PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

DUH NUSU NIKAMATWE NA BOSI

Jamaa alikuwa akifanya kiwandani na kila siku alikuwa anafanya overtime. Bosi wake akamuita na kumsifu sana na kumuahidi akiendelea na moyo huo angemhakikishia kumpa cheo kikubwa katika muda mfupi na hata hisa katika kampuni. Jamaa akaongeza bidii na masaa ya kufanya overtime. Siku moja usiku akiwa katika overtime saa sita ya usiku TANESCO wakakata umeme, akaamua kutoroka na kurudi nyumbani kwake. Alipofika nyumbani kwake akakuta gari la bosi wake limepaki nje, giza likiwa limetanda akazunguka kwenye dirisha la nyumba yake ili amgongee mkewe, alipogonga sauti ya bosi wake ilitoka chumbani kwake ikisema,'Nani huyo?'. Jamaa akashtuka na kukimbia mbio kurudi kazini, akajisemea moyoni,' Dah nusura ningekamatwa na bosi'

Comments