PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SALAM ZA MWAKA WA ZAMANI 2013 KWA WASOMAJI WA CHEKANAKITIME


Leo ni Jumapili ya mwisho ya mwaka 2013, ningependa nichukue nafasi hii, kusema machache kwa wote wale ambao walilazimika kucheka kutokana na aidha post zangu kwenye Facebook au kwenye www.chekanakitime.blogspot.com. Ki ukweli kwa makusudi kabisa niliandika mambo kusudi muondoe stress zenu ambazo zinasababisha mtindio wa ule ugonjwa ambao kisayansi unaitwa medulla oblongata ( wabishi nyamazenu sorry nyamazeni). Utafiti uliofanywa na wanasayansi flani kisiri sana (hili pliz msimwambie mtu) imeonekana kuwa wanaosoma mambo yangu wengi ghafla wamekuwa watu wenye umuhimu katika jamii yetu. Kwa mfano jamaa mmoja aliyekuwa mwembamba sana alienda ujerumani akarudi amenenepa tena kaniletea na saa ya mkononi, juzi juzi kaitwa mpaka kwenye kipindi cha TV aeleze amewezaje kunenepa?. Kiongozi mmoja ambaye awali alikuwa akijulikana kama mzigo baada ya kupata mafunzo ya uongozi bora kutoka chekanaKitime kwa sasa amepasi ameoneka si mzigo tena. Askari mmoja aliyenisalimia pale Msasani amepewa cheo kikubwa cha unesi katika hospitali moja kubwa jijini baada ya kupata mafunzo kutoka humu chekanaKitime. Mama mmoja ambaye majirani wote kwa sababu ambazo hazijulikani humuita Mama Mdogo baada ya kuanza kusoma chekanakitime siku hizi kapandishwa cheo pale mtaani wanamuita Bimkubwa. Jamaa mmoja ambaye alikuwa na ugonjwa wa kuovatek kwenye foleni siku hizi ameokoka baada ya kusoma maelezo kadhaa yaliyokuwa kwenye ukurasa wangu wa Facebook, siku hizi haovatek hovyo, anapanda kibajaji.
Ningependa kusisitiza kuwa 2014 naongeza wataalamu wa kusaidia hii kazi ili chekanakitime iwekwe kwenye silabasi ya vyuo vyote vikuu na vile vikuukuu na vile ambavyo sio vikuu, ili kuweza kuasidia kujenga kizazi kisichoeleweka zaidi ya hali ilivyo sasa. Iwe ni agizo la serikali kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi wafungue ukurasa wangu wa Facebook kabla ya kuanza masomo yao, aftaol kuna mengi ya kujifunza humu au siyo? Tayari kunawafanyakazi wa ofisi nyingi wameshaathirika na kaugonjwa hako kakupitia ukurasa huu wakiwasha tu PC za chama, serikali na kampuni binafsi, mashirika ya umaa, na hata ofisi nyeti .

MWISHO NAWATAKIENI HERI YA MWAKA MPYA……….

Comments