HATUPIMI BANDO

18 October 2013

USHAURI WA BURE WA ANKO KITIME, AKA MHARIRI MTEGAJI WA BLOG HII

Ndugu Mhariri wa Chekanakitime blog aka Anko Kitime,
Nimeona niandike kwenye blog yako ili unisaidie katika tatizo langu, maana kwa kweli nimeona umesaidia wengi wenye matatizo kama yangu. Juzi nilikuwa naenda kazini nikamuacha mume wangu nyumbani anaangalia TV, gari langu likazima ghafla kiasi cha kilomita moja toka nyumbani. Nikaona nitembee mpaka nyumbani kumwomba mume wangu aje anisaidie kutengeza gari, kwa mshangao wangu nilipofika nyumbani nikamkuta mume wangu yuko na chumbani na msichana wa kazi wa nyumba ya jirani. Mume wangu ana miaka 43, mimi nina miaka 39 na msichana huyo ana miaka 19 hivi.Tumekuwa katika ndoa kwa miaka 10. Nilipomuuliza mume wangu alikubali kuwa uhusiano wao umekuwa ukiendelea kwa miezi sita sasa, nifanye nini mimi?.
Gulolia
Jibu
Dear Gulolia,
Hujambo? Mumeo hajambo? Nimesoma vizuri barua yako na naweza kukushauri ifuatavyo, kwa kusema ukweli gari kuzima ghafla linaweza likawa limesababishwa na mambo kadhaa, aidha betri haichaji, au petroli imekwisha au fyuzi imekatika Ni vizuri ukaanaza kuangalia kama filta ya petroli ni safi na jaribu pia kucheki plagi. Nategemea jibu hili litakusaidia
Anko Kitime

No comments: