PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BABA KILA SIKU ALIKUWA ANALALA NJE

Baada ya mkewe kusafiri, wiki ya pili tu jamaa akawa anaboreka chumbani akawa anaangalia TV sebuleni mwisho analala hapohapo mpaka asubuhi. Hatimae mkewe akarudi, kwa umbeya wake akamuita pembeni mdada wa kazi na kuanza kumsaili
MKE: Vipi mambo yalikuwa salama nilipokuwa safarini?
MDADA: Mambo yalikuwa safi tu
MKE: Baba hakukusumbua?
MDADA: Wala hakunisumbua
MKE: Baba alikuwa analala wapi?
MDADA: Mwanzo alikuwa analala ndani, baadae kila siku akawa analala nje
Mke kaanguka kwa presha

Comments