PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SIO BREKING NYUUUUUUUUUUUZ...MABLOGA KWENDA KWA WATAALAMU BAGAMOYO

Habari zilizolifikia blog hili lenye choo ndani ni kuwa kundi la Blogaz leo wanaelekea Bagamoyo. Haijajulikana wanaenda kufanya nini, ila wachunguzi wa mambo wanadhani ni kwa kuwa Bagamoyo ni sehemu moja ambayo watu huenda kwa wazee wa busara kusafisha nyota, inawezekana hawa jamaa
wanataka kuunganisha nguvu za kiasili na nguvu za dijitali ili kuongeza watembeleaji wa blog zao. Bosi wa blog hii alionekana jana Vingunguti akitafuta mbuzi mweupe mwenye doa kwenye paja la kushoto, haikuweza kujulikana kama hilo ni sharti moja wapo la wataalamu wa huko Bagamoyo. Tutawaletea habari zaidi kadri maspai wetu watakavyozipata.

Comments