PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MCHUNGAJI KAMKATAA MBUZI WA WIZI

Jamaa kaenda kaingia nyumbani kwa mchungaji  akionekana ana majonzi makubwa;
MCHUNGAJI: Vipi ndugu yangu?
JAMAA: Familia yangu ina njaa, nimemuibia mtu mbuzi yuko hapo nje, najisikia vibaya naomba tafadhali umchukue
MCHUNGAJI: Aaa wapi, sipokei mali ya wizi mimi. Kwanini usimrudishie mwenye mbuzi wake?
JAMAA: Mwenye mbuzi kamkataa
MCHUNGAJI: Basi kama hivyo huyo halali yako kalishe familia yako
JAMAA:Asante sana mzee asante sana.
  Mchungaji alipoamka kesho yake akagundua mbuzi wake  kaibiwa

Comments