HATUPIMI BANDO

31 October 2013

HAPANA YULE SHEMEJI YANGU

Mwanamke mmoja alifiwa na mumewe na baada ya muda mfupi akaolewa na shemeji yake, mdogo wa mumewe. Picha za mumewe zilikuwa bado zimetundikwa ukutani kwenye sebule yake, wageni wakifika wakimuuliza yule ndio mumeo, alikuwa anajibu hapana, yule shemeji yangu na amefariki muda si mrefu sana.

HAAA KUMBE UNA NYUMBA NDOGO

Baada ya uchaguzi wa serikali za mtaa mgombea karudi kwake amenuna.
MKE; Vipi matokeo?
MUME: Nimeangushwa vibaya
MKE: Umepata kura ngapi?
MUME: Kura mbili, najua moja yangu nyingine sijui nani sijui...
MKE: Mshenzi mkubwa kumbe una nyumba ndogo hapa mtaani leo utamtaja huyo mwingine

MAMBO YA KINYA MCHUNGAJI WA KIUME AMSUBIRI GEST KONDOO WA KIUME..VIDEO

HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA UNAONA ILE MAMBO IKO KULE KWA KENYA?

30 October 2013

DIA TICHA OF MY CHILDS

Ole wenu mnaopeleka watoto shule za Akademia toka nursery, mmama mmoja amelazimika kumuandikia mwalimu wa mwanae Kiinglish kama ifuatavyo-
Dear Ticha,
 Please I not like how you gived my children 2 over 10 in the english ekzam. I have look at the thing she write and, every thing correct well so what is the why that you now gived her 2 over 10. I am speak english every day and she has know it well, so please what is the why for small mark? What is the why.
Yourls, Hangry parent.

UZEE MWISHO CHALINZE


NINA MIMBA YAKO

MDADA: Nina mimba yako
MKAKA: Umeanza uwongo wako
MDADA: Haki ya Mungu tena
MKAKA: Ok nirudishie upesi

USUKANI UKO KUSHOTO NDUGU YANGU

Katika foleni gari moja likaligonga gari lililo mbele, dreva bonge bonge  wa gari lililogongwa akatoka haraka kwenye gari lake na kumtoa jamaa kwenye gari la lililogonga na kuanza kumpa kisago cha nguvu, alipoona ametosheka akaanza kumuuliza;
BONGE BONGE: Kwanini unaendesha gari kizembe?
ALIYENYUKWA: Unanionea bure, usukani wa hili gari uko kushoto ndugu yangu’

DAH KAZINI WATANISIFU SANA

Mume alisafiri aliporudi akamletea mke wake chupi mpya mke akaifurahia sana chupi ile;
MKE: Kazini watanisifu sana

NINGEKUFA MAMA ANGENIUA

Mtoto moja alikuwa anaishi kwenye nyumba iliyokuwa na muembe nje, kila siku alipenda kuupanda mti huo, na kila siku kulikuwa na ugomvi mkubwa na mama yake. Siku hiyo alipanda kwenye muembe huo akaanguka, bahati nzuri hakuumia sana. Akaamka na kumwambia rafiki yake, 'Nina bahati kweli ningekufa, mama angenipiga mpaka aniue'.

29 October 2013

CHEKANAKITIME YAAJIRI WATAALAMU WAPYA KABISA

Baada ya wataalamu waliopo kuonekana wameanza kiburi na zereu wanadai eti kampuni iwanunulie magari kama waandishi wa Ulaya, uongozi wa blogu umeona uwapotezee na kuajiri wataalamu waliobobea katika fani ya uandishi wa blogu za  kiukweli kama hii. Pichani ni wataalamu hao ambao majina yao tunaficha wasije wakalogwa na blogu pinzani, si unajua bongo hata blogu watu wanaenda kwa Wazee wa Busara

TOA NDUGU TOA NDUGU...VIDEO


HATA KWETU WAPOOO...VIDEO


GLORIA GANI HUYO?

MKE: Hello mume wangu, yamenikuta makubwa nashukuru Mungu niko hai. Nilikuwa naelekea kwa Gloria, gari likapata pancha na kuanza kuyumba likatumbukia kwenye daraja, nikajaribu kutoka nikashindwa kwa maumivu na mlango ulikuwa umejibana, bahati nzuri watu wamekuja kuuvunja mlango kwa mashoka wamenitoa na sasa niko hospitali.
MUME: Umesema Gloria? Gloria gani huyo?

BWANA WEE NIRUDISHIENI MIA TANO YANGU

Mjingamjinga mmoja alinunua tiketi ya bahati nasibu kwa shilingi 500 akashinda shilingi milioni 20. Haraka akaenda ofisi ya bahati nasibu, nao wakacheki na kukubali kuwa tiketi yake imeshinda.
Mjingamjinga: Haya nipeni milioni 20 zangu.
Bahati nasibu: Masharti ya malipo ni kuwa tunakupa leo milioni 5 na kila mwezi unakuja kuchukua milioni moja mpaka ziishe.
Mjingamjinga: Msinibabaishe nilipeni milioni 20 zangu
Bahati nasibu: Bwana hiyo ndiyo sheria yetu
Mjinga mjinga: Bwana e kama ni hivyo basi chukueni kitiketi chenu nirudishieni mia tano yangu wajinga wakubwa.

27 October 2013

TUNGA SENTENSI KUTUMIA NENO MKUU

TICHA IRENE: haya nani atunge sentensi kutumia neno MKUU
DINA: Rais ni MKUU wa nchi
TICHA IRENE: Safi haya Dogo
DOGO: Jana nilikuona wewe na Mwalimu MKUU mnaingia gesti.
TICHA IRENE: Toka darasani kwangu

SOV KITENDAWILI HIKI

Wamama wawili walijikuta magari yao yamegongana. Wakashuka kwenye gari wakaanza kutoleana kashfa, hasa yule aliyekuwa na vogue akamtukana sana mwenye Kivitz, japokuwa ndie aliyekuwa na makosa. Mwenye Kivitz akampigia mumewe simu.
MAMAKIVITZ: Mume wangu ninatatizo
MUME: Jamani niko bizy mkutanoni hebu lisov mwenyewe
MWENYE VOGUE akasema anampigia boy friend wake ndiye atakae ongea.
MWENYE VOGUE: Darling kuna mjinga mmoja kagonga gari uliloninunulia, please njoo.
Muda si mrefu jamaa akaja, kumbe alikuwa ndiye mume wa MAMAKIVTZ......kila mtu amalizie sinema hii

JE NDOA NGAPI ZA KIDIJITALI ZITAPONA?


Hivi serikali yetu sikivu ikitulazimisha kuwa ifikapo kesho asubuhi, kila mume na ampe mkewe password yake ya facebook na ya whatsapp na vivyo hivyo kila mke na ampe mumewe. Je ni wangapi wataona ni heri ndoa ife? Na pia kila waliomo katika penzi wabadilishishane password hizo, wangapi wataona heri penzi life? Comment

ETI NOVIDA HAKUPAFOM?

Blog hii tata bado inafanya uchunguzi kujua huyu mdada wa hapa Sinza aliyeenda kwenye tamasha kubwa jana ana maana gani. Anadai umeme ulikatika kabla NOVIDA hajapafom

23 October 2013

VICHWA VYA HABARI TODAY

 Njomba chacha hii kiboko unakuja Tanjania kuangalia Panya Buku? Tunajua njomba unapenda chamaki nchanga lakini hii chacha imechidi kipimo, kwani Nchumbiji hakuna Buku?

Bado mhariri anapeleleza kana kuna hii kitu inaitwa Funs Club, shuleni kwake alijifunza Fans Club, ila si vizuri kupinga wahariri

MBINU ZA KUCHAGULIWA KATIKA KAMATI TENA NA TENA

Siku hizi kila siku zinaundwa kamati za kila aina aina kwa matukio mbalimbali, yaani mpaka maudhi ene wey kuna siri kubwa ya kuonekana unafaa katika kamati zinazoundwa:-
  i. kamwe usiwahi kwenye vikao, ni dalili ya kuwa wewe si mzoefu wa vikao
  ii. Usiongee kitu mpaka mkutano ufikie japo  nusu, hili litakufanya uonekane una busara ya kusikiliza kwa makini kinachoendelea kabla ya kutoa uamuzi
iii. Unapo amua kuongea, hakikisha hakieleweki sawasawa hii itakufanya usiwe na ugomvi na mtu yoyote
iv. Ukiona kuna swala gumu na huna jibu, anzisha hoja ya kutengenezwa kwa kamati ndogo ya kushughulikia tatizo hilo, hapo utaonekana una busara japo kwa kweli wazo lako ni utumbo mtupu
v.Uwe mtu wa kwanza wa kutoa hoja ya kuahirisha kikao. Hii itakufanya upendwe na kila mtu maana wanakamati wote hutaka kikao kiishe lakini wanaogopa kusema


22 October 2013

MASHINE YA KUPIMA UJINGA YAINGIA NCHINI

HATIMAYE SERIKALI ILE SIKIVU IMESIKIA KILIO CHA WANANCHI NA KUNUNUA MASHINE ZITAKAYOWEZESHA KUTUMIKA KUPIMIA KIWANGO CHA UJINGA KATIKA SEKTA, KAMPUNI NA WIZARA MBALIMBALI. KWA KUANZIA KUNA MPANGO MKAKATI WA KUPIMA WAENDESHA BODABODA WOTE, ILI KUWA NA TAKWIMU YA KIWANGO CHAO HII ITASAIDIA KATIKA KUTAFUTA MBINU ZA KUPUNGUZA TATIZO LAO LA KUPIGA HONI OVYO. HII ITAFUATIWA NA MADEREVA WA VIBAJAJ NA HATIMAE DALADALA. BAADA YA HAPO MASHINE ITAHAMIA KWA WALE WASANII WANOONGOZA KWA KUCHEZA UCHI KWA KISINGIZIO CHA KUWA ETI WANAPAFOM MUZIKI. KUTOKANA NA UNYETI WA WATU WENGINE VIPIMO VITAFANYIKA KIINTELIJENSIA

WAKUNYUMBA SUBIRI HUJAFIKA CHUMBANI KWAKO

Binamu yake Gulo kutoka kulikuli kwa watani zangu alipata pesa baada ya kuuza tumbaku akaamua aje Dar akatanue. 
WAKUNYUMBA: Webwanawi nipelek kwenye hoteli ya gharama, natak kwenda kula bata.  Akapelekwa. Akaandikisha chumba bei shilingi alfu 60 kwa siku, akalipa na kuanza kusindikizwa na mhudumu wa hoteli ile kuingizwa kwenye lifti tu akaanzisha vurugu;
WAKUNYUMBA: Hamuwezi kunifanya mi mjingi bwana. Nimilipa alfu stini mnanip kichumbi kidogu hivi? Ntamchinj mtu sas hivi.
MHUDUMU: Mzee subiri punguza ukali, tuko kwenye lifti hatujafika kwenye chumba chako BADO

KAMA HUJUI JIBU NDIO UNAKUWA MKALI HIVYO?

Siku hiyo simba aliamka na kisirani, akamkuta nyani kwa ukali sana akauliza,'Nani mfalme wa wanyama wote?', nyani akawahi,'Simba". Simba akakutana na ng'ombe,'Wewe nani mfalme wa wanyama wote?', Ng'ombe akajibu kwa upole,'Simba'. Hatimae simba akakutana na tembo, akamuuliza naye,'We Bigi nani mfalme wa wanyama wote?', Tembo akamkamata simba akambamiza kwenye mti kama mara tatu hivi kisha akamkanyaga simba akawa hoi, lakini kabla hajapoteza fahamu Simba akasema kwa unyonge,' Sasa ndugu yangu kwa kuwa hujui jibu ndio uwe mkali hivyo?'

TEMBEA NA NGUO ZA NDANI SAFI KUNA MSAKO OHOOO


HAYAKUHUSU

MKE: Naomba tuongee
MUME:Ongea
MKE: Ni kuhusu huyu hausgel wetu
MUME: Hilo ni tatizo lako halinihusu
MKE: Ana mimba
MUME: Hilo ni tatizo lake halituhusu
MKE: Kasema yako
MUME: Hilo ni tatizo langu halikuhusu

MAGAZETINI LEO.....UKIBISHA UTAPIGWA TU

Inaonekana kulikuweko na Press Conference kuhusu pato la Taifa, haya ndio maelezo ya waandishi wetu.
1.
Shughuli za uvivu zilikuwa kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na asilimia 6.5 kwa mwaka jana....kama unabishwa UTAPIGWA TU.
2.
Pato la Taifa mwaka huu ni shilingi milioni 5 ikilinganishwa na shilingi 4.6 milioni kwa mwaka jana...kama unabisha UTAPIGWA TU


21 October 2013

CHEZEA MSWAHILI WEWE


I AM HALF CASTE

YAMENIKUTA....Jana nilienda Karaoke pale Nyumbani Lounge, nikakutana na kabinti ka nguvu;
MZEE MZIMA: Hi mambo binti
KABINTI: Okay, ahh Mzee nanihii uko humu?
MZEE MZIMA: Yaa nawasikiliza mnavyoimba, we unajua kuimba?
KABINTI: Yah, its in my blood
MZEE MZIMA: Kwani we mwenyeji wa wapi?
KABINTI: Mi half caste
MZEE MZIMA: Kivipi?
KABINTI: Mamangu Mtanzania baba yangu Mganda
MZEE MZIMA : Okay

PAMOJA NA KUVAA KONDOM, JAMAA KAFA

Ile dhana ya kuwa Condom huzuia kifo imefeli kabisa katika tukio lililomtokea rafiki yangu karibuni. Rafiki yangu akiwa kavaa condom kafumaniwa na mke wa mtu, amepewa kipigo kitakatifu na kupoteza maisha licha ya kuwa alivaa condom.

MI SIJAIBA SIKU ZAKO

Msela kapata bonge ya zali, binti mzuri kampenda akamkaribisha waishi wote. Maisha yakawa matamu, mapenzi motomoto, hatimae binti akagundua kawa mja mzito akaamua kumtarifu msela;
BINTI: Mwezio sizioni siku zangu
MSELA: Umesema nini wewe? Naona umeshanichoka sasa, tayari umeanza kunihisi mi mwizi? Nakubali ulinikuta na shida lakini mie si mwizi utakuwa umezipoteza mahala pengine

20 October 2013

OYAA USIVUE WEWE

DOKTA: Haya dada tumekupima karibu kila kitu, presha safi, huna kisukari,figo safi, sasa hebu tuone kale kasehemu ambako nyie wakinadada huwa kanawaletea kila aina aina ya matatizo.....Mdada akaanza kuvua nguo;
DOKTA: He vipi tena? Mi nataka kuona ulimi wako tu

TIMU YAPATA TUZO LA CHEKANAKITIME KWA KUONDOLEA WATU STRESS
Tuzo la nanihii ya dhahabu
Blog hii leo imeona itoe tuzo la Chekanakitime kwa timu iliyofanya kitendo cha uzalendo wa hali ya juu  kwa kukwepesha stress, majonzi na vifo vya maelfu ya wapenzi wa timu pinzani, kwa kujitolea kuachia timu pinzani kupata draw.
Timu hiyo ambayo ilikuwa tayari mbele kwa magoli kadhaa iliamua kucheza kizembe katika nusu ya pili ili kuruhusu timu pinzani kurudisha magoli. Kitendo hiki cha kizalendo kimepelekea blog hii kuipatimu hiyo tuzo hilo ambalo ni ngao ya nanihii ya dhahabu.

18 October 2013

SABUNI YA KUZUI UCHAWI..WASILIANA NA MABOSI WA HII BLOGU


LAIV LEO TOKA KWENE UWANJA WA MAOMBI

MDADA: E Bwana  tuma malaika wako wanisaidie nipate mume mapema, lakini vunja vunja nguvu zote za giza zitakazosababisha nipate mume mfupi, tengua mipango yote ya adui kuniletea mume mfupi....Jirani kulikuwa na bwana mfupi sana nae anaomba.
FUPI: E Bwana asante kwa kunifanya bilionea asante sana Bwana sasa naomba mke, naomba mwenza wa kutumia nae mali hii uliyonipa
MDADA: Bwana naona umesikia ombi langu, nisamehe kwa kujidai nachagua mume, hata huyu jirani atanifaa tu, asante sana

TANGAZO TUKITAMKA PLEJI KWENYE MICHANGO, AJE KUCHUKUA MUHUSIKA TU

Kumekuweko na tabia nzuri sana ya kuruhusu watu kuplej wakati wa kukusanya michango mbalimbali. Hii imewezesha kuwa mtu unaweza kupleji hata Milioni mia, mtu ukajijengea sifa au kama waBongo wanavyoita "Kuuza sura" Katika kipindi cha wiki chache zilizopita tumejifunza kitu cha msingi sana ambacho sisi kama vigogo wa blog hii feki tumeamua kuwa ni lazima tujifunze na kutekeleza kuanzia sasa. 
Sisi vigogo vya blog hii tunasema kuanzia sasa tukiplej mchango wowote, ni muhusika mkuu tu wa pleji na tena  atakuja akitembea kwa magoti ndio sisi tutaweza kutoa pleji yetu. 
Hivyo basi kama ni kikao cha harusi, plej tutakayotoa itakuja kufuatwa na Bwana harusi au Bibi harusi mhusika tu ndipo plej itatolewa. Tena aje akitembea kwa magoti. Kama ni plej ya msiba, ni marehemu tu aje mwenyewe achukue mchango huo na si mwingine.
 Hivyo basi mambo ya kumtuma sijui muweka hazina, sijui mhasibu haitasaidia. Hatutatoa kitu. Hivi mnajua maumivu ya kutoa mchango ulio pleji ni makubwa sana, mtu saa nyingine unaplej umelewa, au unakuta adui yako kaplej sasa we lazima upleji mara kumi yake hivyo kutoa huo mkwanja inauma sana. Kwa hiyo hatukubali kutoa kwa asiye muhusika.

WABONGO WACHAWI SANA, wameondoa nanihii.............

Mdau mmoja katuletea hii picha akidai mdada pichani alikuwa kaenda chooni hakikutoka kitu, kumbe watu wamemloga wameondoa pale pa kujisaidia alijaribu kupatafuta ikashindikana. Alishauriwa atumie njia ya Big Results Now....ambapo kule bagamoyo kuna wataalamu wangesov tatizo lake.

DOGO UMECHEZA MNO DOGO


HUYU ANATAFUTA UMAARUFU TU


NDUGU ANKO KITIME NAOMBA USHAURI

Ndugu Anko Kitime aka Mhariri Mtegaji wa Blog, tafadhali nipe ushauri katika hili tatizo langu.
 Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi katikati ya jiji letu la joto hili, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi na taxi, wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu yake alikuwa mkali kwelikweli, nilidhani ataniua. Ni kweli sijawahi kumuuliza kuhusu wasiwasi wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, wakapanda taxi nami nikawafuata  na wakaishia kuingia kwenye gest moja pale Kinondoni Mosko, nikaona ni vizuri niangalie saa nijue ni saa ngapi wameingia mle kwani itanisaidia katika ushahidi wakati wa kesi hapo baadae, si ndio nikagundua saa yangu imesimama, saa hii ni Rolex na nilipewa na bosi wangu mzungu kazini alinunua kwao huko Uswisi, na ni expensivu sana, kiukweli nilichanganyikiwa ntamwambia nini mzungu wangu? Si ataniona sina akili nimeharibu saa aliyonipa kirahisi kabisa?  sasa je, unanishauri nimrudishie bosi akaitengeneze kwao? au ni bahatishe mafundi wetu wa Bongo?

USHAURI WA BURE WA ANKO KITIME, AKA MHARIRI MTEGAJI WA BLOG HII

Ndugu Mhariri wa Chekanakitime blog aka Anko Kitime,
Nimeona niandike kwenye blog yako ili unisaidie katika tatizo langu, maana kwa kweli nimeona umesaidia wengi wenye matatizo kama yangu. Juzi nilikuwa naenda kazini nikamuacha mume wangu nyumbani anaangalia TV, gari langu likazima ghafla kiasi cha kilomita moja toka nyumbani. Nikaona nitembee mpaka nyumbani kumwomba mume wangu aje anisaidie kutengeza gari, kwa mshangao wangu nilipofika nyumbani nikamkuta mume wangu yuko na chumbani na msichana wa kazi wa nyumba ya jirani. Mume wangu ana miaka 43, mimi nina miaka 39 na msichana huyo ana miaka 19 hivi.Tumekuwa katika ndoa kwa miaka 10. Nilipomuuliza mume wangu alikubali kuwa uhusiano wao umekuwa ukiendelea kwa miezi sita sasa, nifanye nini mimi?.
Gulolia
Jibu
Dear Gulolia,
Hujambo? Mumeo hajambo? Nimesoma vizuri barua yako na naweza kukushauri ifuatavyo, kwa kusema ukweli gari kuzima ghafla linaweza likawa limesababishwa na mambo kadhaa, aidha betri haichaji, au petroli imekwisha au fyuzi imekatika Ni vizuri ukaanaza kuangalia kama filta ya petroli ni safi na jaribu pia kucheki plagi. Nategemea jibu hili litakusaidia
Anko Kitime

NIKICHELEWA NTAKUTA BAGIA ZIMEISHA

Mtoto ambaye kwa kawaida ni mvivu kuamka kwenda shule, siku hiyo akaonekana alfajiri analilia kwenda shule; BABA: We vipi leo mbona unawahi namna hii kwenda shule? DOGO: Mwalimu anaeuza bagia leo anakuja asubuhi, nikichelewa nitakuta bagia zimeisha

16 October 2013

JUMA MBONA UNARUSHA NGUMI?

 Juma alikuwa anajifanya anajua sana kutania watu. Siku hiyo akamkuta rafiki yake Jaks kakaa ana mawazo akamshika shavu na kumtania kuwa ana shavu  laini kama tako la mke wake, Jaks akajishika shavu lake, kisha akawa kama anatafakari na kusema bila ukali,’Aise kweli bwana Juma, nilikuwa sijagundua na mimi sasa nakubali ni kweli shavu langu linafanana ulaini na tako la mkeo’ Eti Juma akaanza kurusha ngumi

HAYA NENDA KAFLASH CHOO SASA

Mzee mmoja bingwa wa kubana matumizi, aliyekuwa anafuatilia matumizi ya kila kitu nyumbani kwake, alikuwa na taratibu ya kuiita famili yake kila siku usiku kabla ya kulala kisha anaanza kumuuliza mmoja mmoja;
MZEE: Mke wangu umeshashusha?
MKE: Ndiyo
MZEE: Dogo umeshashusha?
DOGO: Ndio
MZEE: Dada umeshashusha?
DADA: Ndio
MZEE: Mlinzi umeshashusha?
MLINZI: Ndio
MZEE: Haya sasa mlinzi nenda ukaflash choo.

HELA HANA KACHANGANYIKIWA KABISAAA


Jamaa yangu kenda hospitali kagundulika ana cerebrocerebelloencephalotrigeminomedulloangiomatosis, ambayo imetokana na kuwa na tatizo la awali la pneumoconiosiliconosarcoidohistoplasmocryptococcitis, hii imepelekea kuwa na tatizo jipya la gastroenteroproctoentamoebovibrioescherichiosis. Halafu hela hana KACHANGANYIKIWA KABISAAA

SIMBA ANATISHA BWANA

MTANGANYIKA:Leo nimeponea chupuchupu kuuwawa na simba
MBONGO: He ilikuwaje?
MTANGANYIKA: Nilikuwa nimechuchumaa najisaidia nyuma ya chaka simba akatokea ghafla
MBONGO: Sasa uliponaje?
TANGANYIKA: Nakwambia kama sio simba kuteleza teleza ningekuwa marehemu.
MBONGO: E bwanaee hapo ningekuwa mimi kwa vyovyote ningejiharishia hovyo
TANGANYIKA: Unafikiri simba alikuwa anateleza kwanini? We acha bwana simba anatisha bwana

VEROSSA LANGU MWENYEWE NIMEPEWA BUREEEE

Dah mambo mengine bwana, juzi nilipita pale Sinza darajani nikielekea home nikaona mfuko umetupwa, kuuangalia ndani nimekuta dola 20,000. Niwe mkweli woga ulinishika nikaangalia kushoto na kulia nilipoona watu hawanioni nikachukua ule mfuko na kwenda haraka home. Nilipomwaga kila kitu nikakuta vitambulisho, kadi za ATM, makaratasi mengi na iphone, nilitaka kuzima simu nitoe sim kadi lakini nikaacha roho ikanisuta kuwa mwenye mali anaweza akanipigia. Na kweli baada ya muda si mrefu simu ililia na kwa maelezo ikawa wazi mali zile ni za aliyepiga simu, nikamuelekeza niliko akaja kuchukua mzigo wake akanipa dola 2000 nikakataa kistaarabu, akachukua namba yangu akaondoka. Jana akanipigia simu kuwa yuko nje ya nyumba yangu alikuwa kaja na VEROSSA mpya kabisa, akanipa ufunguo na kuniambia hiyo ni zawadi yangu kutokana na tabia niliyoonyesha. Nikamshukuru sana wala sikuamini macho yangu, ile nataka kuwasha gari nilitest si nikasikia,'Baba baba amka chakula tayari'

ZEREU ZAKO ULIPOKUWA MTOTO ZITAKUKOSTI UKIWA MKUBWA


ITAKUWAJE MWAKA 2020


KAAZI KWELIKWELI MBOMBO NGAFUU

Mshikaji alijikuta yuko mahakamani kwa kosa la kuiba gari. HAKIMU: Mshtakiwa unamaelezo yoyote? MSHKAJI: Mzee, hawa jamaa wamenibambikia kesi, ishu nzima ilianza nilipokuwa pale masikani kwetu naosha magari kama kawa. Yule maza pale akaja na ndinga lake la nguvu, akaniambia nilioshe, mi nikalipiga maji kisawasawa, huyu maza akanambia niiingie kwenye gari yake kuna ishu muhimu, akanichukua mpaka pale Mwenge, akaniambia nichague viwalo, nikachagua nguo za nguvu akalipa, akanambia nimsindikize home kwake, tukasepa, nikafika kwake, mjengo wa nguvu, akanambia nioge nikaoga fresh, ile natoka bafuni akanipa msosi wa nguvu nikashushia na mzinga wa Nyagi, kisha akaniita chumbani kwake, akasaula akajitosa kitandani, kisha akanambia, MAZA: Mpenzi nimekupenda sana, nimekuridhia kila kitu, chukua unachotaka.  Basi kusikia hivyo mzee wangu nikacheki kushoto , nikacheki kulia nikaziona funguo za ndinga lake, nikaona poa ngoja nichukue mkoko. Nikachukua nikasepa, sasa hawa polisi wanasema nimeiba gari how kam mzee wangu? HAKIMU: Kaaazi kwelikweli mbombo ngafu.

HAPA NI DRY CLEANER SIYO DUKA LA NGUO TAFADHALI

Masupasta wawili maarufu walikuwa wanazunguka kwenye maduka mjini wakiingia kila duka na kuonyesha vimbwanga kuwa wao ni masupasta. Wakaingia duka moja wakaangalia nguo zilizotundikwa kwenye henga, hatimae wakaanza kuzijaribu kwa mbwembwe, na kubishana na wahudumu wote waliotaka kuwashauri, japo tayari nje ya duka lile watu walianza kukusanyika wakiwashangaa, wao wakaona huo ndio ujiko wenyewe. Hatimae mwenye duka akaja,' Samahani tunawaomba muache kujaribu nguo za watu, Hapa ni Dry Cleaner siyo duka la nguo?'

KOSA LA KWANZA TALAKA YA NINI?

Jamaa kamfumania mkewe;
JAMAA: Yaani mke wangu unanifanyia hivi mimi? Kitu gani nimekukosea?
MKE: Mume wangu najisikia aibu kubwa sana, nimekutendea kitu kibaya sana, naomba unipe talaka upate mtu mwaminifu
JAMAA: Ngoja kwanza mbona umefika mbali sana? Kosa lenyewe ni la kwanza talaka ya nini?

12 October 2013

MAMA MBONA BABA ANA KIPARA?

DOGO: Mama mbona baba ana kipara?
MAMA: Baba yako ana mambo mengi kichwani, anawaza tutakula nini, tutalala vipi, ada ya shule, kazi na mambo mengi ya kutusaidia
DOGO: Sasa mbona wewe una nywele nyingi

VICHWA VYA HABARI...LEO KUNA WATU WAMERUHUSIWA KUCHAPWA KILA SIKU

 OKAY IMERUHUSIWA WACHAPWE KILA SIKU OKAY

 KIZIMBANI KWA BANGI UNATAFUTA NINI WE NANDO, HUWEZI KWENDA KIZIMBANI KWA JOHN UKAKAA HUKO?

BINDING BLOOD SUGAR, CHECK URGED au BINDING BLOOD SUGAR CHECK, URGED AU .........................

ATHANTE NA WEWE

Jamaa alikuwa kwenye basi wakawa wanapita kwenye mji mmoja akamuuliza binti waliyekuwa wamekaa kiti kimoja;
JAMAA: Hapa panaitwaje?
BINTI: Thame
JAMAA: Asante
BINTI: Athante na wewe

MUME WANGU KUANZIA REO NI RAZIMA UJIPIKIE NA KUJIFURIA MWENYEWE HARI NDIO HIYO

Mkutano wa mwaka wa Chama cha Walioolewa Duniani (CHAWADU) ulikuwa inaendelea, na akina mama kutoka nchi mbali mbali walikuwa wanatoa ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa mwaka uliopita;
MAMA UK: Baada ya maazimio ya mkutano wa mwisho kuwa lazima waume zetu waanze kujipikia  wenyewe, nilipofika London nilimueleza mume wangu maamuzi hayo, siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili pia sikuona kitu, siku ya tatu akaelewa kuwa niko serious, mwenyewe aliingia jikoni na kuanza kupika (Makofi na vigelegele)
MAMA USA: Baada ya maazimio ya mwaka jana niliporudi Boston, nilimwambia mume wangu kuwa sitampikia wala kumfulia tena. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili alifua nguo chache, siku ya tatu mwenyewe alifua nguo zote pamoja na zangu na akaingia jikoni kupika (Makofi vifijo na vigelegele)
MAMA TZ: Baada ya maazimio ya mwaka jana, niriporudi kwetu Musoma, nikamwambia mume wangu kuanzia reo, razima ujipikie mwenyewe, ufue nguo zako mwenyewe, ufagie nyumba na kutandika kitanda mwenyewe, tumeshaamua na hata wazungu ndio wataenderea kufanya hivyo kwao. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili sikuona kitu, siku ya tatu sikuona kitu, siku ya nne kwa mbari nilianza kuona kwa jicho ra kushoto, maana uvimbe usoni urianza kupungua, ira jicho rangu ra kuria mpaka reo bado rinatoa machozi harijapona sawasawa 

11 October 2013

NA WASIWASI NA ELIMU YAKO

NDUGU MSOMAJI...............Je wewe ni msomi? Je, wewe hukuwa unatoroka darasani? Je , wewe hukua unalala usingizi darasani? Kama kweli ulihudhuria shule yako vizuri tafadhali nitajie neno au maneno ya Kiswahili yanayoishia na  fo, ukiacha Kifo, vifo, na fofofo

TAARIFA YA NAIBU MHARIRI WA BLOG HII KWA VYOMBO VYA KUPIKIA, NA VYOMBO VINGINE VYA MUZIKI NA VYOMBO VYA UJENZI


Napenda kuufahamisha wananchi wote wa blog ya Chekanakitime kwamba mimi ndiye niliyeruhusu taarifa hii ichapishwe katika tovuti hii. Kama hata hii nayo ni tovuti.
Ninalazimika kutoa ufafanuzi kwa njia hii maana tayari wadaku mmeanza kuuliza eti mbona Mhariri Mkuu alisema mi nisiwe nachapisha taarifa kwenye vyombo vya kupikia na mi eti nachapisha?
Kiukweli kuna watu waliniomba niwe nachapisha  ishu zangu hizi zisizo na kichwa wala mguu basi tukakaa nao kikao si wakaniomba wee wakaniomba wee, nikaona heri niwahurumie nichapishe, sasa kumbe nikawa sijamwambia Mhariri Mkuu. Kwa sababu nilisema nitamwambie kesho, ndio maana maona kama tunasigana sisi hatusigani ila wote tuna kubaliana kuwa nisiachapishage ila mimi niliombwa tu nichapishage ndipo nikachapishaga, Mmeonaee

SHOSTI KWANI KWAKO KUNA VITA?

Mama mmoja mdaku wa kutupwa alikuwa akimuona Mchungaji anaingia kwenye nyumba ya jirani yake kila siku, akashindwa kujizuia akamfwata mwenzie; 
Mama Udaku: Jirani mambo? 
Jirani: Poa 
Mama Udaku: Jirani kila siku namuona Baba Mchungaji anaingia kwako vipi anakuja kukuombea? 
Jirani: Shoga tafadhali achana na mimi. Kwako kila siku kuna Mwanajeshi anaingia, kuna vita kwako? Nijibu, Kwako kuna vita?

WE FALA NINI ANGEKUWA NA NJAA SI NINGESHALIWASungura na Simba waliingia hotelini. Weita akaja kuwasikiliza,
SUNGURA: Nipe majani kidogo na karoti nyingi pembeni
WEITA: Vipi rafiki yako?
SUNGURA: Hali kitu
WEITA: Vipi hana njaa?
SUNGURA: We fala nini angekuwa ana njaa mi siningekuwa marehemu tayari

BLAZAA WAMEKUIBIA DEMU WAKO

Jamaa alikuwa bizi anafanya mazoezi kando ya barabara, baada ya jogging na kuruka kichura akaamua kupiga push up. Wakati anaendelea na push up, mlevi moja akiwa njwiii akamsogelea na kumuangalia kwa makini kisha akamwita;
Mlevi: Blaza, blaza, subiri kidogo blaza, hapa ni sehemu hatari.
Jamaa: Nini tena wewe mlevi?
Mlevi: Okay mi mlevi lakini nilitaka kukujulisha naona unananihii peke yako, vibaka wamekwisha kuibia demu wako, angalia mwenyewe hapo chini

SAMAHANI KUNA MASWALI ANDIKENI COMMENTS


AISE WE UNA BAHATI SANA SANA

Jamaa kagongwa na baiskeli, mwendesha baiskeli akaanza kumnyanyua jamaa; MWENDESHA BAISKELI: Aise una bahati sana JAMAA: Umenigonga na baiskeli halafu unanambia nina bahati MWENDESHA BAISKELI: Ni kweli una bahati sana, maana kwa kawaida huwa naendesha daladala

10 October 2013

TOTO NJULII KULA UPECHII

Bikizee kasikia ‘Izrail mtoa roho’ anasaka vizee zaidi akaona ajifanye mtoto mdogo ili asipatikane. Akaanza kula vyakula vya kitoto na kuongea kitoto. Siku moja wakati anakula Celelac, Izrail akamshukia.
IZRAIL: We unafanya nini?
BIKIZEE: Atula nyamnyam
IZRAIL: Haya tula upechi toto njuli alafu twende atembea mjiniii achikia?

NGOJA NIJIFICHE HUKU


NIMEOTA NIKO NA OBAMA PALE TWITTER PUB KINONDONI


Dah ndoto nyingine bwana, ghafla si nikajiona nimeingia Twitter Pub mitaa ya Kinondoni A, nikajisogeza kaunta kulikuwa kama watu watatu mmoja akiwa kahegamia kaunta anashusha safari huku pembeni kalaza Kikonyagi, nikamsogelea, nikashtuka kidogo maana jamaa anaekunywa huo mchanganyiko wa safari na Konyagi nilikuwa kama namfananisha, halafu akili yangu ikanambia haiwezekani. Nikamcheki tena nikakuta sasa kawasha fegi yaani jamaa kafanana kila kitu na Obama. Akili ikanambia Obama atatafuta nini huku Kino, ila kwa kweli watu wamefanana , nikaaagiza kakinywaji kangu, nikaona nimchokonoe jamaa ili kumwambia anavyofanana na yule mshkaji wa Marekani. Nikaanza
MIMI: Vipi Mheshmiwa
JAMAA: Hi…ebwanaee hata sauti kama jamaa
MIMI: Naona upo unamawazo
JAMAA: Pardon?
MIMI: Ahhh it is you it like Obama in the face.
JAMAA: I am Obama and who are you?
MIMI: My name is Joni
JAMAA: Great, you have a great place here, I came to relax  I just  have too much in my mind presently…sasa hapa akawa kaniacha kabisaaaa
MIMI: Yes yes
JAMAA: Do you know the Republicans?
MIMI: Yes my kantry is Republic of Tanzania is vere nice
JAMAA: The Republicans are giving me a headache
MIMI: Vere nice, the Plezdent of Republic is Mr J Kikwete……..sasa nikashangaa naona mwenzangu kaanza kukasirika,ndo tatizo la kuchanganya konyagi na safari, lazima utavurugwa, nikaona nijitose nimwage kizungu unaweza kukuta zali tu, akanambia turudi kwao wote
MIMI: You like Repulicans of Tanzania it is many animals in Arusha and Mikumi, and the womens of Republic is very nice.Hehehehehe
JAMAA: Something is wrong with you Brother, I am just telling you I had to escape here just to relax from Republicans and you keep on saying Republicans are good, shucks you crazy or something
MIMI: Yes yes Republic of Tanzania vere good sir Obama
Ndipo hapo akanirushia kibao nikashtuka na kujikuta kumbe ilikuwa ndoto tu. Kuna haja ya kujifunza kingleza, hizi ndoto za Kingleza mbona zinakuwa soo.


BABA YAKE NI WEWE

MUME: Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, hataki shule yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie, kiukweli halitabadili mapenzi yangu kwako.
MKE:(Huku akipiga magoti) Mume wangu najisikia vibaya naomba unisamehe ni kweli huyo mtoto baba yake ni tofauti na wenzie
MUME: (Machozi yakimlengalenga) Dah mke wangu... baba yake ni nani?
MKE: Baba yake ni wewe.

MLETENI YULE DEMU MWENYE JINO BOVU

Jamaa kaingia bar kakuta kibao kaunta
;;;BIA BURE MWAKA MZIMA KWA ATAKAYEWEZA SHINDANO LETU;;;;;; akamuuliza kaunta kuhusu lile tangazo akaambiwa masharti yenyewe ni kuwa kwanza anywe dumu zima la gongo bila uso wake kuonyesha makunyanzi, kisha aingie chumba chenye mamba ambae anaumwa jino na kuling'oa halafu apande gorofani kuna chumba yuko mwanamke mmoja mkorofi sana amshughulikie.
JAMAA: Duh gongo dumu zima si uchizi huo.
Basi akaendelea kunywa bia zake zilipomkolea akamwambia kaunta hebu leta lile dumu la gongo. Akalinywa bila kukunja uso japo machozi yalikuwa yanamlenga. Alipomaliza akafunguliwa chumba chenye mamba akaingia, kukasikika kelele vurugu hatimaee kimya kikatawala, ile watu wanataka kwenda kufungua mlango wakijua jamaa atakuwa kaliwa na mamba, jamaa akatoka na michubuko ya hapa na pale lakini akiwa salama. Jamaa huku akiyumba kwa ulevi wa dumu la gongo,akamuuliza kaunta
JAMAA: Haya nishamshughulikia mamba wenu, sasa mleteni yule demu wenu mlisema anaumwa jino nimng'oe sasa hivi.

VIONGOZI MBALIMBALI WAKICHEKA IKISEMEKANA BAADA YA KUSOMA CHEKANAKITIME BLOG


 Yule kocha wa ile timu
 Inasemekana huyu ni Mbunge wa India

Putin wa Urusi
 Haka kamagamba ni kakiongozi ka kata fulani

 "tih tih tih huyu Kitime bwana sijui nimpe uraia wa huku tih tih tih"
Hahahahahaha uwiiii My God funny

NDIO HIVYO TENA YAMENIKUTA NALAZIMIKA KUVAA HELENI

Mbabe mmoja aliwasili kazini kwake katoboa masikio na kavaa hereni.
RAFIKI: Hee ebwanee vipi tena hata wewe umevaa hereni?
MBABE: Yamenikuta makubwa ndugu yangu, wife alisafiri sinikafanya ujinga nikamkaribisha binti mmoja home, mdada alipoondoka kumbe kasahau hereni zake sebuleni kwangu, wife akazikuta kwenye kochi. Aliponiuliza zinafanya nini, nikalazimika kujitetea kuwa nimeamua kutoga masikio, ndo hivo tena, nilikuwa nalinda ndoa, sina ujanja

9 October 2013

HAIKUBALIKI, WANAUME TUNANYANYASWA KWENYE NCHI YETU TULIYOZALIWA, SIO FEA

Nimejaribu kupeleleza na nikaona kuna unyanyasaji mkubwa wa kijinsia hapa nchini, wanaume tunanyanyasika na serikali imekaa kimya, hivi ni haki kweli? Ni wakati mwafaka wanaume na sisi tugome bwana, sio fea hata kidogo. Hebu fikiria umewahi kusikia yafuatayo
 1. Daktari Bingwa wa magonjwa ya wanaume?
2. Hospitali maalumu kwa magonjwa ya wanaume?
3. Wodi ya magonjwa ya wanaume?
Kwanini hakuna vitu hivyo?. WANAUMEEE TUSILALE LALE LALE WANAUME TUSILALE

********TAFAKARI CHUKUA HATUA**********************

USIPANIKI MUME WANGU MLEVI WA KUTUPWA

WIFE alikuwa kaingiza mwanaume kwenye chumba chake cha ndoa. Wakiwa wamelala mume akapiga hodi, jamaa akapanik; WIFE: Tulia huyu ni mlevi kiasi akiingia humu hataweza kukuona... mume akaingia akiwa njwii, akavua nguo zake na kuingia kitandani bila kulalamika, ghafla akshtuka alipoangalia miguuni MUME: We mbona kuna miguu sita? Kuna nini kinaendelea? WIFE: Ulevi wako huo sasa umezidi, mi naona miguu minne hebu amka toka kwenye kitanda uhesabu vizuri.....MUME akaamka na akaanza kuhesabu; MUME: Moja , mbili , tatu, nne aaah kweli, sori mke wangu hizi pombe zinanipeleka pabaya

MUME WANGU NAFA

Mume alikuwa baa anakunywa, akamtext mkewe,' Vipi wife habari za saa hizi?'. Mke akajibu 'Mume wangu nafa'. Mume akashuka kwenye kiti cha bar na kuanza kucheza kiduku kwa furaha, akaagiza mzinga mzima wa konyagi, na kutoa ofa kwa jamaa hata hawajui. Dakika mbili baadae ikaingia text, 'Samahani mume wangu nimetuma txt nusu, nilikuwa nasema NAFAnya usafi huku chumbani kwetu'

TUANGALIE VICHWA VYA HABARI

 Dah wapi hapo tunaomba wasomaji wafafanuliwe.

Mi nafikiri inawezekana betri daun au pengine injini zimenoki, ila madereva wangewaita mafundi makanika wasaidiane na matandiboi, hizi gari zingewaka, au wananchi wangesukuma na zingeshtuliwa zingewaka tu, Nashangaa sana mabasi yagemo wakati madereva wapo why?

8 October 2013

HANI WE NDO MPENZI WANGU WA KWANZA SIJAWAHIGI KUWA NA MWINGINE

MKAKA: Sweety mi ndie mpenzi wako wa kwanza? MDADA: Yaani hani sijawahigi kuwa na  mwingine tena, you are so sweet. Lakini nyie wanaume sijui mkoje, wote mnaulizaga swali hilohilo

MHARIRI WA BLOGU HII ALMANUSRA AFUKUZWE KAZI ALAZIMISHWA KUCHAMBUA VICHWA VYA HABARI USIKU

 Ni kweli hakuna kitu kibaya kama UGADI lazima wanaswe na umeme.

 Tunataka tozo ngumu, Tozo laini hatuzitaki banaaa

Mpanda vespa agongwa gari veye kwani hujui kiswahili hicho ki fasaha veyeeee

KARIBU KATIKA KUNDI LA FREEMASON NDUGU YETU MPENDWA

Jamaa kakosea namba si akatuma 220,000/-kwa MPESA  kwenda namba tofauti na aliyotaka, hapo hapo akili ya haraka ikamjia akatuma text ifuatayo.MPENDWA TUNATEGEMEA UMEPATA FEDHA ZETU. WEWE NI MMOJA ULIYEBAHATIKA KUUNGANISHWA KATIKA KUNDI LETU TUKUFU LA FREEMASON. ILI KUKAMILISHA MAKUBALIANO NDUGU YAKO WA KARIBU ATAFARIKI KATIKA MUDA WA MASAA MATATU BAADA YA KUPOKEA FEDHA HIZO. MARA HILO LITAKAPOTOKEA FIKA UPESI KWENYE NJIA PANDA YOYOTE ILIYOKARIBU NAWE, NA MTUMISHI WETU ATAKUFUATA NA GARI JEUSI NAWE UTAKUJA KUNYWA DAMU YA KIAPO ILI UWE MWANACHAMA KAMILI. KARIBU KWA FURAHA KUU.........Dakika moja na nusu baadaye mesej ikaja umepokea 220,000/ kutoka kwa...........

WARAKA MUHIMU KWA WALEVI WAPYA...

Ndugu zangu wanywaji wapya wa pombe, kutokana na uzoefu wa muda mrefu wa  kulewa nimeona niwape ushauri ambao unaweza kuwapa majibu mtakapojikuta katika hali mbalimbali baada ya kufakamia pombe, urabu, ngumu kumeza na kadhalika.
Tafadhali ieleweke kuwa kuwa matatizo haya hutokea kwa pombe zote zilizohalali na zisizo halali;
1.   Unaamka ghafla unakuta kimya kikuu na giza zito- mara nyingi ni dalili za wazi kuwa umelala baa na wamekufungia, ni busara kutokupanik na kuendelea kulala mpaka watakapofungua kesho yake, kama umeoa au umeolewa ndoa yako iko pabaya.
2.   Unakuta kila mtu anakuangalia ana cheka – Je uko juu ya meza unacheza? Umejikojolea? Au miguu imekataa kufanya kazi. Au umevua nguo zote unajiita John Cenna? Ni bora uwataarifu wote wanaokuangalia kuwa wewe una pesa ndio maana umelewa mno, japo hilo litaalika vibaka wakuandame wakuvuruge.
3.   Unajikuta ghafla unatoka damu mdomoni na puani- ni dalili kuwa umepigwa, kikubwa ni nyamaza usianze kujitetea au kuonyesha kuwa umeonewa, utapigwa zaidi, we omba msamaha tu yaishe.
4.   Uko kwenye bar hukumbuki uliingia  saa ngapi na pia hakuna mtu unaemtambua, wala hata mtaa ulipo huelewi- Hii ni mbaya mtu wa Masaki unaweza ukawa uko Manzese, au unadhani uko kwa mji ulikozaliwa au pengine uko  Kinondoni kumbe uko Dar Live Mbagala, kuolewa ni rahisi sana katika mazingira haya, na hii haijalishi kama ni mwanaume au mwanamke kuna watu hawajali hilo wanaoa tu
5.   Unajikuta unalilia penzi la mhudumu- Hizi ni dalili mbaya ambazo zinaweza kukusababisha uje kupigwa tena, maana mara nyingi unajiona kuwa hakuna mwanamke mzuri kama huyo na uko tayari kuruka kung fu kwa ajili yake.
USHAURI: Mrudie MUNGU akusaidie uache pombe au utapigwa na kuolewa sana  

VAA SURUALI VIZURI WEWE, CHUPI YENYEWE MBAYA


JE MTU UNAJUAJE KUWA UMELEWA?

Mlevi wa ukweli hupitia hatua kadhaa za ulevi, hatua ya kwanza ni BUSARA, katika hatua hii pombe zinakupa BUSARA kuliko mtu yoyote duniani, hapa unakuwa na uwezo wa kuongelea chochote na majibu unakuwa nayo, iwe ni matibabu ya ukimwi au ni namna rahisi ya kuleta maendeleo hapa Tanzania kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, yote hayo unaweza kuyaelezea, yakiwa na takwimu na mifano kutka nchi kama Kenya , Uholanzi na hata Iceland. Ukiendelea kulewa kidogo unaanza kuwa MTANASHATI, kwa kweli hapa unakuwa ni mtu mwenye sura ya mvuto, kama ni mwanaume, wadada wote wakikuona tu wanakutaka wao, na ukiwa mdada katika hatua hii hakuna mwanaume duniani anaeweza kukukataa, katika hatua hii, wanaume kwa wanawake huanza kurembua macho, ikiwa ni kama ishara ya uhandsome au ubeauty (wanaume nao hurembua macho sana tu). Hatua inayofuata ya ulevi ni kuwa PEDESHE, katika hatua hii unakuwa na uwezo wa kuagizia mtu yoyote kinywaji hasa wale ambao hawajatambua kuwa unavutia, pesa zinakuwa hazina kazi mfukoni zaidi ya kununulia watu kinywaji, soda hununui wewe ni pombe tu, tena ikiwa na bei kubwa zaidi kwako ni bora zaidi. Ukiongeza ulevi unaingia hatua ya kuwa BAUNSA na kuwa na nguvu kuliko mtu yoyote duniani, katika hatua hii unajikuta unaweza kuruka Kungfu kwa ufanisi zaidi kuliko Jackie Chan, ni hatari sana kwa mtu yoyote kupinga kuwa wewe si MZURI au wewe si PEDESHE wa kutisha au kupinga BUSARA zako ukifikia hatua hii. Mara nyingi ukiendelea na ulevi baada ya hapa unaingia katika hatua ya kuwa na uwezo wa UCHAWI wa kuweza kutokuoneka. Hapa unaweza kuwa na uwezo wa kukojoa chini ya meza katikati ya baa na hakuna mtu anakuona, yaani hapa unaweza kuanza kuvua nguo moja moja na watu hawakuoni kabisa. Nawasilisha hoja.

'MUME WANGU NIKIFA UTAOA?'

Mke: Mume wangu hivi nikifa utaoa tena?
Mume: Hapana
Mke: Kwanini? Hutaki ndoa?
Mume: Basi tu
Mke: Kwa hiyo hata sasa hutaki ndoa?
Mume: Nataka
Mke: Kwa hiyo kwanini usioe?
Mume: Haya labda ukipita muda ntaoa
Mke: Mtaishi nyumba hii hii?
Mume: Ndio sidhani kama ntahama nyumba tuliyojenga
Mke: Mtatumia sahani na vikombe vyangu
Mume: Ehh nadhani
Mke: Atavaa nguo zangu?
Mume: Ndio
Mke: Atavaa viatu vyangu?
Mume: Hapana, vyako vidogo ye anavaa namba 6
HAPO NDIPO NGUMI ZILIPOANZA

7 October 2013

MAFALA SANA, UKUBWA WOTE HUO MNAAMINI STORI ZA MAZIMWI

Supasta alipopata mkwanja akaamua kuhamia mitaa ya watu wenye pesa akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae alipokuwa anacheza na manati akavunja kioo cha nyumba ya jirani. Supastar na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafukua mbaba mmoja;
MBABA: karibuni
SUPASTA: Samahani sie tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza
MBABA: Karibuni kwenye kiti niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi. Mimi ni ZIMWI nilikuwa nimefungiwa kwa zaidi ya miaka 200 kwenye kichupa kilikuwa kwenye kile chumba ambacho dirisha limevunjwa, chupa nayo imevunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa
SUPASTAA:Mi naomba niwe bilionea mpaka nife
MBABA: Hilo jambo dogo sana kwangu, umepata na kesho utaamka tajiri
MKE WA SUPASTA: Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na HongKong
MBABA:Umepata kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina ombi dogo.
SUPASTAA: Sema tu
MBABA: Mi naomba nilale na mkeo leo tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu. Asubuhi ikifika hamtaniona tena, itakuwa siri yetu
Supasta na mkewe wakajadili, wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana hilo jambo ni dogo wakakubali sharti. Mke akalala kwa Mbaba mpaka asubuhi. Wakati mke akijitayarisha kurudi kwake Mbaba akakohoa kidogo;
MBABA: We una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi??
MKE: Mume wangu 32 na mimi 30
MBABA: Sasa nyinyi mafala mpaka leo mnaamini stori za MAZIMWI?

WALI UMEKWISHA MZEE

Kaiza: Weita leta menu
Weita: Mzee hatuna menu, we agiza chochote kile sisi tunacho. Kaiza akaona amtanie weita.
Kaiza: Poa basi niletee wali kwa filigisi ya twiga
Weita: Hakuna tabu mzee subiri....Baada ya muda Weita akarudi
Weita:Samahani mzee oda yako hatuna, agiza kingine Kaiza: We si umesema una kila kitu.
Weita
: Ndio mzee, lakini bahati mbaya saa hizi wali umekwisha.

BABY PLEASE NISAIDIE HELA NINUNUE SCRIPT ZA BLUU LOVE YOU MWAHHHH

BABY NAMALIZIA KUTENGENEZA MUVI YANGU, SASA TUMETENGENEZA KILA KITU ILA SASA TUNATAKIWA TUNUNUE SCRIPT TATU MBILI ZA BLUU NA MOJA NYEKUNDU BABY, HIZI ZINATAKIWA SANA MAANA SIKU HIZI MUVI LAZIMA ZIWE DIJITO. BABY DA WEMA ANAENDA CHINA WIKI IJAYO NILIKUWA NATAKA AKANINUNULIE ILI KUSEV GHARAMA. BABY PLEASE NAOMBA MILIONI KUMI TU ZA KUNUNULIA HIZO SCRIPT TATU NA MBILI ZA ZAIDA KWA AJILI YA MUVI IJAYO. BABY PLEASE'

JE UNATAKA MAISHA YA RAHA? FUATA HAYA UKIKAMATWA MI SIMO

Ukitaka kupata raha katika maisha yako,
1. Tafuta mwenza ambaye ni msaada mkubwa nyumbani
2. Tafuta mwenza ambaye unaweza kutoka nae 'out' bila kuaibika
3. Tafuta mwenza ambae mnaweza kuzungumza malengo na matarajio yanayofanana
4. Tafuta mwenza ambae mnafurahiana katika faragha........Kazi ngumu hapa ni kuhakikisha hawa watu wanne hawajikujuana wala kugongana

TANGAZO LA BURE KWA SHULE YA WAVULANA ILIYOKO KENYA.............

JE UNA KIJAMA WAKO MVULANA ANAHITAJI ELIMU ? HEBU CHEKI WEBSITE HII http://usengehigh.shuleweb.net/
BLOG YA JAMII KWA AJILI YA JAMII

JAMAA WALIKUWA WANAOSHA MAITI...........................

Jamaa walikuwa wanaosha maiti kuitayarisha kwa mazishi, ghafla maiti ikaanza kucheka;
MAITI: Kwi kwi kwi kwi Mnanitekenya mwanzenu jamani ahh...............Mlango ulikuwa mdogo

BLOG YAPATA MPIGA PICHA MPYA

TUNGEPENDA KUWATANGAZIA KUWA KWA SASA BLOG YENU YENYE CHOO NDANI, INAPOKEA MAOMBI YA WATU WANAOTAKA KUPICHA PIGWA KWENYE SHUGHULI ZAO ZINAZOHITAJI KUMBUKUMBU. TUNAPOKEA MAOMBI YA KUPIGA PICHA SIKU ZA KUACHANA, SIKU UNAPOSHINDWA UCHAGUZI, SIKU YA KUFUKUZWA KAZI, SIKU UNAPOFUMANIWA, SIKU UNAPOCHUNWA, SIKU UNAPOTANDIKWA VIBAO NA MKEO NA KADHALIKA. BEI ZETU NI NAFUU, NA MPIGA PICHA WETU NI MHAMIAJI HARAMU, HII NI KUTOKANA NA UHABA WA WAPIGA PICHA HAPA NCHINI AKSANTE KWA KUCHAGUA HUDUMA ZETU.

HAPPY BIRTHDAY MR PREZDENT

Good morning Sir,
As meneging director of the blog,
 we wish you a very Happy Birthday of siku ya kuzaliwa.

6 October 2013

HUYU NAMUACHA

 Leo kanipigia simu mapema asubuhi, eti ananiuliza,
'Good morning Baby, eti  namba yako ya simu ngapi? Nikumbushe mie nimeisahau nataka kuchat na wewe'

MAMA WA KIVITZ VERSUS MAMA MWENYE VOGUE

Wamama wawili walijikuta magari yao yamegongana. Wakashuka kwenye gari wakaanza kutoleana kashfa, hasa yule aliyekuwa na vogue akamtukana sana mwenye Kivitz, japokuwa ndie aliyekuwa na makosa. Mwenye Kivitz akampigia mumewe simu.
MAMAKIVITZ: Mume wangu ninatatizo
MUME: Jamani niko bizy mkutanoni hebu lisov mwenyewe
MWENYE VOGUE akasema anampigia boy friend wake ndiye atakae ongea.
MWENYE VOGUE: Darling kuna mjinga mmoja kagonga gari uliloninunulia, please njoo.
Muda si mrefu jamaa akaja, kumbe alikuwa ndiye mume wa MAMAKIVTZ......kila mtu amalizie sinema hii

5 October 2013

NAUZA WHATSAPP


YAANI HONGO YAKO IMESAIDIA SANA

Jamaa alikuwa na kesi nzito ya mauaji, ikafikia wakati wa kutoa hukumu akahisi wazee wa baraza watamuona ana hatiana anaweza akanyongwa, basi akampata mzee mmoja wa baraza akamhonga ili ashawishi wenzie wasimpate na kosa la mauaji ya kukusudia maana atanyongwa, ila japo liwe kosa la mauaji bila kukusudia ili afungwe tu. Kweli baada ya siku tatu wazee wa baraza wakakubaliana kuwa jamaa aliua bila kukusudia, Jaji akampa adhabu ya kifungo cha  miaka saba, akashukuru. Alipopata nafasi ya kuongea na mzee aliyemhonga;
MFUNGWA: Mzee nashukuru sana nategemea sikukupa kazi nzito
MZEE: Loh ilikuwa kazi nzito sana, wenzangu wote walikuwa wameona huna hatia hivyo kuwabembeleza wakubali kuwa umeua bila kukusudia ilikuwa ngumu sana.

WE NITIBU ACHA MASWALI DOKTA

Jamaa kaenda hospitali kutibiwa, kavimba  jicho;
DOKTA: Vipi ulifanya nini hapa?
JAMAA:Ahh bwana mambo yetu yale, nilimkumbatia hauzgelo,
DOKTA: Hapo sijaelewa kumkumbatia hausgelo inaletaje kuvimba jicho
JAMAA: Si waif akaingia ghafla, we nitibu bwana acha maswali.

NAUZA DUNIA

MLEVI 1: Mi naweza kukununulia dunia
MLEVI 2: Huwezi
MLEVI 1: Nasema NAWEZA
MLEVI 2: Huwezi kwa sababu siuziiii

MASUPASTAA HAMNAGA AIBU, BOSI HAWEZI KURUHUSU

Mdada msupastaa alikuwa anapita madukani akiangalia vitu, akaiona suruali nzuri kwenye dirisha la duka moja akaingia;
MSUPASTAA: mambo dada?
MUUZADUKA
: Heee jamani, leo na bahati nimekuona laiv, karibu dada nikusaidie nini?
MSUPASTAA: Samahani naweza kujaribu ile suruali pale dirishani
MUUZADUKA: Dah najua nyie masupastaa  hamuonagi aibu, lakini bosi hawezi kuruhusu ujaribie pale dirishani, italazimika ukajaribie kwenye kichumba huko ndani kama watu wengine.

NDOA BASI IMENISHINDA

Mdada baada ya kuolewa kwa siku chache kampigia simu mama yake;
MDADA: Mama mi ndoa imenishinda huyu mwanaume ananipigia kelele hata vitu vidogo,mama huyu ana gubu sana
MAMA: kwani vipi tena?
MDADA: Jana nimemtengenezea soseji 2 badala ya kushukuru kaanza kulalamika eti natumia hela hovyo
MAMA: He mbona shida, bei ya soseji mbili tu kelele
MDADA: Sio bei ya soseji ni microwave
MAMA: Sasa sielewi
MDADA: Nilitaka kumpashia moto zile soseji kwenye mfuko wameandika tumia microwave, ndio nikakodi taxi nikaenda supamaketi nikanunua microwave mpya , mume wangu apate soseji za moto ananipigia kelele, mi naona nimechoka kelele.