PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HURUMA TU MTOTO SI RIZKI LAKINI SI MBAYA SANA


BAADA YA KUKUTANA kwa mara ya kwanza toka walipoachana sekondari miaka 30 iliyopita marafiki watatu walikaa kwenye kwenye club moja na kuanza kuhadithiana juu ya maisha yao. Wakati mmoja wao kaenda chooni yakaanza mazungumzo kuhusu mafanikio ya watoto wao wa kiume.
 Wa kwanza akasema "Mwanangu kasomea mambo ya uchumi akafanya kazi benki kadhaa na hatimae amekuwa tajiri kiasi cha kuweza kumzawadia rafiki yake Vogue jipya siku ya birthday yake”.
 Wa pili akasema  "Hayo madogo mwanangu amekuwa tajiri kiasi cha kuweza kumnunulia rafiki yake mpenzi ndege ndogo siku ya birthday yake”. 
Watatu akasema, “Mwanangu amekuwa injinia mwenye mafanikio makubwa kiasi cha kuweza kumjengea rafiki yake bonge ya jumba la kifahari na kumkabidhi siku ya birthday yake?. 
Yule wanne ndio akarudi toka chooni, akauliza “ Mnazungumzia nini?” Wakamwambia wanazungumzia mafanikio ya watoto wao. Jamaa akajibu,” Ahh hilo jambo acheni tu , mi mwenzenu mtoto wangu mwenyewe mmoja tu na si amekuwa shoga mkubwa”. Wenzie wakamwambia , “Pole lazima inauma yaani umezaa mtoto hana mafanikio”. Jamaa akajibu,” Hapana si mbaya kihivyo, siku ya birthday yake mabwana zake wamempa zawadi kubwa sana, mmoja kampa Vogue jipya, mwingine kampa ndege ndogo, mwingine kamjengea bonge la jumba. Nabaki kushukuru Mungu tu”.

Comments