HATUPIMI BANDO

30 September 2013

BLOGA MAARUFU APANIA KUWA MPIGA SOLO WA MSONDO AANZA MAZOEZI MAKALI CHINI YA MKUFUNZI ZEE LA NYETI

Baada ya mwanamuziki mmoja kujifanya bloga, na kupita huku na kule kujitangaza kuwa nae eti ni bloga mwenye blog ya kwanza kuwa na choo ndani duniani, mmoja wa vigogo wa maBloga Tanzania, nae eti ameanza kujifua ili awe mwanamuziki wa Kimataifa. Bloga huyu mrefu kidogo , mwembamba kidogo, mwenye tabasamu la wastani, na kicheko cha hapa na pale alikutwa akiwa kaweka kambi katika mji wenye chuo maarufu cha sanaa na ambao pia hufahamika kwa kutoa njia za mkato kwa matatizo kama, kutajirika haraka, kumrudisha mpenzi aliyekuacha, kushinda Ubunge, kupandishwa vyeo, kushusha mishipa wanoko, na hata wanamuziki kukimbilia huko ili kuweza kujaza wapenzi kwenye show ambazo wanazifanya bila kuwa na nyimbo nzuri, na pia hata wacheza mpira kwenda kuomba kuzifunga timu pinzani ambazo nazo huwa hukohuko zikitegemea huduma hiyohiyo kwa kifupi jiji lenye huduma mbadala wenye mtizamo wa BIG RESULTS NOW. Bloga huyu anajifua kulipiza kisasi kwanini mwanamuziki ameingia kwenye anga zake. Blog hii tata isiyo na matangazo inamtakia kila la heri katika taaluma yake mpya ya kusaka usupastaa. 

No comments: