HATUPIMI BANDO

24 November 2013

JAMAA AGEUZWA NA JINI KUWA SAMSUNG S6

Jamaa alikuwa anaokota chupa za plastik akauze, ghafla akaokota chupa moja ya ajabu kidogo iliyokuwa na mfuniko na ndani imejaa akaifungua, ili kufungua tu moshi mzito ukatoka kumbe kulikuwa na jini lilifungiwa mle ndani;
JINI: Dah asante kwa kuniweka huru omba vitu viwili vyovyote ntakupa
JAMAA: Naomba fedha, nifanyie kitu kama bilioni moja...mara ileile jini likampa jamaa ATM kadi mpyaa  
JINI: Nipe ombi lako la pili
JAMAA: Nataka unigeuze niwe kile kitu ambacho mademu wa kisasa wanakipenda
JINI AKAMGEUZA JAMAA AKAWA SIMU YA SAMSUNG S6 

No comments: