WARAKA MUHIMU KWA WALEVI WAPYA...

Ndugu zangu wanywaji wapya wa pombe, kutokana na uzoefu wa muda mrefu wa  kulewa nimeona niwape ushauri ambao unaweza kuwapa majibu mtakapojikuta katika hali mbalimbali baada ya kufakamia pombe, urabu, ngumu kumeza na kadhalika.
Tafadhali ieleweke kuwa kuwa matatizo haya hutokea kwa pombe zote zilizohalali na zisizo halali;
1.   Unaamka ghafla unakuta kimya kikuu na giza zito- mara nyingi ni dalili za wazi kuwa umelala baa na wamekufungia, ni busara kutokupanik na kuendelea kulala mpaka watakapofungua kesho yake, kama umeoa au umeolewa ndoa yako iko pabaya.
2.   Unakuta kila mtu anakuangalia ana cheka – Je uko juu ya meza unacheza? Umejikojolea? Au miguu imekataa kufanya kazi. Au umevua nguo zote unajiita John Cenna? Ni bora uwataarifu wote wanaokuangalia kuwa wewe una pesa ndio maana umelewa mno, japo hilo litaalika vibaka wakuandame wakuvuruge.
3.   Unajikuta ghafla unatoka damu mdomoni na puani- ni dalili kuwa umepigwa, kikubwa ni nyamaza usianze kujitetea au kuonyesha kuwa umeonewa, utapigwa zaidi, we omba msamaha tu yaishe.
4.   Uko kwenye bar hukumbuki uliingia  saa ngapi na pia hakuna mtu unaemtambua, wala hata mtaa ulipo huelewi- Hii ni mbaya mtu wa Masaki unaweza ukawa uko Manzese, au unadhani uko kwa mji ulikozaliwa au pengine uko  Kinondoni kumbe uko Dar Live Mbagala, kuolewa ni rahisi sana katika mazingira haya, na hii haijalishi kama ni mwanaume au mwanamke kuna watu hawajali hilo wanaoa tu
5.   Unajikuta unalilia penzi la mhudumu- Hizi ni dalili mbaya ambazo zinaweza kukusababisha uje kupigwa tena, maana mara nyingi unajiona kuwa hakuna mwanamke mzuri kama huyo na uko tayari kuruka kung fu kwa ajili yake.
USHAURI: Mrudie MUNGU akusaidie uache pombe au utapigwa na kuolewa sana  

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.