PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SI UMESEMA NIMKATEKATE

Jamaa mmoja mwenye akili hazijatosha kenda kuomba kazi ya usanii  Bongo muvi ili aekt. Kuondoa kero dairekta akamkubali . Wakampa na panga kabisa.
DAIREKTA: Sasa  wew utaekti kama mlinzi wa geti unasikia? Na huyu supasta ataekti kama mwizi, we utamfukuza sawa? haya chukua na panga hili la kuektia
MLINZI: Sawa.
DAIREKTA: Ukisikia nasema ekshen, unaanza kumfukuza umesikia? Haya kila mtu tayari? EKSHEN....mlinzi akaanza kumfukuza supasta kwa bidii
DAIREKTA: Cut cut cut......si chizi akaanza kumkata mapanga supasta, ilikuwa kimbembe kumuamulia
DAIREKTA: Sasa wewe unafanya nini?
MLINZI: Si umesema nimkatekate?

Comments