HATUPIMI BANDO

23 November 2013

MAMA YUKO JUU YA PAA

Jamaa mmoja alikuwa akiishi na mdogo wake na mama yake, pia wakawa na kambwa ambako jamaa alikapenda mno. Siku moja akapata safari ya wiki moja, siku aliporudi tu kabla hajaingia ndani, mdogo wake akamuwahi;
DOGO: Kaka mbwa wako kafariki juzi......jamaa alisikitika sana, na zaidi hakupenda jinsi alivyopewa taarifa ya msiba huu
MJAMAA: We vipi unaona nilivyoshtuka, ilitakiwa  jambo la msiba kama hili ungeanza kunambia, mbwa wako yuko juu kwenye paa, halafu unanambia mbwa kadondoka toka kwenye paa, nakuwa nimejitayarisha kisaikolojia
DOGO: Sawa kaka ntajirekibisha
MJAMAA: Mama yuko wapi?
DOGO: Mama yuko juu kwenye paa
MJAMAA: Ehh!