIPIA

Nimekuta choo cha kulipia kimeweka bango la Promo likisema wazi, LIPIA KUBWA MBILI UTARUHUSIWA NDOGO MOJA BURE

27 January 2014

KILIMO KWANZA


SIJUI NIKIMBIE MJI?

Text messages za leo; MDADA: Baby naomba credit ya elfu tano nataka kumpigia simu baba Arusha. MDADA:Baby nakuja geto niandalie chips na kuku mzima nakuja na friends wangu, alafu nadaiwa elfu 35 nilikopa mpenzi wangu, mwenyewe ntakuja nae achukue. MDADA:Baby please naomba elfu 45 ya saluni kusudi nikija na wenzangu nisikutie aibu, I love you mwaahhhhhhhh.
MDADA: Baby nikija nitayarishie na hela kidogo tukitoka hapo tunaenda na wenzangu shopping mi sina hata hela ya kununua kitu. Baby hata alfu 60 zitasaidia kidogo. Love you my sweet

MINYA SEND, MINYA SEND

Jamaa mmoja kwa muda mrefu alikuwa anamfukuzia binti mmoja mrembo  na kila mara alikuwa anatolewa nje na yule binti kwa visingizio mbalimbali, hatimae siku moja wakati yumo kwenye taxi mitaa ya Tandale, mesej ikaingia ilikuwa inatoka kwa yule binti mrembo imeandikwa hivi, 'Kwa kweli sasa nimeamini unanipenda kweli, maana ni muda sasa umeonyesha nia ya kuwa nami bila kuchoka. Naomba uje kwangu jioni ya leo, je nikutegemee?'. Jamaa kwa furaha kubwa akajibu, "Ndiyo'.  Kabla hajaminya send kibaka mmoja akaipitia ile simu kama mwewe. Jamaa akabaki kupiga kelele, 'Minya send, minya send"

BREAKING NYEUSSSSSSSSSSI........ HELA ZIMEZIDI UZITO MPAKA ZIMEVUNJA SAKAFU

Kumbe zile hela ambazo huwa TUNAKATWA zilihifadhiwa ghorofa ya nne, sasa kwa sababu ni machenjichenji si yakazidi uzito, ghorofa la chini yake likaanza kuchanika. So nadhani kuanzia leo nikinunua bando nitatumia kihalali maana hela kule zimekuwa nyingi mpaka zinazavunja sakafu......

TANGAZO--ANAHITAJIKA MGANGA WA TIMU YETU, inafungwa hovyo hovyo

TANGAZO TANGAZO TANGAZO
Timu yetu ya soka ilikuwa kali kinoma, lakini katika kipindi hiki tumekuwa tunafungwa mfululizo a karibu na kila timu. Kama mashabikiwa damu,tumegundua kuwa timu yetu inalogwa sana ndio maana tunafungwa, kwa hiyo tumeamua kutangaza nafasi ya Mtaalamu Mkazi wa Timu.
Kazi ambazo Mtaalamu atalazimika kufanya ni zifuatazo;
- Kusafisha nyota ya timu ili tuweze kupata magoli
- kusafisha nyota ya kocha wetu mpya, maana kuna kitu katupiwa kinaleta mkosi
- kuhakikisha kila timu ikicheza inashinda
- kuvunja timu pinzani zisambaratike kabisa
Ili kupata mtaalam aliyebobea kutakua na usaili ambao utafanywa mwisho wa mwezi huu mbele ya viongozi wa mashabiki wa timu. Mtaalamu anaeona anaweza kufanya kazi hii atume maombi ili aelekezwe wapi aje kusailiwa.
KLABU YETU HOYEEEEEEEEEEEEEEEEE....

HE UNA UGONJWA WA ZINAA

Manesi wengine noma, jamaa alienda hospitali kumuona dokta. Akamuendea nesi aliyekuwa akipokea wageni ambao walikuwa wengi wamejazana kwenye mabenchi wanasubiri huduma; JAMAA: Samahani naomba kumuona dokta anishauri dawa, nimefanyiwa  vipimo hivi hapa...akampa nesi karatasi, nesi akasoma kile kikaratasi NESI: ( Kwa sauti kubwa) He kumbe una ugonjwa wa zinaa JAMAA: (Nae kwa sauti) Ndio, dokta alinambia na wewe ugonjwa huu ulikusumbua kwa muda mrefu sana

"MKUBWA, CHUPI HIYO MKUBWA"

KAMA UNATAKA KUVAA MLEGEZO HAKIKISHA CHUPI IKO FRESH

ZAMANI BINADAMU WALIKUWA NYANI?

DOGO: Mama hivi binadamu walitokea wapi?
MAMA: Kwanza kulikuweko na Adam na Hawa. Hawa ndio walikuwa wazazi wa kwanza wa binadamu, wakazaa watoto na watoto wao wakazaa ndio mpaka dunia ikajaa. (Dogo akaenda kwa baba yake)
DOGO: Baba hivi binadamu wametokea wapi?
BABA: Hapo zamani binadamu walikuwa nyani, wakabadilika taratibu na kuwa binadamu (Dogo akarudi kwa mama)
DOGO: Mama umenidanganya, baba amesema binadamu walikuwa nyani zamani
MAMA: Sijakudanganya, baba yako alikuwa anakuelezea historia ya ukoo wake

VICHWA VYA HABARI KIBONGOBONGO KADRI YA MHARIRI WETU MZIGO

BAADA YA KUONA MHARIRI WA BLOG HII ELIMU YAKE YA UHARIRI NI BOGUS, NA HIVYO KIMSINGI NI MZIGO, UTAWALA WA BLOG ULIMPELEKA KATA YA JIRANI KUSOMEA UHARIRI SASA KARUDI NA KUANZA KAZI YA KUHARIRI VICHWA VYA HABARI

 Acheni hizo nyie, hivi JW wakija hapo Msimbazi patakalika kweli?
 We mdada lini uliambiwa bata wanaishi baharini. Acha hizo, kula samaki.

 Ohoo hapa nikisema itakuwa taabu, Mzee dai chako mpaka kieleweke

 Teh teh teh

 Hii nimeipenda, maana mashabiki wengine wanakuja dansini bila kuoga, hivyo mama Luiza kakasirika kaona awakoshe wawe wasafi classic.

 Yanga mnatafuta kesi sasa, haya mambo ya kukuna watu mmeanza lini, tena mnamkuna mzungu si heri mnemkuna mwenzenu?

 Blog imejaribu kupiga simu ya Dida wa Times hipatikana maana tulitaka kubalans stori kama kweli kampiku Kaseja

 Watu mnaishi nyumba moja si lazima mtakuwa mnakutana kila mara? Mkiamka, mkiwa mnakunywa chai, mkiwa mnakula, mi naona swali hili la kifala la mwaka

Kingleza kigumu, sijui wana maana bado chaji imo? Yaani sio betry low, au sijui wana maana gani sijui

25 January 2014

I WANT TO MARRIAGE A GIRL PLEASE

Dear Lads and gentlemens of Facbook, Twitar, and blog, goodmoning. I am now full man, I want to merry. My Father and my mother they I am saying get marryd. I am see meny gelz and wimens in the facbook, and twitar and instantgram, I am say I am still single. I am is very good face, smilling face, I am also in Kiswahili langwej mtanashati. My father has richness of many cows for cow milk, if you come you will get many milk.  I am studied education of o levo.in St Jon seco, english medium, of internatshno teachers of Uganda and Kenya East Africa. Teacher is teaching many things to us, if you come you will enjoy. I have TV and gas cooker of 3 plates, I have sofa set ‘magongo’. I am working in Indian house, I am get very very expensive salary, if you come you will enjoy. Please beautiful gelz and wimens of facbook an twita I love you very very, so say yes for me to merry you you will enjoy.

24 January 2014

WANAUME WENGI WANANIAMBIA HIVYO

DOKTA: Binti we wamoto sana
BINTI: Teh teh teh kweli dokta wanaume wengi huwa wananambia hivyo
DOKTA: Acha ujinga nina  maana we wa moto nadhani una homa

NI KINYA TENA UWANJANI

MSANII KING KINYA KALETA KITU HIKI MUDA MFUPI ULIOPITA

INBOX YA MKAKA VS INBOX YA MDADA KWENYE SIMU


INBOX YA MDADA:
1. I luv u dear (JUMA).
 2.Nikutoe out leo? (John)
3..Huwa inaniuma sana nikikuona na wanaume wengine (Mwambi)
4.. Sweetie usisahau trip ya Bagamoyo, unambie nikupitie wapi (MD)
5..Darling, have you seen d credit I sent u?
(Mboss 1)
6..Honey najitahidi kukamilisha taratibu za kuleta posa  nakupenda sana (Evans)
7. Hilo jione kama umeshapata(Mheshimiwa 2)
8..Baby, check akaunti yako nimekuwekea kitu (Chairman)

INBOX YA MKAKA:

1..Salio lako halitoshi kukamilisha ombi lako (TIGO)
2..Ukinitumia txt nyingine namwambia rafiki yako (Jane)
3.Mwanaume gani unashindwa kutoa msaada (Patricia)
4..Unajifanya hupokei simu lakini wiki hii ni ya mwisho lipa kodi au utoke kwenye nyumba yangu(Baba mwenye nyumba)
5..Kaka nakutegemea ada (Jaki)
6..Mwanangu njaa inatuuwa usitusahau, Mungu akubariki(Mama)
7..Sijaziona siku zangu , napenda ujue hilo (Jirani House girl)

NAFUNGA BLOG

Kumpima mtumie ujumbe wa simu mwambie "Baby I love you", atakujibu 'I love you too".
Ukimwambia "I miss you", atakujibu 'I miss you too"
 Kisha umwambie,"Baby nakutumia 150,000/- kwenye M Pesa". Kama yeye atajibu,"Na mimi nakutumia 150,000/- kwenye TIGO Pesa" Nafunga blog na kutembea uchi miezi sita

KUWA WA KWANZA KUJIFUNZA KUPIGA MUZIKI KUPITIA KWAPA LAKO


23 January 2014

DAKTARI MIMACHO BWIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Mama mmoja kaingia na kitoto kichanga kwa daktari akaomba kichanga kipimwe maana kinalia lia hovyo. Daktari amamcheki mtoto, kisha akamuuliza yule mama, "Huyu mtoto ananyonya kweli?" Mama akajibu, "Ndio kila wakati". Daktari akamwambia yule mama, "Hebu tuangalie manyonyo yako". Mama akafungua blauzi, daktari akayaminya minya manyonyo kwa ufundi kisha akajaribu kuyanyonya, akatikisha kichwa. "Mama ndio maana huyu mtoto yuko hali hii, ni njaa inamsumbua. Matiti yako hayatoi maziwa kabisaaaaa". Mama akajibu, "Mi sio mama yake mi ni bibi yake, lakini nashukuru nimemleta mjukuu wangu" Daktari mimacho bwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

JIRANI UWE UNAFUNGA PAZIA USIKU

JIRANI: Oyaa ndugu yangu uwe unafunga pazia usiku jana nimekuona na wife wako mkiwa faraga.
JAMAA: Hahahahaha unachekesha sana, ukiitwa mbeya utakataa? we uliniona mimi jana? Jana mimi nilikuwa safarini Moro bwana, mke wangu alikuwa peke yake, acha hizooo

MWANANGU KAOLEWA NA JAMAA MTARATIBU SANAAkina mama wawili waliosoma pamoja walikutana sokoni baada ya salamu;
ISABELA: Jamani Adela vipi mwanao?
ADELA: Kwa kweli mwanangu kaoa mwanamke mchawi, kamloga kamuinamisha mwanangu, we fikiria, mwanamke anaamka saa 5, akiamka hapo ni kuzurula mji mzima kutumia pesa za mwanangu, mwanangu akirudi kachoka jioni, hakuti chakula, badala yake hao wanaenda kula kwenye mahoteli ya gharama, yaani we acha tu. Vipi binti yako?
ISABELA: Mtoto wangu kaolewa na mwanaume mtaratibu sana, na mpole sana, anaamka alfajiri anamtengenezea binti yangu chai anamletea chumbani, anamuachia pesa nyingi za kutumia kwenda kununua anachotaka, kila siku akirudi anampeleka kula kwenye hoteli za gharama maisha yao kwa kweli mazuri sana

22 January 2014

ONYO VALENTINE DAY HIYOOO INAKUJA, ANZENI KUJIPANGA

Kutokana na matatizo makubwa wanayopata wapenzi haswa wanaume wakati wa Valentine ni vizuri kuanza kujipanga mapema. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kufanyika :-
1. Panga kupata malaria kali kati ya tarehe 12 mpaka 15 February. Kama utaweza kuugua mpaka ukalazwa itakuwa bora zaidi
2. Tarehe 10 February anzisha zogo, mtiti, vurugu, ili mapenzi yasitishwe, tarehe 15 rudi na kupiga magoti kuomba msamaha
3. Tafuta safari ya kikazi kwenda kutembelea miradi ya vijiji vilivyo pembezoni safari ianze tarehe 10 na kumalizika 15 Februari
4. Ugua kikohozi kikali ambacho kitasababisha upoteze sauti. Fanya haya kati ya tarehe 13 na 15 February
5. Tarehe 12 February mshirikishe mwenzio katika uzinduzi wa mradi wako wa ujenzi. Hivyo kuanza kununua vifaa siku hiyo 
6. Ugua depresion na daktari atoe amri usimwone mtu anayeweza kukuletea msongo wa mawazo kuanzia tarehe 12 hadi 15 February. USHAURI MWINGINE UNAFUATIA

VAA UPESI KAITE AMBULENSI

Jamaa karudi ghafla nyumbani si akasikia sauti za ajabu toka chumbani kwake, akapiga ukelele na kuvunja mlango akamkuta mkewe akitetemeka;
Jamaa: We vipi?
Mke: Presha imepanda, jamaa akakimbia sebuleni ili apige simu ambulensi ije wakati anahangaika kutafuta namba, mwanae akaja akamwabia,'Baba anko yuko uchi kwenye kabati chumbani', jamaa akatupa simu na kurudi chumbani alipofungua mlango wa kabati akamkuta mdogo wake kabatini bila nguo nae anatetemeka ,
Jamaa: Na wewe vipi unazubaazubaa bila nguo unatisha watoto wakati shemeji yako  ameshikwa na presha. Vaa upesi kaite ambulance

VICHWA VYA HABARI MUHIMU LEO TEH TEH TEH20 January 2014

BARUA KWA MHARIRI TOKA KWA MSOMAJI WETU....

Mhariri wa Blog hii leo kaletewa barua ifuatayo
 Ndugu Mhariri shkamoo,
Mimi nina umri wa miaka 23, najisikia vibaya sana kuwa mpaka sasa sijavunja ungo. Mdogo wangu Jeni alivunja ungo toka ana miaka 14. Hili linanifanya nikose raha sana. Je, ni tatizo la mimi kuchelewa kukua? au kwa sisi wavulana tunachelewa kidogo kuvunja ungo?
M

BREAKING NEWSSSSSSSS AUKOSA UWAZIRI ATOSWA NA NYUMBA NDOGO

Katika hali ya kusikitisha bosi wetu wa Blog hii ambaye kwa muda mrefu alikuwa akitamba kwenye mabaa kuwa lazima atateuliwa kuwa Waziri, na hata akaweza kupata nyumba ndogo kwa mtaji huo, amejikuta akitupiwa virago vyake toka kwenye nyumba aliyompangishia nyumba ndogo huyo. Bosi wetu huyo ambaye na blog nayo imemfukuza kazi,kwa kuwa ilionekana angekuwa Waziri blog hii ndio ingekuwa Blog ya Taifa. Blog imejikuta ikipoteza ndoto hiyo siku ambayo Manchester United, timu pendwa ya blog hii ikilambwa 3 -1. Hivyo kisirani cha kukosekana kwa mfanya kazi Waziri na Man U kupakatwa, kimesababisha jamaa afukuzwe kazi na mabosi wenzie tena hadharani.
Asante kwa kupoteza muda kusoma hii ishu

HABARI KUTOKA MAGAZETI MBALIMBALI


1. Mtoto huyo alifariki baada ya kula nyama iliyopakwa sumu ya panya kwa ajli ya mtego. Polisi wamesema wanachunguza sababu ya kifo hicho.
 2. Jambazi alipigwa risasi na kufa hapohapo. Kwa sasa yuko ICU akiwa mahututi. chini ya ulinzi mkali wa polisi
3. Majina ya watuhumiwa hayawezi kutajwa kwa sasa kwani yataharibu upelelezi. Moja ya watuhumiwa Bwana Joni ni mfanyabiashara maarufu, na wa pili Kizigo ni mwalimu wa shule ya msingi
4.Gari lilipinduka na kuuwa abiria wote, hata hivyo kulikuweko na majeruhi wawili ambao wametibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao
5. Marehemu alifikishwa hospitali na baada ya vipimo madaktari waligundua kuwa amekwisha kufa

19 January 2014

MBONA ZOTE RANGI MOJAMume kaingia duka la nguo na kamnunulia my waif wake chupi dazani moja zote za rangi moja, akaenda kumzawadia. Mupenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote rangi moja si akalopoka.
MAI WAIF: Sasa umeninunulia chupi zote rangi moja, watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili................................... Hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
MUME:Watu gani hao? Leo utanambia'

KWA WATENDA DHAMBI TUU


Kuna watu huwa wanajifanya wajanja lakini ujanja wao ndio kifo chao halafu huwa hawajifunzi kila anapojifanya mjanja anakula za uso lakini utakuta hakomi wala habadiliki.  Jamaa yangu fulani baada ya kufa, na kutokana na midhambi yake mingi aliyokuwa akiitenda hapa duniani, akaenda moja kwa moja motoni. Kufika kule shetani akamkaribisha vizuri ila akamwambia kuwa pale kuna vyumba vyenye adhabu tofauti, jamaa yangu akaambiwa azunguke zunguke  aingie kila chumba achague adhabu anayotaka na ndiyo itakuwa adhabu yake  milele.
Jamaa yangu akaona duh kumbe mambo fresh anaweza akapata kaadhabu ambako kidogo kana nafuu, basi  kachungulia chumba cha kwanza kakuta watu wanakula mijeledi kwa kwenda mbele, mijeledi yenyewe imewekwa mizumari halafu imechovya kwenye tindikali, akaona hakufai maana kilio cha jamaa kilikuwa kikubwa. Akachungulia chumba cha pili kakuta watu wako vichwa chini miguu juu, lakini hapo chini ni misumari mitupu, tena misumari yenye moto, wanaumia wanalia na kulaani dhambi walizofanya,  akachungulia chumba kingine kakuta watu huko wako vichwa chini miguu juu na hapo chini moto unawaka vichwa viko kwenye moto, akakimbia haraka . Alipochungulia chumba kilichofuata si akakuta watu wamesimama wanatia stori wengine wanavuta fegi, wengine sigara kubwa, wengine bia mkononi, masupasta wakiume na kike kibao, rafiki zake wanawake kwa wanaume wakitia stori basi raha tu, lakini kulikuwa na harufu mbaya sana kwani walikuwa wamesimama kwenye mfereji wa maji yaliyotoka kwenye vyoo vyote kule motoni. Maji machafu ajabu yamefika kwenye magoti. Ukiondoa maudhi hayo mambo yalikuwa fresh sana.  Jamaa yangu si akaona heri ajiunge adhabu hii maana japo inaudhi  lakini ina starehe. Ile kuingia tu kakutana na jamaa wengi wakamkaribisha kinywaji, kabla hajamaliza hata chupa moja, kengele ikalia na kukatolewa tangazo kwenye spika, “Haya mapumziko kwa sasa yameisha. Mapumziko mengine ni baada ya miaka miaka mia sita, haya wote rudieni hali mliokuwa ya vichwa chini miguu juu………….

17 January 2014

SHETANI ATAKA KUMUOA MGANGA

Jamaa mmoja bonge ya mtu alikuwa na matatizo ya akili, ndugu zake wakampeleka kwa mganga, aliyekuwa katawanya mabango mji mzima kuwa yeye katoka Nigeria. Mganga akafanya vibwanga vyake mgonjwa akapandisha shetani, akawa mkorofi hashikiki, huku akipiga kelele,
MGONJWA:Nataka nataka nataka
MGANGA: Unataka nini?
MGONJWA: Nataka nataka.
MGANGA: Sema unataka nini tukupe utulie?
MGONJWA: Mganga nataka kulala na mganga
MGANGA: Umesema?
MGONJWA: Nataka kukuoa wewe.......mganga akatimua mbio vibaya sana

HEBU RUDIA TENA UMESEMAJE?

Mtoto: Mama leo tulipokuwa kwenye daladala na baba, si akaniambia nisimame nilipokaa kusudi akae Anti.
Mama: Safi sana mwanangu, baba yako anakufundisha adabu nzuri, kwa hiyo kumbuka kila mara wakubwa wakija unawaachia kiti.
Mtoto: Sikuwaachia kiti, baba alikuwa amenipakata ndio akaniambia nisimame Anti akae.
Mama: Hebu rudia tena sijasikia vizuri

MAMA DEVI NJOO UNG'OE JINOYUSI: Aise dokta nyie mnapenda sana hela mi nataka ung'oe jino bila kuleta vimbwanga vyenu, mnavyofanya kusudi tu ya kupata hela.
DOKTA: We unatakaje?
YUSI: Hivi kung'oa tu bila ganzi wala nini, itakuwa shilingi ngapi?
DOKTA: Mia tatu tu, japo si ungejitahidi uongeze alfu mbili mia mbili ung'oe na ganzi?
YUSI: Hapana  fanya hiyo ya mia tatu.
DOKTA : Dah haya kaa hapo kwenye kiti
YUSI: Hapana sio mimi, ni mke wangu. Mama Devi njoo upate matibabu

16 January 2014

HAKUNA KULALIANA HAPA

DOGO: mama naomba nikalale kwa akina Helena, mama yake amesema ataturuhusu tulale chumba kimoja mmoja juu mwingine chini
MAZA: Kasema nini? Mshenzi mkubwa huyo, hebu twende…. Maza akafunga kibwebwe tayari kwa valangati
MAZA: We mama Helena mbona huna akili kwanini unataka kuniharibia mtoto wangu mshenzi mkubwa wewe?
MAMA HELENA: Jamani kwani nini?
MAZA: We umesema watoto waje kwako wakalaliane ndio nini? Mwanamke huna haya weweeeeeeee
MAMA HELENA: Jamani  we mtoto mi nimekwambiaje
DOGO: Umesema nije nilale kwenu na Helena, moja juu mwingine chini.
MAMA HELENA: Jamani Mama Dogo, kuna kitanda cha ghorofa mtoto moja analala juu mwingine chini haaa mwanamke

NILIDHANI UMESEMA WEWE ULIKUWA YAYA

Binti alirudi kijijini baada ya miaka 5.
BABA: We mwanaharamu umeondoka hapa kwa miaka mitano hukutaka hata kutuandikia barua wala kutuma salamu unajua ulimtesa sana mama yako?
BINTI: Baba niliona niwe kimya nilikuwa nafanya kazi ya umalaya
BABA: Ayaaaaaa umetia aibu kubwa familia yangu lohh, ntatembelea wapi mimi? Kijiji chote watanicheka, kanisa litanitenga, loh jamani jamani. Ondoka hapa kijijini haraka sasa hivi
BINTI: Sawa baba, lakini nimemletea mama sanduku la nguo na kanga 20 na pesa, na hii hapa ni hati ya kiwanja nimemnunulia. Na wewe baba nimekununulia hilo Fuso nililokuja nalo na nimekufungulia akaunti benki, ina pesa utaweza kulima vizuri na kujenga nyumba nyingine ya kisasa, mwaka kesho nakuletea trekta.
BABA: Ulisema ulikuwa unafanya kazi gani?
BINTI: Umalaya
BABA: Unajua nilisikia vibaya nilidhani ulisema Uyaya, pole na kazi mwanangu

MAPENZI YA KIZUNGU IGA UFE


NI KWELI ANA MDOMO KAMA TAIRI YA TREKTA

Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni jirani kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta. Mume akapandisha na kuapa kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi. Siku walipokutana mume kanywea maana jamaa alikuwa baunsa wa ukweli;
MUME: Mambo jirani?
JIRANI: Mbona poa sana tu
MUME: Jirani nasikia ulimtukana mke wangu kuwa ana mdomo kama tairi la trekta
JIRANI: Ndio
MUME: Ahahha, tairi la mbele au la nyuma?
JIRANI: La nyuma
MUME
: Ahaa nilidhani ulisema la mbele, inaonekana mimi na wewe tunawaza sawa, ila tu sijamwambia wife, si unajua akina mama wanavyoweza kupanik.

PUNDA AFE MZIGO UFIKE


14 January 2014

SOKA............................


USIOMBE KUFUMANIA OHOOO


Usiombe kufumania, narudia tea kwa lugha ya kileo, kufumnia ni soo.
 Nilishawahi kuweko kwenye kijiwe cha washkaji fulani kukawa na mjadala kuhusu kufumania. Swali likawa Je, ukifumania utafanya nini? Majibu yalikuwa mengi, mengine yenye uamuzi mgumu, ‘ohh mi ntaua’. ‘Ohh mi ntapiga mtu  mpaka kieleweke, ‘Ohh mi namuacha mpenzi wangu hapohapo asinijue tena’ , basi majibu yalikuwa mengi, mengine siwezi kuandika humu, kuna madogo wanasoma hii ishu.
Narudia tena usiombe kufumania, kuna jamaa, jina namhifadhi alipashwa habari na watu wenye kufwatafwata mambo ya watu kuwa mkewe ana nyumba ndogo, hahahahaha, kama unadhani wanaume tu wana nyumba ndogo basi ujue hujaufahamu huu mji. Basi jamaa akapewa taarifa kuwa mkewe ana nyumba ndogo, akaamua kwa ushauri usiofaa eti akafumanie. Akaseti mambo yake na siku ya siku akalengeshwa gest ambako kulikuwa kunafanyika usaliti, hakika akawabamba mkewe na nyumba ndogo yake wakiwa katika ulimwengu mwingine kabisa, jamaa akafanya vurugu kubwa sana pale, baadae kwa kelele akaanza kumsaili mkewe.
JAMAA: Mke wangu kweli unanifanyia mimi hivi kweli?
MKE: …macho chini akiwa kimyaaaa…jamaa aliyefumaniwa akatumia wasaa huu kukimbia akiwa na shuka la gesti tupu.
JAMAA: Mke wangu nijibu kwanini umenifanyia usaliti huu? Mapenzi yote niliyokuonyesha, mipango yote tuliyopanga, oohhhhh mamama weee……Jamaa si akaanza kulia mwenyewe……yaani mke wangu unanifanyia hivi mimi, kumbuka tulikotoka, mengi tuliyopitia ….Kimya kikapita mke akakohoa kidogo.
MKE: Mume wangu kwa kweli nakiri nimekudhalilisha sana, sasa kuna kitu naomba niseme
MUME: Yaani unajibu kihuni bila aibu, unajua naweza kukufanya chochote mimi?
MKE: Ndio mume wangu naomba uiruhusu niseme
MUME: Haya sema pumba zako halafu usikie neno langu mimi kama mwanaume.
MKE: Mume wangu mi naona nimekudhalilisha mno hivyo naomba nikitoka hapa hata kwako sirudi, nakubali wewe kuniacha kuanzia leo……Sekunde kama 120 zilipita kwa kimya kikuu, feni tu la gesti lilisikika.
MUME: Sasa mke wangu mbona unaenda mbali, mi sijaongelea hayo ya kuachana
MKE: Hapana hili jambo ni la aibu nimeamua niondoke ubaki na heshima na amani ya akili.
MUME: Ngoja kwanza mi sijafika huko mke wangu, kwanza hili ni kosa la kwanza. Wahenga walisema mwenye makosa husamehewa na mimi nimekusamehe
MKE: Mume wangu mimi ntashindwa kukuangalia machoni nitakuwa sina raha kabisa ukiwepo, aibu imenizidi
MUME: Hapana mke wangu mi nimesha kusamehe, yameisha twende tu nyumbani. Tusahau yaliyopiya tugange yajayo
MKE: Hapana mume wangu, leo mwisho naona aibu
MUME: Usinifanye hivi mke wangu, kosa lenyewe hili ni dogo tu…wakati huo mzee mzima machozi yameshaanza kumlenga
MKE: Mume wangu usijidanganye, hili litatusumbua tukiendelea kuishi pamoja
MUME: Pliz mke wangu yaishe, jifanye mimi sikuja , nisamehe mke wangu kwa kuja huku nisamehe chondechonde…chezea kufumania wewe ILITOKA PIA KATIKA GAZETI LA UWAZI

KIPI BORA KUITWA JEMBE AU MPINI?

Bado najiuliza ni bora kuitwa jembe au mpini?

CHEZEA UGALI WEWE


BREKING NYEUSIIIII MSANII AKAMATWA KAMEZA MAJANI YA BANGI

Baada ya wasanii kadhaa kukamatwa wamemeza na madawa ya kulevya katika nchi mbalimbali na kujikuta kwenye mamidia na magazeti, msanii mmoja wa longi kidogo nae kaamua kukamatwa na madawa ya kulevya mitaa ya Sinza ili kusafisha nyota, inadaiwa na yeye eti kaamua kumeza majani ya bangi kama walivyomeza wenzie kete, inadaiwa yuko kituo fulani anangojewa atoe majani hayo kupitia njia ya kujisaidia.......habari zaidi zitafuatia baada ya blog hii kuwapata  wandishi wake  ambao imegundulika kuwa wako katika likizo ya wikiendi ndeeeefuuuuuuu

OYAA MJESHI VIPI TENA?


RASTA KIPARA


VICHWA VYA HABARI HAHAHAHAHAHA

 Chezea Bongo wewe

Aliyeandika hili ana ishu ya siri

11 January 2014

MTEJA MFALME

Jamaa kapata kazi ya kuuza duka, siku moja bosi wake kaingia ghafla dukani kakuta ubishi mkali na kijana wake anamtukana mteja. Akaamulia ugomvi, mteja akaondoka;
MWENYE DUKA: Leo mi nakufukuza kazi, mara ngapi na kuambia kuwa mteja ni mfalme na analosema mteja ndio sahihi? Kamwe usimbishie mteja, anachosema wewe kubali, kwani utapata kovu gani ukikubali?
JAMAA: Mteja yule kaja hapa akaanza kusema mwenye duka hili, punguwani hana akili

WE MKUBALI TU, KIKUBWA UHAI


Jamaa alitoroka jela ambako alikuwa kafungwa miaka 25. Nyumba ya kwanza aliyovunja akamkuta mtu na mkewe wamelala. Akawaamsha kwa vitisho kisha akawafunga kamba kwenye kitanda. Baada ya hapo akainama na kumnong’oneza kitu yule mke, kisha akaelekea bafuni. Wakati yuko huko mume akamwambia mkewe, ‘Sikiliza huyu jamaa ni wazi katoroka jela si unaona nguo zake? Sasa nimemuona anavyokuangalia, ili asituuwe chochote atakachotaka we mkubali tu, mridhishe hata kama kitakuwa kinakuchefua, itakuwa siri yetu kikubwa uhai. Nakuenda sana mke wangu’. Mke akajibu,’ Si umeona kaninong’oneza kitu? Alikuwa ananiambia jela kumemzoesha wanaume, na wewe kakupenda, kaenda bafuni kujitayarisha. Mume wangu ili asituuwe chochote atakachotaka we mkubali tu, mridhishe hata kama kitakuwa kinakuchefua, itakuwa siri yetu kikubwa ni uhai. Na mie nakupenda sana mume wangu”

MBINU MPYA


BEBI NINA MIMBA

MDADA: Bebi sizioni siku zangu
MKAKA: Kwa hiyo mie nimekuibia? mie mwizi sio? Yaani umeona sasa ndio unidharau kabisaaa. Hebu beba kilicho chako na usepe

OHHH BEBI OHH BEBI NAKUPENDA SANA

MKAKA: Unajua bebi, mi sina fedha kama Diamond, wala sina gari kama Diamond lakini mimi nina mapenzi ya kweli. Ntakupenda mpaka kufa
MDADA: Bebi hata mimi nakupenda sana, Diamond anakaa wapi?

UNATUMIA SAHANI YAKE

MGENI: Dah mbwa wenu mbona ananiangalia sana ninapokula?
DOGO: Labda kwa sababu unatumia sahani yake anayotumiaga kula

9 January 2014

JE UNATAKA KUONDOA TATOO BURE, INGIA HAPA

Kuna wadada na wakaka wengi ambao wamejikuta wakiingia kwenye mkumbo wa kuchora tattoo kwenye miili yao mwaka 2013 na sasa wamegundua hawazitaki na wangependa kuziondoa. Blog yenu inayowapenda imewatafutia jibu la tatizo hili sugu. Andika namba au email yako hapa chini tukufuate popote ulipo na kuondoa tatto kwa dakika tano tu. We love you our people

YAANI BEBI WE HENDSAM WA MWAKA 2014


BINTI YANGU NI WA KIKE

Wababa watatu wamekutana bar, ulevi ulipowazidia  wakaanza kuongea kuhusu binti zao,
BABA 1: Kuna siku niliingia chumba cha binti yangu nikashanga kukuta kichungi cha sigara wakati najua havuti
BABA 2: Mi nilikuta chupa tupu ya bia wakati binti yangu hanywi
BABA 3: Wangu ndo ya ajabu zaidi, mi nilikuta kondom ya kiume imetumika chumbani kwake wakati yeye mwanamke.

HILO PILAU LA KWENYE MSIBA WAKO

Jamaa alikuwa kitandani hoi kwa maradhi muda mrefu, siku hiyo akasikia harufu ya bonge la pilau. Na alikuwa akipenda kweli pilau. Kwa kuwa hata kauli alikuwa kakata akatambaa toka kitandani hadi jikoni alipotaka kuchota pilau mkewe akamkemea,' We acha hiyo ni pilau, ya watakao kuja kwenye msiba wako'