HATUPIMI BANDO

2 October 2013

MPUMBAVU GANI HUYO ANANIGUSA?

Bonge ya ugomvi ulikuwa umezuka kati ya Henry na mkewe, kwa kisirani mkewe akamtukana mumewe,'Mpumbavu mkubwa'. Sasa hapo ndipo moto ulipowaka, Henry kaja juu, 'Mwanamke hawezi kuniita mimi mpumbavu, hata kama ni mke wangu leo lazima utoke humu ndani uende kwenu". Majirani wakaingilia na kubembeleza sana hatimaye ugomvi ukaisha amani ikarudia kiasi ndani ya nyumba, japo mtu na mkewe wakawa wamenuniana.
Usiku wakiwa kitandani hamu ikamjia Henry akawa anahitaji haki yake ya ndoa. Akamgusa bega mkewe, mke kwa hasira akauliza, 'Mpumbavu gani huyo ananigusa?'. Bwana Henry kwa adabu na upole wa hali ya juu akajibu, 'Ni mimi mpenzi'

No comments: