HATUPIMI BANDO

30 September 2013

BLOGA MAARUFU APANIA KUWA MPIGA SOLO WA MSONDO AANZA MAZOEZI MAKALI CHINI YA MKUFUNZI ZEE LA NYETI

Baada ya mwanamuziki mmoja kujifanya bloga, na kupita huku na kule kujitangaza kuwa nae eti ni bloga mwenye blog ya kwanza kuwa na choo ndani duniani, mmoja wa vigogo wa maBloga Tanzania, nae eti ameanza kujifua ili awe mwanamuziki wa Kimataifa. Bloga huyu mrefu kidogo , mwembamba kidogo, mwenye tabasamu la wastani, na kicheko cha hapa na pale alikutwa akiwa kaweka kambi katika mji wenye chuo maarufu cha sanaa na ambao pia hufahamika kwa kutoa njia za mkato kwa matatizo kama, kutajirika haraka, kumrudisha mpenzi aliyekuacha, kushinda Ubunge, kupandishwa vyeo, kushusha mishipa wanoko, na hata wanamuziki kukimbilia huko ili kuweza kujaza wapenzi kwenye show ambazo wanazifanya bila kuwa na nyimbo nzuri, na pia hata wacheza mpira kwenda kuomba kuzifunga timu pinzani ambazo nazo huwa hukohuko zikitegemea huduma hiyohiyo kwa kifupi jiji lenye huduma mbadala wenye mtizamo wa BIG RESULTS NOW. Bloga huyu anajifua kulipiza kisasi kwanini mwanamuziki ameingia kwenye anga zake. Blog hii tata isiyo na matangazo inamtakia kila la heri katika taaluma yake mpya ya kusaka usupastaa. 

KICHWA CHA HABARI CHAMKUMBUSHA MHARIRI SOMO LA KEMIA FOM WAN

Acid is from the Latin language  acidus/acēre meaning sour. Acid is a chemical substance whose aqueous solutions are characterized by a sour taste, the ability to turn blue litmus red, and the ability to react with bases  and certain metals (like calcium) to form salts....CHEZEA MHARIRI WEWE

29 September 2013

JE, HII INGEWEZA TOKEA KWENYE GAZETI LA KISWAHILI? AU LINGEFUNGIWA

AU KWA KIZUNGU IKO POA LAKINI TAFSIRI YA KISWAHILI NDO VIBAYA?

NILIKUWA NAKOJOA KISIRISIRI

Mlevi alikuwa anakojoa kando ya barabara, mgambo akamzukia;
MGAMBO: We acha kukojoa funga zipu haraka. Mlevi akafunga zipu haraka, mgambo akaondoka. Mlevi akaanza kucheka
JIRANI: Sasa unacheka nini?
MLEVI: Mi mtoto wa mjini bwana, yaani nimemdanganya mgambo hivihivi?
JIRANI: Umefanya nini?
MLEVI: Nimefunga zipu lakini nikaendelea kukojoa kisiri kwenye suruali mpaka nimemaliza, na yule fala wala hakutambua.

BAA HII WASHENZI WOTE SIRUDI TENA

Baunsa mmoja aliyekuwa kakaa kaunta ya baa fulani akinyanyasa watu na misuli yake, aliondoka kwa furaha kwenda chooni, lakini akarudi amekasirika jasho linamtoka; BAUNSA: Baa hii washenzi wote KAUNTA: Kwani vipi mzee? Tumekukosea nini mbona unatuonea? BAUNSA: Nimeenda chooni mwenzenu mmoja kaja na kuniwekea pisto kichwani akadai nikikataa asinibake ananilipua na risasi ya kichwa KAUNTA: He pole wahuni hao, sasa imekuwaje? BAUNSA: Imekuwaje nini? Maswali gani hayo? Kwani umesikia mlio wa bunduki. Washenzi wote baa hii na sirudi tena kunywa humu.

28 September 2013

NI KWELI YULE NI MAMA YAKE, TENA MAMA YAKE MZAZI

Shugamami na Kiserengeti boi chake walifika guest moja kuomba chumba;
SHUGAMAMA: Naomba chumba, nipe dabo
MWENYEGESTI(Mlokole): Hapa hatuwapi chumba labda mngekuwa mke na mume katika ndoa halali
SHUGAMAMA:We baba we mbona una matusi? Huyu ni mwanangu
MWENYEGESTI: Samahani mama chumba kipo karibu samahani............Baada ya kupewa chumba mwenye gesti akamwita muhudumu,
MWENYEGESTI: Hebu kawachugulie wale maana yule mama amesema eti yule kijana ni mwanae ila mimi siamini sana............muhudumu akaenda kuchungulia kisha akarudi
MHUDUMU: Kweli ni mama yake, tena ana huruma sana, nimechungulia nimeona anamnyonyesha mtoto wake

MCHUNGAJI KASEMA LEO HAKUNA IBADA

Jamaa alikuwa njiani anaenda kanisani, si akashtuka kukumbuka kuwa ameacha simu yake nyumbani. Haraka akageuza njia na kuanza kurudi  nyumbani, alipofika home presha ikiwa juu bahati nzuri akauta mkewe hajaamka akaichukua simu yake na kuvunja safari ya kwenda kanisani akaanza kuangalia TV, mkewe alipoamka akamkuta jamaa kajaa tele sebuleni,
MKE: Jamani si nilidhani umeenda kanisani?
JAMAA: Mchungaji kanitext kasema leo hakuna ibada.

27 September 2013

KAMA UNANIPENDA TURUDIE LA PILI

DOGO: Baba lini mnaanza shule?
BABA: Shule? Kwanini nianze shule mi nimemaliza zamani mwanangu
DOGO: Mbona jana usiku nilikusikia unamwambia mama "Kama unanipenda turudie la pili"

KIMBUNGA BANA MATUMIZI PART 1

KUTOKANA NAMATATIZO YA KIUCHUMI YALIYOKO TAFADHALI WAFANYAKAZI WOTE WA SERIKALI YANGU YA BLOGU HII, WATALAZIMIKA KUFUATA TARATIBU HIZI ILI KUPUNGUZA MATUMIZI
Malazi:
Watumishi wa ngazi za Uwaziri mnashauriwa kulala kwa ndugu zenu na marafiki wakati mkiwa katika ziara za kikazi. Wafanya kazi wa ngazi za chini ya hapo tumieni madarasa, vituo vya basi au hata vibaraza vya ofisi za serikali za mitaa mtakazozitembelea kwa ajili ya kujihifadhi wakati wa usiku.
Usafiri:
Ni busara kubwa kuomba lifti kila uwapo katika shughuli za kazi. Waheshimiwa Mawaziri na hata wabunge watumie mabasi na hatimae treni pale zilipo. Usafiri wa ndege utatolewa pale ambapo ni lazima kwa mfano ikiwa umefariki ghafla mbali na kwenu, au unaenda India kwa matibabu au wewe ni mimi bosi.
Chakula:
Ulafi ni hasara, hindi la kuchoma na maji vinaweza kabisa vikakufikisha siku ya pili kama uko mbali nakwenu. Kwa viongozi ndizi sukari mbili tatu za ziada zinashauriwa.
ALLOWANCE:
Hiki ni kimoja cha vitu vilivyopunguza uzalendo katika nchi hii. Blog yangu inakataza wafanya kazi wake kulipwa hii kitu ya ajabu. Nashauri na serikali yetu tukufu iwe sikivu ifuate utaratibu huu wa blog hii ili kuleta displin ya kazi na fedha husika kutumika katika kununua vitanda hospitalini 
IT CAN BE DONE PLAY YOUR PART

MHARIRI WA BLOGU AWEWESEKA AACHA KUCHAMBUA VICHWA ACHARUKA


SOPHIA SIMBA!!!!!!!!!!!!!!!???????? Ni wazi  wahariri wameamua kuchukua akili zetu na kuamua zielekee wapi.... sasa KACHARUKA au AWEWESEKA?

26 September 2013

KWA HUDUMA TAFADHALI PIGA 88888888888888888


KWA HISANI YA GAZETI LA VISA...HAHAHAHAHAHAHA DAH WATU WANAJUA UTANI


JAMANI NYOA NDEVU

NYUMBA NDOGO: Jamani nyoa hizi ndevu zako mi sizipendii
BUZI: Hapana bwana unataka ninyoe za nini?
NYUMBA NDOGO: Nataka niione hiyo sura handsome, please nyoa bebii
BUZI : Hapana ntakorofishana na mke wangu anapenda niwe hivi
NYUMBA NDOGO: Jamani Eddy nyoa bwana......jamaa akakubali akanyoa. Saa nane za usiku Eddy akarudi kwake akinyata na taratibu akaingia kwake alipojifunika shuka, mkewe akageuka akiwa nusu usingizini si akamgusa jamaa kidevu
WIFE: Haaa jamani Devi unatafuta nini saa hizi? Unataka tuuwawe? Ondoka haraka mume wangu atarudi wakati wowote

SINA LAKINI NINA...........

MKAKA: Nakupenda naomba nikuoe
MDADA: Unanyumba
MKAKA: Sina lakini...
MDADA:Una Verosa?
MKAKA:Sina lakini...
MDADA:Lakini nini? Mshahara wako shilingi ngapi?
MKAKA: Sina lakini....
MDADA: Hebu tambaa, kila kitu huna.
MKAKA: Poa naondoka, lakini sina nyumba nina bungalow, sina Verosa nina Range Rover Vogue, sina mshahara nina kampuni kadhaa
MDADA: Ehh

SUMU YA PANYA YA MICE KILLER

Mhariri alikwepa kwenda Bagamoyo akakutwa anasoma kipande hiki cha galizeti. Bado hajajua ikiwa 'watu wawili wamekufa akiwamo aliyetaka kufa??????? Na pia amekunywa sumu ya panya ya mice killer!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!OKAY OKAY OKAY

FRIJI LINAUZWA

Jamaa alinunua friji jipya, akawaza namna ya kuondokana na lile la zamani, basi akaliweka nje ya nyumba yake na kuandika kibao ANAE TAKA KUCHUKUA ACHUKUE BURE, watu wakawa wanapita wanafungua lakini kila mtu akawa anaogopa kuchukua maana hakuna aliyeamini mtu anaweza akagawa friji zima bure. Baada ya kuona wiki imepita halijachukuliwa, akaandika FRIJI INAUZWA LAKI 3, usiku uleule likaibiwa

HAPO ZAMANI ZA KALE KABLA MAGOROFA HAYAJAJENGWA KILA KONA


UTENDAJI KISERIKALI ZAIDI


USISIKITIKE BWANA NTAOA TENA

Jamaa alifiwa na mkewe,baada ya maziko akamwona jamaa mwingine ambae hakuwa anamfahamu analia kwa uchungu sana, na hata kujigaragaza kwenye kaburi la marehemu. Akamuuliza jirani yake Juma ; Mume: Aise Juma huyu ni nani mbona ana uchungu sana? Juma: Swali lako gumu lakini kiukweli huyo ndio alikuwa anakuibia mkeo...... Mume akamuendea yule jamaa Mume: Pole bwana usisikitike sana, ntaoa tena

SIO BREKING NYUUUUUUUUUUUZ...MABLOGA KWENDA KWA WATAALAMU BAGAMOYO

Habari zilizolifikia blog hili lenye choo ndani ni kuwa kundi la Blogaz leo wanaelekea Bagamoyo. Haijajulikana wanaenda kufanya nini, ila wachunguzi wa mambo wanadhani ni kwa kuwa Bagamoyo ni sehemu moja ambayo watu huenda kwa wazee wa busara kusafisha nyota, inawezekana hawa jamaa
wanataka kuunganisha nguvu za kiasili na nguvu za dijitali ili kuongeza watembeleaji wa blog zao. Bosi wa blog hii alionekana jana Vingunguti akitafuta mbuzi mweupe mwenye doa kwenye paja la kushoto, haikuweza kujulikana kama hilo ni sharti moja wapo la wataalamu wa huko Bagamoyo. Tutawaletea habari zaidi kadri maspai wetu watakavyozipata.

25 September 2013

CHAMBUA CHAMBUA YA VICHWA VYA HABARI

 HATA SISI HATUJUI TUSEME NINI

 JAMANI VICHWA VYA HABARI VINGINE KIBOKO

 ALAAAAA KUMBEEEEEE

TAFSIRI KWA KIINGEREZA

UNAJUA SIJAONA BAISKELI SIKU NYINGI SANA

Babu mmoja mwenye heshima kama mhariri mkuu wa blog hii alipita mitaa fulani akakuta vijana wamejipanga barabarani kwa furaha;
BABU: Kuna nini tena hapa vijana?
YANKI: Babu tumeambiwa kuna mwanamke mmoja supastaa atapita mtaa huo anaendesha baiskeli lakini hajavaa hata kipande cha nguo.
BABU: Dah ngoja na mie ningoje unajua sijaona baiskeli siku nyingi sana

23 September 2013

SANAMU KWA HESHIMA YA SHUGHULI MUHIMU


CHAMBUACHAMBUA YA VICHWA VYA HABARI

 Hapo ndipo ninapoona mamlaka husika zinatimiza wajibu wake. Wote tunajua hata mbuyu ulianza kama mchicha, hivyo kuna vigogo vilivyotokana na mchicha. Kwa hiyo hata vigogo vya miti ya bandi vigogo vya mpapai na vigogo vya migomba vilianza taratibu. Najua hapa lazima vigogo vilivyokatwa kutokana na miti ya bangi vitakubwa na Kimbunga si eti ehhh au nimekosea?

 Mmeshawaita haramu watakuwaje halali tena lazima watakataliwa kila mahala.

Najua Mbogo ndio Nyati kwa hiyo ohooo...........dah siendelei

KATIKA KUJALI WATEJA BLOG YENU IMETENGA SEHEMU YA KUJISAIDIA aka MSALANI

Tafadhali angalia hapo juu utaona kiti kinakuelekeza uende wapi. Tafadhali tutumie vyoo kistaarabu....

22 September 2013

ALAMBA ALAMBA AAAM AAAMM AAAMMMHE KUMBE UNA UGONJWA WA ZINAA?

Manesi wengine noma, jamaa alikuwa na appointment na dokta. Akamuendea nesi aliyekuwa akipokea wageni ambao walikuwa wengi wamejazana kwenye mabenchi wanasubiri huduma;
JAMAA: Samahani naomba kumuona dokta anishauri dawa vipimo hivi hapa...akampa nesi karatasi, nesi akasoma kile kikaratasi
NESI: ( Kwa sauti kubwa) He kumbe una ugonjwa wa zinaa, muwe na nyie mnajichunga jamani
JAMAA: (Nae kwa sauti) Sawa nesi, dokta alinambia na wewe ugonjwa huu ulikusumbua kwa muda mrefu sana, vipi dawa hizi zilikusaidia?

KUTOKANA NA BLOG HII KUPIGWA KIPAPAI ISIPATE MATANGAZO, MHARIRI WA BLOG AMEAMUA KUTUMIA MKAKATI WA BIG RESULTS NOW


HURUMA TU MTOTO SI RIZKI LAKINI SI MBAYA SANA


BAADA YA KUKUTANA kwa mara ya kwanza toka walipoachana sekondari miaka 30 iliyopita marafiki watatu walikaa kwenye kwenye club moja na kuanza kuhadithiana juu ya maisha yao. Wakati mmoja wao kaenda chooni yakaanza mazungumzo kuhusu mafanikio ya watoto wao wa kiume.
 Wa kwanza akasema "Mwanangu kasomea mambo ya uchumi akafanya kazi benki kadhaa na hatimae amekuwa tajiri kiasi cha kuweza kumzawadia rafiki yake Vogue jipya siku ya birthday yake”.
 Wa pili akasema  "Hayo madogo mwanangu amekuwa tajiri kiasi cha kuweza kumnunulia rafiki yake mpenzi ndege ndogo siku ya birthday yake”. 
Watatu akasema, “Mwanangu amekuwa injinia mwenye mafanikio makubwa kiasi cha kuweza kumjengea rafiki yake bonge ya jumba la kifahari na kumkabidhi siku ya birthday yake?. 
Yule wanne ndio akarudi toka chooni, akauliza “ Mnazungumzia nini?” Wakamwambia wanazungumzia mafanikio ya watoto wao. Jamaa akajibu,” Ahh hilo jambo acheni tu , mi mwenzenu mtoto wangu mwenyewe mmoja tu na si amekuwa shoga mkubwa”. Wenzie wakamwambia , “Pole lazima inauma yaani umezaa mtoto hana mafanikio”. Jamaa akajibu,” Hapana si mbaya kihivyo, siku ya birthday yake mabwana zake wamempa zawadi kubwa sana, mmoja kampa Vogue jipya, mwingine kampa ndege ndogo, mwingine kamjengea bonge la jumba. Nabaki kushukuru Mungu tu”.

MHARIRI WETU ANAENDA KUSOMA ULAYA HIVYO AMEANZA KUCHAMBUA VICHWA KWA KINGLEZA SAMAHANI KWA USUMBUFU

 THE DOCTOR WHO WAS MAKING A HEAD WHICH WAS TALKING IS SAVED

 LION, MBEYA CITY NOBODY IS CUT HERE

SHE HAS GIVEN BIRTH TO FOUR TWINS

21 September 2013

MADAM YUU AA KIBONGLOSI

" Madam madam soli madam, madam ekskyuz mi yua nanihii is kibongolosi madam jaman mi kizungu sijui"

BIZE KUTAFUTA MKWANJA WA WIKIENDI, WAPI LULU? WAPI WOLPER? WAPI MONA?


TANGAZO TANGAZO TANGAZO----UKIONA NJIGI UTADHANI NJEGE, NA UKIONA NJEGE UTAFIKIRI NJIGI

Hatimae kile kitendawili cha UKIONA NJIGI UTADHANI NJEGE NA UKIONA NJEGE UTAFIKIRI NJIGI kimetenguliwa kisayansi.......
Ndugu wananchi wa himaya ya Chekanakitime. Katika wiki chache zilizopita kuna wadada walipitisha magunia kadhaa ya Njigi pale kwenye geti letu umeona, sasa kwa kuwa walipitisha Njigi na sisi tumesema kamwe hatukubali watu wapitishe Njigi kwenye geti letu tukawatandika viboko wote walioruhusu Njigi zipite. In fekt tukatumia mihela yenu kadhaa kupanda ndege na kulala hoteli za bei mbaya ili kufuatilia Njigi zilikokwenda na ili kujua Je, zile ni Njigi au ? Umeonaee. Utafiti wa kisayansi uliotumia nguvu za mionzi ya jua umegundua kumbe tuliona Njege na sisi tukadhani Njigi. Therefore, kumbe yale yalikuwa magunia ya Njege sio magunia ya Njigi umeonae. So,
kwa hiyo geti letu ni Fresh kabisa halijawahi kupitisha Njigi, kwa wale waliolambwa viboko uchunguzi bado unaendelea kama walifanya kosa ama hawakufanya kosa, maana haya mambo yana taratibu zake huwezi ukarash, unaweza kupata wrong answers for right kweshens. Kwa hiyo kwa tangazo hili tungependa kufahamisha umaa wa chekanakitime kuwa zile kilo 150 zilikuwa ni NJEGE sio NJIGI. Asante wananchi

VICHWA VYA HABARI VYA LEOLEO

 He nyee(wacha nishangae kikwetu) nyee nye nye hifi ni kweli?


Simba 'eye' na French investors 'eye', sipendi kujidanganya kuwa hawa walioandika hapa walienda shule moja na mwalimu wao alikuwa mmoja chini ya chama kimoja......................

20 September 2013

KABANDIKA PLASTA KWENYE MAKALIO

Chekibob kaget krash kwenye mnuso akalewa njwiii, akaondoka huko na chupa nyingine za Nyagi kaweka mifuko ya nyuma ya KATA K yake. Sababu ya ulevi alipofika karibu na kwake akateleza akaangukia makalio chupa zikavunjika na kumchanachana makalio. Akajikongoja mpaka ndani kwakwe, alipovua suruali akaamua kujitibu kwa kubadika plasta kwenye vidonda, basi kwa msaada wa kioo cha kabati lake akawa anajiaangalia palipo na kidonda na anabandika plasta. Hatimae akaona amefanya kazi nzuri akajitosa akalala...... Asubuhi alipoamka, akashangaa kioo chote kimebadikwa plasta na makalio yanauma

WE BWAN WE HAP PANAITWA NINI?

Watani zangu waliokuwa wanaingia kwa mara ya kwanza na basi katika jiji la Dar es Salaam walikuwa wanabishana namna ya kutamka jina hilo, mmoja akasema Darislamu mwingine akisema Daslam. Waliposhuka tu kwenye basi wakamwona jamaa mmoja baada ya salamu wakamwambia 'Bwanawewe si tunu ubishi, hebu sema wewe polipoli hapa panaitwa wapii?' Jamaa akawaambia, 'Hapa panaitwa UUUU BUUUU NGOOO'

KITU HICHO, VIDEO YA BLUU, UKIMALIZA FUTA DELETE KABISA

MAMBO MAZITO VIDEO YA BLUE, WATOTO WAKAE MBALI UKIMALIZA FUTA DELETE KABISA!!!!!!!!!!!!!!!!

UNAPENDA PICHA ZA BLUE? CHEKANAKITIME IMEKUWEKEA HAPA

UCHAMBUZI WA VILE VICHWA


 Alikuwa anatafuta nini kwenye mijumba mibovu jamani?

 Bonge ya ahadfi sijui atakuwa kocha huyo, lazima alisema "Mkifungwa nawauwa"

 Dah hakimu sijui alikaa kwenye kitanda?

Noma Kichizi, mshkaji yuko tol kinoma au vipi?

19 September 2013

CHAMBO HIYO WEWE FALA


TUNATAKA KAZI HATUTAKI NANIHII


SAMAHANI MADEREVA TUNAPUMZIKA KIDOGOOOO


MDOGO WAKE MGOSI MKOLONI AKIWA SHAMBANI


NAJILAUMU KUNUNUA SIMU FEKI DAH


Kweli hawa jamaa simu zao feki. Simu yangu imeanguka, Phonebook imechanika karatasi zote zimepeperuka, na sina sasa hata kumbukumbu moja. Hela zote kwenye Tigo Pesa  zimedondoka watu wameokota yaani nimekula hasara sana, haya huku kwenye Bluetooth meno yote yameng’oka fizi zinatoka damu sana, message zangu nazo zimetapakaa chini watu wanazisoma, najisikia aibu maana message nyingi zilikuwa za siri sana. Rafiki zangu wengi wa kwenye facebook na whatsapp wameumia, kuna mdada mmoja alikuwa mgeni kabisa kakamatwa eti mhamiaji haramu, password  zangu zote zimeharibika kabisa sina raha najilaumu kwanini nilinunua simu feki.

NIPE MIMI HIYO TENDA MKUU

Jamaa watatu walienda kuomba tenda ya kujenga uzio wa nyumba ya serikali,
MJENZI 1: Mimi naweza kujenga uzio kwa shilingi milioni 12, vifaa milioni sita, wajenzi ntawalipa milioni mbili na mimi nitapata faida milioni nne.
MJENZI 2: Mimi nanaweza kujenga uzio huo kwa shilingi milioni kumi na tatu, vifaa milioni sita, wajenzi milioni mbili na mimi mwenyewe ntapata faida ya milioni tano. 
Mjenzi wa tatu akamwita pembeni mtoa tenda,
MJENZI 3: Sikiliza mkuu mi nataka milioni 42, milioni kumi zako, milioni 20  zangu halafu tunamkodisha yule fala wa kwanza ajenge uzio, imekaaje hiyo?  Akapata tenda mara moja.

VAA UPESI KAITE AMBULENSI WEWE

Jamaa karudi ghafla nyumbani si akasikia sauti za ajabu toka chumbani kwake, akapiga ukelele na kuvunja mlango akamkuta mkewe akitetemeka;
MUME: We vipi?
MKE: Presha imepanda...............jamaa akakimbia sebuleni ili apige simu ambulensi ije wakati anahangaika kutafuta namba ya simu, mwanae akaja 
DOGO: Baba anko yuko uchi kwenye kabati chumbani .........jamaa akatupa simu na kurudi chumbani alipofungua mlango wa kabati akamkuta mdogo wake kabatini bile nguo nae anatetemeka 
MUME: Na wewe vipi? Unazubaazubaa bila nguo kabatini wakati mke wangu ameshikwa na presha. Vaa upesi kaite ambulance

MWANANGU KAOLEWA NA MALAIKA

Akina mama wawili waliosoma pamoja walikutana sokoni baada ya salamu;
ISABELA: Jamani Adela vipi mwanao?
ADELA: Kwa kweli mwanangu kaoa mwanamke mchawi, kamloga kamuinamisha mwanangu, we fikiria, mwanamke anaamka saa 5, akiamka hapo ni kuzurula mji mzima kutumia pesa za mwanangu, mwanangu akirudi kachoka jioni, hakuti chakula, badala yake hao wanaenda kula kwenye mahoteli ya gharama, yaani we acha tu. Vipi binti yako?
ISABELA: Mtoto wangu kaolewa na malaika, mwanaume anaamka alfajiri anamtengenezea binti yangu chai anamletea chumbani, anamuachia pesa nyingi za kutumia kwenda kununua anachotaka, kila siku akirudi anampeleka kula kwenye hoteli za gharama maisha yao kwa kweli mazuri sana

MBONA ZOTE RANGI MOJA?

MKAKA kaingia duka la nguo na kamnunulia swity wake chupi dazani moja zote za rangi moja, akaenda kumzawadia. Mupenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote rangi moja si akalopoka.
SWITY: Sasa umeninunulia chupi zote rangi moja, watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili................................... Hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
MKAKA:Watu gani hao? Leo utanambia'

UCHAMBUZI WA VICHWA VYA HABARI KADRI YA MHARIRI WETU CHIZI FRESHI

 Hahahahaha jamani ilitakiwa tuonyeshwe video ya hili, pata picha polisi wako pale wanamsuta mtu, wanamtia masinge, na kusutana kunahusu kujifunga kitenge kiunoni hahahahaha

 Ohoooo sasa hii inakuwa mbaya, mnapiga roba mpaka timu dah

 Kwa vyovyote Rooney hawezi kukubali malipo ya kiana hii

 Ngoja tumpe dada isiwe tabu

John Kitime
Juma Katundu
John Kijiko