PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KABILA GANI WABISHI ZAIDI TANZANIA?

Naambiwa kuna kabila moja ni wabishi hao hujapata kuona, wanaweza kubishana hata na taarifa ya habari kwenye redio au TV. Wakati wa enzi za Taifa Cup ambapo mechi zilikuwa ni kati ya mikoa, mechi iliyochezwa mkoani kwao ilivunjwa baada ya kukataa goli lililofungwa kwa kichwa, wapenzi walianzisha ubishi kuwa hawakukubaliana kabla ya mchezo kuwa watakuwa wanafunga kwa vichwa.
Nafanya utafiti ni kabila gani bishi hivi? je bado liko? je kabila hili katika enzi hizi za google haiwezekani kulitengenezea web yao wabishane na google? nawasilisha hoja.

Comments

Anonymous said…
a.k.a leka dutigite
Anonymous said…
jamaa walianza kubishana ndani ya treni third class kutoka Dar hadi mwisho wa reli, kwa vile walikuwa hawatazamani kwa jinsi viti vilivyopeana mgongo, walipofika safari wakati wanatoka kwenye behewa heh kumbe alikuwa mtu na mjomba wake...eh kumbe ni mjomba?!
Anonymous said…
Jamaa wa mwisho wa reli hushikiana ubishi mmoja akienda msalani, akirudi huuliza Hanzuruni umefikia wapi niendelee?