PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MSUKULE WA MJOMBA WAKO ULIPITA HAPA JANA

Jamaa kaaga kazini kuwa anaenda kwenye mazishi ya mjomba wake. Baada ya siku tatu alipo ripoti kazini akaambiwa anahitajika kwa bosi,
Bosi: Pole na msiba wa mjomba wako
Jamaa: Asante bosi, umeniuma sana kwa kweli.
Bosi: Ukoo wenu kuna tatizo la misukule?
Jamaa: Hapana bosi, kwanza mimi siamini mambo ya kishirikina
Bosi: Nadhani sasa limeanza, maana jana wakati umeenda kwenye mazishi ya mjomba wako,msukule wake ulipita hapa kuja kukusalimia.

Comments