HATUPIMI BANDO

3 October 2013

SPIDERMAN AKUTWA CHOONI LAIVU KUWA WA KWANZA KUONA HAPA

Wale wapiga picha wetu makini sana leo wamepata scoop, yaani bonge la sooo. Kumbe Spiderman mbwembwe zote za kuruka na kadhalika kumbe anaenda chooni peace kama watu wengine. Mwandishi wetu akini alikuwa bar moja kule Tandika Maguruwe akinywa kitu chake baada ya kupewa mshahara mnono na mabosi wa blog hii, ndipo alipotupa jicho kushoto hakuamini kabisa macho yake maana alichokiona hakikuwa cha kawaida, akimuona Spiderman anaingia chooni. Kwa kuwa mwandishi wetu alikuwa amekunywa bia tisa tu alijua kuwa kiukweli hajalewa, basi akawasha kamera yake ya simu, akanyata na kupata picha ya Spiderman akijisaidia bila matatizo wala nini. Nasi tumeona tuilete hapa hii picha maana ni wazi Spiderman kama msanii ni kioo cha jamii sasa tunajiuliza kwanini anenda chooni, yeye kama msanii haoni watu watamuiga kwenda chooni. Tunaomba vyombo vinavyoshughulika na sanaa waingilie jambo hili kwani ni baya kuliko yule mwanamuziki aliyenyonywa nanihii kwenye show kwa kisingizio cha kuwa ni mwanamuziki
Na Mwandishi Wetu

No comments: