HATUPIMI BANDO

29 November 2013

WELCOME TO BONGOLAND...PLEASE COME WITH YOUR OWN ELECTRICITY


MCHUNGAJI KAMKATAA MBUZI WA WIZI

Jamaa kaenda kaingia nyumbani kwa mchungaji  akionekana ana majonzi makubwa;
MCHUNGAJI: Vipi ndugu yangu?
JAMAA: Familia yangu ina njaa, nimemuibia mtu mbuzi yuko hapo nje, najisikia vibaya naomba tafadhali umchukue
MCHUNGAJI: Aaa wapi, sipokei mali ya wizi mimi. Kwanini usimrudishie mwenye mbuzi wake?
JAMAA: Mwenye mbuzi kamkataa
MCHUNGAJI: Basi kama hivyo huyo halali yako kalishe familia yako
JAMAA:Asante sana mzee asante sana.
  Mchungaji alipoamka kesho yake akagundua mbuzi wake  kaibiwa

28 November 2013

BINTI UNASEMA ULIBAKWA?

Binti mahakamani kashtaki kuwa kabakwa,
HAKIMU: Binti umeshtaki kuwa umebakwa na mwenzio anasema mlikubaliana, unaweza kuieleza mahakama kwanini unasema umebakwa?

MDADA: Mheshimiwa ni pale huyu jamaa alipokataa kunilipa hela yangu, ndo nikagundua kuwa kanibaka

BONGO SUPERSTAR'S COMEDY NI KU..........LILILOWEKA KAMBI TANGA

BLOG HII TATA BADO INASHANGAA SHANGAA BAADA YA KUSOMA MAELEZO YA BONGO SUPERSTAR'S COMEDY SOMA KWA MAKINI HAPA

HATA INDIA WAKO SANA TU


26 November 2013

SI UMESEMA NIMKATEKATE

Jamaa mmoja mwenye akili hazijatosha kenda kuomba kazi ya usanii  Bongo muvi ili aekt. Kuondoa kero dairekta akamkubali . Wakampa na panga kabisa.
DAIREKTA: Sasa  wew utaekti kama mlinzi wa geti unasikia? Na huyu supasta ataekti kama mwizi, we utamfukuza sawa? haya chukua na panga hili la kuektia
MLINZI: Sawa.
DAIREKTA: Ukisikia nasema ekshen, unaanza kumfukuza umesikia? Haya kila mtu tayari? EKSHEN....mlinzi akaanza kumfukuza supasta kwa bidii
DAIREKTA: Cut cut cut......si chizi akaanza kumkata mapanga supasta, ilikuwa kimbembe kumuamulia
DAIREKTA: Sasa wewe unafanya nini?
MLINZI: Si umesema nimkatekate?

24 November 2013

HUWEZI KUOLEWA NA KAKA YAKO

Ugomvi mkubwa ulikuwa unaendelea kati ya mtu na mkewe;
MKE: Yaani heri ningeolewa na shetani kuliko baba wewe.
MUME: Dini na mila zingekukataza kuolewa na kaka yako

JAMAA AGEUZWA NA JINI KUWA SAMSUNG S6

Jamaa alikuwa anaokota chupa za plastik akauze, ghafla akaokota chupa moja ya ajabu kidogo iliyokuwa na mfuniko na ndani imejaa akaifungua, ili kufungua tu moshi mzito ukatoka kumbe kulikuwa na jini lilifungiwa mle ndani;
JINI: Dah asante kwa kuniweka huru omba vitu viwili vyovyote ntakupa
JAMAA: Naomba fedha, nifanyie kitu kama bilioni moja...mara ileile jini likampa jamaa ATM kadi mpyaa  
JINI: Nipe ombi lako la pili
JAMAA: Nataka unigeuze niwe kile kitu ambacho mademu wa kisasa wanakipenda
JINI AKAMGEUZA JAMAA AKAWA SIMU YA SAMSUNG S6 

23 November 2013

MAMA YUKO JUU YA PAA

Jamaa mmoja alikuwa akiishi na mdogo wake na mama yake, pia wakawa na kambwa ambako jamaa alikapenda mno. Siku moja akapata safari ya wiki moja, siku aliporudi tu kabla hajaingia ndani, mdogo wake akamuwahi;
DOGO: Kaka mbwa wako kafariki juzi......jamaa alisikitika sana, na zaidi hakupenda jinsi alivyopewa taarifa ya msiba huu
MJAMAA: We vipi unaona nilivyoshtuka, ilitakiwa  jambo la msiba kama hili ungeanza kunambia, mbwa wako yuko juu kwenye paa, halafu unanambia mbwa kadondoka toka kwenye paa, nakuwa nimejitayarisha kisaikolojia
DOGO: Sawa kaka ntajirekibisha
MJAMAA: Mama yuko wapi?
DOGO: Mama yuko juu kwenye paa
MJAMAA: Ehh!

NIMEFOL IN LAV NIMEFOL IN LAV WEWEEEEE


21 November 2013

WANAMUZIKI WA KISASA, SWAGA KWA KWENDA MBELE

OYAAAAAA NASEMA MIMI NI MKALI NATOKA MBALI NAENDA MBALI
SINA HABARI
 SEMA YEEEEEAAAA WATU WOTE MIKONO JUUU

JIFUNZE KUKAMATA NYOKA LAIV..SOMO KWA PICHA

Blog yenu kali kuliko zote katika nchi ya Wagagagigikoko, inakuletea somo la namna ya kukamata nyoka laiv. Yaani wewe fuata haya maelekezo utaweza kukamata nyoka laiv bila chenga
20 November 2013

NAIBU WAZIRI AFUNGWA MWAKA MMOJA NA KAZI NGUMU KWA KUFOJI VYETI VYA CHUO CHA UHASIBU

Waziri aliwa mikono juu kwa raha zake
BLOG YENU TATA leo ina taarifa tofauti na kawaida, kwa hiyo hakuna kucheka. Naibu Waziri wa Michezo wa Zambia Stephen Masumba, ambaye ni kijana mjanja mjanja anaependa totoz, ameingia katika tatizo kubwa baada ya kukutwa na hatia ya kufoji vyeti vya elimu yake. Na mahakama imeona im zawadie tuzo la kifungo cha mwaka mmoja na kazi ngumu, mjanja mjanja huyu pia ni Mbunge wa jimbo la Mfumbwe
 Chezea Zambia weweee
Kwa wale wabishi someni HAPA
Waziri na staili yake ya mikono juu

Waziri akionyesha vyeti vilivyokuja kumponza

MAUMIVU YATAHAMIA KWA BABA WA MTOTO

Mama mmoja mja mzito na mumewe walikwenda kwa mganga wa kienyeji awape dawa ya kuondoa maumivu wakati yule mama anazaa. Mganga akawapa punje tatu za karanga akamwambia yule mama akisikia maumivu atafune karanga moja maumivu yatahamia kwa baba wa mtoto. Mumewe akakubali kubeba mzigo wa maumivu. Siku ya kujifungua wakawa hospitali, mama alipoona maumivu yanaanza akatafuna punje moja, maumivu yakapotea, mumewe aliyekuwa pembeni yake akamwambia,'Nyie wanawake kumbe huwa mnajidekeza tu, mbona sioni maumivu yoyote'. Baada ya muda maumivu yakamrudia yule mama akala punje nyingine, matokeo yakawa vilevile, mume hakusikia chochote akawa anacheka sana tu. Hatimae yule mama akaanza kupata maumivu makali ya kujifungua akatafuna punje ya mwisho na kujifungua salama bila maumivu kwake wala kwa mumewe. Wakarudi nyumbani na furaha, furaha yao ikakatishwa kwa kukuta kuna msiba wa kijana wao wa kazi aliyekutwa amefariki. Majirani walidai alikuwa analalamika kwa maumivu makali kama vile anataka kuzaa.....

19 November 2013

MJANE MZEE ANAKAA WAPI?

Jamaa: Mjomba nina jambo linanizingua.
Mjomba: Nini tena nambie
Jamaa: Nataka kuoa sasa nina wapenzi wawili, wa kwanza ambaye ndiye moyo wangu unampenda ni msichana mzuri lakini masikini, wa pili ni bibi moja mjane mzee lakini tajiri, nifanye nini mjomba?
Mjomba: Fwata moyo wako mjomba wangu, fuata moyo, muoe unaempenda mjomba wangu.
Jamaa: Yaani mjomba asante kwa mawazo mazuri , hata mimi nilikuwa nafikiria hivyohivyo,
Mjomba: Sasa umesema huyo mjane mzee anakaa wapi

LEO NI SIKU YA CHOO DUNIANI - WORLD TOILET DAY


18 November 2013

15 November 2013

KAMA WE NI DIVISHENI V HUONI NDANI HAPA...sepaaa


Blogu yenu makini yagundua makubwa sana

VIATU VINAUZWA

Pendeza wiki endi hii na viatu swafiii toka Uchina. Vinatumika mara moja ukibahatisha kuwa navyo mara mbili shukuru Mungu.


MAKALIO MAZIMA KABISA YAMETUPWA

Chizi kapita katika uchochoro mmoja si akakuta mtu kalala kwenye pia la taka. Kumbe yule mtu alikuwa mlevi tu kapitiliza . Chizi kamuangalia kisha akamshika makalio yule mlevi na kujaribu kumuamsha, mlevi akashtuka kidogo, chizi akarudi nyuma kwa mshangao na kusema kwa nguvu, "Dah mtaa huu matajiri kweli, makalio mazima kabisa wameyatupa"

CHEKANAKITIME AWARDS 2013 YAMUENDEA 'LE PROFESERE'

ILE KAMATI YA CHEKANAKITIME AWARDS AMBAYO INAYOJULIKANA WAZI BILA KIFICHO KUWA INAPENDA SANA  RUSHWA (YENYEWE HAIJIFICHI KAMA HIZO NYINGINE),  KWA MARA YA KWANZA IMETOA UAMUZI BILA MJUMBE YOYOTE KULA RUSHWA, KUWA 'LE PROFESERE' APEWE CHEKANAKITIME AWARDS KWA "THE BEST UDWANZI  2013".
KUNA MADWANZI LAKINI 'LE PROFESERE' AMEWAZIDI. HONGERA  'LE PROFESERE'. AWARDS HIZI UTAKABIDHIWA MARA TU UTAKAPOKABIDHIWA CHETI CHA KUFUZU KUINGIA LOPANGO UNIVESITI

NAJICHANGANYA KWA DEMU WA KICHINA NA KINGLEZA CHANGU CHA DIVISHEN V


Kingleza bwana we acha tu. Jana si nimeenda klabu nikanyooshe viungo, kwenye kona moja  nikakutana na bonge ya binti wa Kichina, hajui Kiswahili mi sijui Kichina, tukaanza kuhangaishana  kwa Kingleza cha divishen V ya Bongo, kikienda ana kwa ana na kingleza cha divishen V ya China, hatimae tukafikia pazuri tu na muwekezaji huyu nikaona nimuombe namba yake ya simu, si unajua siku hizi, whatsapp na viber na hookt yanarahisisha mawasiliano ( if you know what I mean),
MIMI: Please give me ze number of you
MCHINA: Ok  All night sex sex ,free sex free sex tonight.
MIMI: (Nikiwa nimetoa mimacho) Umesema? Excuse  me what you I am saying?
MCHINA: Flend me give you phone, All night sex sex
free sex free sex tonight…………wakati kengele za furaha zinagonga kichwani kwa sababu ambazo kumbe sizo, si  ndo nikagundua kumbe ananipa namba yake ya simu 0966-363629

14 November 2013

WAMEMUONEA TU, ILE G STRING NI YAKE MWENYEWE ANAIVAAGA USHAHIDI HUU HAPA


AKUU MI SIVAAGI

MAMA MWENYE NYUMBA:Jamani chupi zangu sizioni zinaenda wapi? We dada au umechukua wewe?
MDADA WA KAZI: Akuu mi sivaagi muulize hata baba

UTACHEKA HUKU UNALIA

MUME: Hawa wanasaikolojia wanachekesha, eti mtu unaweza kusikia jambo likakuudhi na kukufurahisha wakati huohuo. Hahahahaha mke wangu unaweza kunambia jambo kama hilo?
MKE: We mtamu kuliko rafiki zako

13 November 2013

ACHA MASWALI YA KIJINGA MI NALALA

MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike?
MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala
MKE: Na lipstiki kwenye shati?
MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu
MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali?
MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi
MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani
MUME: Umesema nini wewe?
MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi

12 November 2013

PICHA LA KIDOSI....VIDEO
UZEE MWISHO CHALINZE. HAPA KILA MTU BEBII


MUKISHIKIA NIMEKUFA MUSIWEKE MUSIBA MUKO NA RHOHO MUBAYAAA

Jue vile bantu bako na rhoho mubaya, hawanagha wupendo ule uko ndani ya rhoho. Mi nalizaliwagha hapa hapa pa Tanzanii, mama yangu eko na shamba mukubwa kuli kuiringa, Mi nikatumika kufwasi mingi ya miziki na mi nilifaaga mukazi kumuyi mukulu wa Dodome, watu yote ya Dodome iko wananiyuaga. Eti batu banabambia ba imigrasyo , banasema mimi iko mutu ya fashi ya ngambo ya mayi, shi ndyo roho mubaya. Mukisikia nimekufa musiweke musiba, mimi iko ni mutanzanii, ile ya damu

KISWAHILI CHA JAMAA ZETU WA KENYA


Jamaa watatu walikuwa wamepanda matatu;
MLUO: Kondakta Sukisa mimi hapo sell gas steson. MKIKUYU: Ehh dugu yagu,naona ukona chida ya matamuchi……na akacheka sanaa
MSOMALI: Habana jeka menzako, nyinyi yote hamajui gubronounce mazuri swahel

MASHINE KUBWA BADILISHA SPEA

Dingi mmoja ya miaka 80 alioa kabinti ka miaka 21. Baada ya mwaka kabinti kakajifungua mtoto wa kwanza, mzee akawa anapita na kujigamba kuwa yeye mashine kubwa. Baada ya miaka miwili kabinti kakajifungua tena mtoto mwingine, kabla hata Dingi hajamuona mtoto akapita mitaani tena akijisifu tena kuwa mashine kubwa. Alipofika hospitali akamkuta nesi,
Mzee: Nesi mashine kubwa nimefika wapi mali zangu?
Nesi: Mzee mashine yako inatumia spea za Kihindi?
Mzee: Kwanini unanuliza?
Mzee: Badilisha maana safari hii kazaliwa Mhindi

JE UMEWAHI KUSAHAU NINI?

DOKTA: Umesema una ugonjwa wa kusahau sahau?
MGONJWA: Ndio
DOKTA:Hebu nipe mfano wa kitu ulichowahi kusahau...

9 November 2013

KWAHERINI MAISHA MAGUMU


IMEANDIKWA KWENYE SKRIPT HAKUUMI

Dairekta wa Bongo muvi kamwambia muigizaji supasta;
DAIREKTA: Sasa sini inayofuata tutamuachia mbwa mkali, akufukuze, sasa atakufukuza tu lakini hawezi kukuuma
SUPASTAA: Unajuaje kama mbwa hawezi kuniuma?
DAIREKTA: Hivyo ndivyo ilivyoandikwa kwenye skript
SUPASTAA: We  we we acha hizo, huyo mbwa amesoma hiyo skripti?

UNANITAFUNA KICHWA MIMI?

Dogo alikuwa katika usingizi mzito akaota anatafuna papai, akalitafuna mpaka likaisha, ghafla akaona nazi, akajaribu kuivunja akashindwa akaona heri aitafune tu kwa meno, ila anaanza tu, akaamshwa kwa bonge la kofi toka kwa baba yake.
BABA: Pumbafu mkubwa, umetafuna mto nakuangalia, umemaliza sasa unaanza kunitafuna kichwa changu mjinga mkubwa

TUNAUZA MVUA TOKA CHINA

Kijana ndio kwanza kaajiriwa kuuza dukani, siku hiyo mwenye duka akiwa kakaa kwenye kiofisi cha ndani akasikia kijana wake akimjibu mteja;
KIJANA: Kwa kweli mama hatuna kabisaa, na nikiangalia dalili sidhani kama tutakuwa nayo karibuni...mwenye duka katoka haraka kwenye ofisi na kumuwahi mteja;
MWENYE DUKA: Hapana mama. kijana wangu amekosea, hiyo tumeishiwa jana tu na nimekwisha agiza oda kubwa toka Uchina, ukija wiki ijayo utapata kila aina. Kisha akamvuta kijana wake pembeni......
MWENYE DUKA: Nakumwambia..mwiko, nasema mwiko katika duka langu kusema kitu hakuna umeona nilivyojibu? Na huyu mama sasa amepata imani na duka hili. Haya huyu mama alikuwa anaulizia nini?
KIJANA: Mzee ulitukatisha tulikuwa tunaongelea MVUA

8 November 2013

BABA NA MAMA WAMENIIBIA BAISKELI

Dogo kaenda polisi post kushtaki baiskeli yake imeibiwa, na anadhani walioiba ni baba na mama yake.
POLISI: Hee Dogo kwanini unadhani wazazi wako ndio wamekuibia baiskeli?
DOGO: Usiku nilishtuka nikamsikia mama ana mwambia baba, simamisha  nipande, asubuhi nilipo amka sikuiona baiskeli

HONGERAAA BLOGU YETU YAPATA UFAULU WA DIVISHENI YA TANO +

KWA FURAHA  kuu mabosi wa Blog wamepata barua kutoka kwa Mamlaka inayohusika ikiwasifu ALIVE watumiaji na watayarishaji wa Blogu hii kuwa wote wamefuzu kwa kiwango cha Divishen 5 au V au aka 0.
Ufaulu huu ni wa kupongezwa kwa kuwa kwetu hakuna kufeli na ndio maana nchi jirani zinatuonea wivu zinaanza eti kujitafutia kamuungano kake. Ndugu wasomaji wa Blog hi hasa wale wanaosoma blogu saa za kazi huu ni wakati wa kusheherekea I mean kushekerekea, I mean kusherehekeaa ufaulu huu unaotuweka katika kiwango cha kitaifa na kimataifa.
Asanteni.

BARUA TOKA KWA MDAU WA BLOG HII MUHIMU KITAIFA NA KIMATAIFA

Good morning Sir Anko Kitime,
Pliz my name is ************ I am finish fom for. Ze everybody is to say we get za divishen 0, My part I am saying not I am not get divshen 0. I am vere vere intelijens, but pipoz don’t like me. I have experience in singing bongoflava, so pipoz are jelas, the have put majik so I get diveshen 0. But I am clever becoz ask me forekzampo, what is fomula for water? Ze fomula for water iz Hech to o. Now why you give me dishen 0? Ok ask me anadha forekzampo what iz President of America? Ze president of America iz Obama. Ze gavament shud change my marks to dishen 5, because the youth are  future of my country. If we get divishen 0 zen all the future is divishen 0. So giv us more maks becoz of ze future.
I know you know Mr Prezdent, pliz nibembelezee for me and ze future

ULIPOKUWA MDOGO ULIKUWA UNALIA SANA

Ndani ya daladala dogo mmoja alikuwa analia kwa nguvu,
MBABA: We nyamaza kulia ukilia sana ukiwa mkubwa utakuwa na sura mbaya....Dogo akanyamaza ghafla, halafu akamuangalia yule Mbaba kwa muda .....
DOGO: Ndio kusema we ulipokuwa mdogo ulikuwa unalia sana?

7 November 2013

MAMBO YA MUVI HAYA


CHONDE CHONDE DOKTA NIKATE HII MIKONO

MGONJWA:Dokta kuna ndoto inanijia kila usiku naomba msaada wako
DOKTA: Unaota nini?
MGONJWA: Dokta naota warembo masupasta wote wa bongo  wanapigania kunibaka, mi napigana nao nawatandika mingumi mpaka wanakimbia wote
DOKTA: Sasa watakaje ndugu yangu
MGONJWA: Dokta chonde chonde nikate hii mikono dokta

MSUKULE WA MJOMBA WAKO ULIPITA HAPA JANA

Jamaa kaaga kazini kuwa anaenda kwenye mazishi ya mjomba wake. Baada ya siku tatu alipo ripoti kazini akaambiwa anahitajika kwa bosi,
Bosi: Pole na msiba wa mjomba wako
Jamaa: Asante bosi, umeniuma sana kwa kweli.
Bosi: Ukoo wenu kuna tatizo la misukule?
Jamaa: Hapana bosi, kwanza mimi siamini mambo ya kishirikina
Bosi: Nadhani sasa limeanza, maana jana wakati umeenda kwenye mazishi ya mjomba wako,msukule wake ulipita hapa kuja kukusalimia.

BABA KILA SIKU ALIKUWA ANALALA NJE

Baada ya mkewe kusafiri, wiki ya pili tu jamaa akawa anaboreka chumbani akawa anaangalia TV sebuleni mwisho analala hapohapo mpaka asubuhi. Hatimae mkewe akarudi, kwa umbeya wake akamuita pembeni mdada wa kazi na kuanza kumsaili
MKE: Vipi mambo yalikuwa salama nilipokuwa safarini?
MDADA: Mambo yalikuwa safi tu
MKE: Baba hakukusumbua?
MDADA: Wala hakunisumbua
MKE: Baba alikuwa analala wapi?
MDADA: Mwanzo alikuwa analala ndani, baadae kila siku akawa analala nje
Mke kaanguka kwa presha

MTANI WANGU ATAKA KUNUNUA TV

Mdada mmoja kutoka lile kabila la watani zangu kaingia kwenye duka moja akaangalia kisha akamuendea muuzaji
MDADA: Niuzii ili tivi ili pali
MUUZAJI: Hebu sepa siuzii kitu chochote kabila lenu .....kesho yake mdada akaja kavaa wigi na sun glasiz kubwaa
MDADA: Niuzii ili tivii ili palii
MUUZAJI: Sepa nishakwambia kabila lenu siliuzii kitu hapa.
MDADA: We umijuaje kuwa mi ndii yuli wa jana?
MUUZAJI: Hiyo unayoiita  TV ni microwave, haya sepa

NAMFUKUZA KAZI HAUZGELO WANGU

Yaani kwa kweli sasa nimechoka, huyu hausgelo ni mvivu kupindukia, kwa hiyo nimeamua kumfukuza kazi. Hajua kupika, anafagia sehemu zinazoonekana tu, kufua ni mgogoro, anashinda anaangalia Bongomovies mchana kutwa, yaani ugomvi kila siku 'I am tired arudi kwao kijijini niliko mtoa kwisha, naenda kumnunulia tiketi.

DOKTA NIKASTRETI PLZ

SUPASTA:(Mwenye upeo mdogo wa Kiingereza lakini hakubali hilo) Dokta, how are you mshkaji?
DOKTA: I am okay
SUPASTA: Dok unajua I am supasta men, so Can you help me?
DOKTA: Hakuna tabu supasta.Unatakaje
SUPASTA: Nataka kufanyiwa ile operesheni ya Kastreshen
DOKTA: Du kwanini tena? Huoni utateseka?
SUPASTA:Unajua madem wananidistab men, so nataka nichenj, nitateseka kwa muda halafu ntainjoy life my men.
DOKTA: Ok haya japo sikuelewi
SUPASTA: We fanya men....Siku mbili baadae Sharo akiwa kitandani anauguza kidonda, akatembelewa na rafiki yake.
RAFIKI: Pole bwana wameshakusakumsaiz?
SUPASTA: Ndio nini?Si ulinambia niwambie wanikastreti
RAFIKI: Nilikwambia waku SAKUMSAIZ, siyo wakuKASTRETI???? Sasa ndugu yangu mbona umewaambia wakutengue sehemu?
SUPASTA: Duh mama yangu nimekwisha

4 November 2013

HILO JINA LA MTOTO NTAKAE MZAA

Musa akiwa na mkewe katika shughuli nzito ya kutafuta mtoto, maneno  ya ajabu ajabu yakimtoka kwa raha, mara akamsikia mkewe akitaja jina "John John"........zoezi likasimama ghafla kwa hasira
MUSA: John ndio nani?
MKE: Mume wangu samahanai nilikuwa nimeanza kufikiria jina la mtoto ntakae mzaa

BONGEEE YA DOMO


MBONA WEWE UNAVAA CHUPI?

Mr na Mrs walikuwa katika hali ya kununiana,
MKE: Naomba hela nikanunulie sidiria
MUME: Sidiria ya kufanyia nini? Matiti yenyewe huna
MKE: Mbona we unavaa chupi?

VUA CHONDE VUA UMEGEUZA KANDA MBILI VUA


Mtu na mkewe waliingia kibanda cha mganga wa kienyeji kutafuta dawa kwa ajili ya mbaba aliyekuwa hawezi kutimiza majukumu yake kama mume. 
MGANGA: Nina dawa nzuri sana ni kanda mbili ambazo zitamaliza tatizo lenu.
 MUME: Hiyo siamini, kanda mbili na tatizo langu wapi na wapi?........Mganga akatoa kanda mbili;
MGANGA: Vaa uone kazi ya mizimu, mama jitayarishe hapa lazima kieleweke,dawa hii ina nguvu sana... Jamaa ile kuvaa tu alipiga ukelele akamrukia mganga akaanza kumvua nguo mganga, mganga alijaribu kila njia kuponyoka ikawa ngumu, hatimae akaanza kupiga kelele;
MGANGA: Vua, vua, umegeuza kanda mbili mamaeee