HATUPIMI BANDO

9 November 2013

TUNAUZA MVUA TOKA CHINA

Kijana ndio kwanza kaajiriwa kuuza dukani, siku hiyo mwenye duka akiwa kakaa kwenye kiofisi cha ndani akasikia kijana wake akimjibu mteja;
KIJANA: Kwa kweli mama hatuna kabisaa, na nikiangalia dalili sidhani kama tutakuwa nayo karibuni...mwenye duka katoka haraka kwenye ofisi na kumuwahi mteja;
MWENYE DUKA: Hapana mama. kijana wangu amekosea, hiyo tumeishiwa jana tu na nimekwisha agiza oda kubwa toka Uchina, ukija wiki ijayo utapata kila aina. Kisha akamvuta kijana wake pembeni......
MWENYE DUKA: Nakumwambia..mwiko, nasema mwiko katika duka langu kusema kitu hakuna umeona nilivyojibu? Na huyu mama sasa amepata imani na duka hili. Haya huyu mama alikuwa anaulizia nini?
KIJANA: Mzee ulitukatisha tulikuwa tunaongelea MVUA

No comments: