PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAJILAUMU KUNUNUA SIMU FEKI DAH


Kweli hawa jamaa simu zao feki. Simu yangu imeanguka, Phonebook imechanika karatasi zote zimepeperuka, na sina sasa hata kumbukumbu moja. Hela zote kwenye Tigo Pesa  zimedondoka watu wameokota yaani nimekula hasara sana, haya huku kwenye Bluetooth meno yote yameng’oka fizi zinatoka damu sana, message zangu nazo zimetapakaa chini watu wanazisoma, najisikia aibu maana message nyingi zilikuwa za siri sana. Rafiki zangu wengi wa kwenye facebook na whatsapp wameumia, kuna mdada mmoja alikuwa mgeni kabisa kakamatwa eti mhamiaji haramu, password  zangu zote zimeharibika kabisa sina raha najilaumu kwanini nilinunua simu feki.

Comments