PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MALIZA BIA YAKO NTALIPA MIMI

Jamaa yangu Devi hana raha, amepanic, mchana leo alipigiwa simu na Bosi wake ambae alikuwa safari, yeye mwenyewe wakati huo alikuwa bar akipata moja moto moja baridi saa za kazi;
Bosi: Vipi Devi? Mnaendeleaje na kazi hapo ofisini?
Devi: Mkuu hapa mambo safi sana tuko bizi sana, watu leo wamekuwa wengi utafikiri wametumwa bosi, hakuna hata nafasi ya kupumua, ingekuwa tunaamini mambo ya uchawi tungesema Bosi wamekuloga ukiwepo watu wawe wanaikimbia ofisi
Bosi: Ok, Unaweza kunisaidia kitu kimoja?
Devi: Hakuna tabu  Mzee sema tu.
Bosi: Haya maliza hiyo bia yako, halafu nenda kaunta wambie bili yako wachanganye na yangu mi niko huku pembeni nasubiri mishkaki

Comments