PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

ACHENI KUNITESEA MWANANGU

Mama mmoja alienda kumtembelea mwanae shuleni, akakuta darasa la mwanae wako nje kwenye kipindi cha michezo. Akamtafuta mwanae akamuona kasimama peke yake wakati wenzie wanacheza kwa furaha. Akakaa kama dakika tano akasikitika sana kuona mwanae kasimama mahala pamoja hatoki wala haendi kujiunga na wenzie waliokuwa wakicheza kwa furaha;
MMAMA: Mwalimu kwanini mtoto wangu unambagua?
MWALIMU: Kwani vipi mama?
MMAMA: Usijifanye hujui, nimekaa hapa kitambo, namwona mwanangu mmemtenga wakati wenzie wanacheza wanafurahi, yeye mmemzui mahala pamoja.
MWALIMU: Mbona sikuelewi mama?
MMAMA: Hunielewi nini? Mnajidai mara mnagoma mara nini kumbe kazi kutesa watoto wa wenzenu, hebu muangalie mtoto wenzie wanacheza na mpira yeye mmemsimamisha tu pale kaganda
MWALIMU: Mama hapa wanacheza soka na mwanao golikipa, ndio maana kasimama peke yake anazuia adui wasifunge magoli.

Comments