PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NIPE MIMI HIYO TENDA MKUU

Jamaa watatu walienda kuomba tenda ya kujenga uzio wa nyumba ya serikali,
MJENZI 1: Mimi naweza kujenga uzio kwa shilingi milioni 12, vifaa milioni sita, wajenzi ntawalipa milioni mbili na mimi nitapata faida milioni nne.
MJENZI 2: Mimi nanaweza kujenga uzio huo kwa shilingi milioni kumi na tatu, vifaa milioni sita, wajenzi milioni mbili na mimi mwenyewe ntapata faida ya milioni tano. 
Mjenzi wa tatu akamwita pembeni mtoa tenda,
MJENZI 3: Sikiliza mkuu mi nataka milioni 42, milioni kumi zako, milioni 20  zangu halafu tunamkodisha yule fala wa kwanza ajenge uzio, imekaaje hiyo?  Akapata tenda mara moja.

Comments

Anonymous said…
OZO ni kijana mwenye sifa ya uvumilivu, upole, na kujiamin kulingana na malez na mafunzo aliyo zingatia katika ukuaj wake, imemfanya kupendwa na watu wengi hasa wazee.. mara baada ya kuhitimu kidato cha nne OZO hakubahatika kuendelea na kidato cha tano baada ya matokeo kuwa mabaya, ndipo alipo amua kujiunga na chuo.. Huko aliendelea kuwa na tabia yake ileile nzur ..ilipita miez miwil akiwa chuoni. siku moja aliingia darasan kujisomea majira ya saa 2 ucku.. alishangaa kuona mtu alikuwa mrefu sana ukilinga nisha na nguzo ya umeme. nguvu zilimuisha OZO na kujkuta ana anguka chin.. Itaendelea akipata fahaham.