PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

TANGAZO TUKITAMKA PLEJI KWENYE MICHANGO, AJE KUCHUKUA MUHUSIKA TU

Kumekuweko na tabia nzuri sana ya kuruhusu watu kuplej wakati wa kukusanya michango mbalimbali. Hii imewezesha kuwa mtu unaweza kupleji hata Milioni mia, mtu ukajijengea sifa au kama waBongo wanavyoita "Kuuza sura" Katika kipindi cha wiki chache zilizopita tumejifunza kitu cha msingi sana ambacho sisi kama vigogo wa blog hii feki tumeamua kuwa ni lazima tujifunze na kutekeleza kuanzia sasa. 
Sisi vigogo vya blog hii tunasema kuanzia sasa tukiplej mchango wowote, ni muhusika mkuu tu wa pleji na tena  atakuja akitembea kwa magoti ndio sisi tutaweza kutoa pleji yetu. 
Hivyo basi kama ni kikao cha harusi, plej tutakayotoa itakuja kufuatwa na Bwana harusi au Bibi harusi mhusika tu ndipo plej itatolewa. Tena aje akitembea kwa magoti. Kama ni plej ya msiba, ni marehemu tu aje mwenyewe achukue mchango huo na si mwingine.
 Hivyo basi mambo ya kumtuma sijui muweka hazina, sijui mhasibu haitasaidia. Hatutatoa kitu. Hivi mnajua maumivu ya kutoa mchango ulio pleji ni makubwa sana, mtu saa nyingine unaplej umelewa, au unakuta adui yako kaplej sasa we lazima upleji mara kumi yake hivyo kutoa huo mkwanja inauma sana. Kwa hiyo hatukubali kutoa kwa asiye muhusika.

Comments