PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

LEO TUNAGAWANA MAJENGO YA SERIKALI, YEYE MUHIMBILI MIMI SEGEREA

Mama mkwe kamkuta jamaa sebuleni kapandisha hasira anadai ataua mtu.
MAMKWE: Mwanangu kwani kuna nini jamani?
MJAMAA: Leo namuua mwanao, mshenzi sana?
MAMKWE: Tulia jamani kimetokea nini?
MJAMAA: Mwanao mshenzi nilikuwa nimesafiri, nikamtumia meseji kuwa nakuja, eti bado leo nimefika nimemkuta na mwanaume kwenye kitanda chetu dharau gani hii, sikubali leo tunagawana majengo ya serikali, yeye anaenda kulala Muhimbili mi naenda kulala Segerea
MAMKWE: Subiri kwanza mwanangu hayuko hivyo lazima kuna maelezo fulani kuhusu hili ngoja nimuulize...mama mkwe akamfwata mwanawe na baada ya muda akarudi sebuleni
MAMKWE: Unaona, nilijua mimi lazima kuna sababu. Kumbe mwenzio hakupata ile meseji uliyomtumia

Comments