HATUPIMI BANDO

20 August 2013

YAANI MKE WANGU HAELEWI KABISAAA

Mfugaji mmoja kakutwa bar kalewa wakati kwa kawaida hanywi pombe.
RAFIKI:He vipi tena hata wewe leo umelewa
MFUGAJI: We acha bwana we acha, nimechanganyikiwa hapa
RAFIKI: Kuna nini nikusaidie?
MFUGAJI: Alfajiri nimeamka ili nikamkamue ng'ombe maziwa. Leo ng'ombe kawa mkorofi sana hataki kukamuliwa anatupa mateke hovyo, nikatafuta kamba nikatanua miguu nikamfunga kwenye  nguzo, kisha nikaunyanyua mkia nikaufunga kwenye kenchi, nilipomaliza kazi hii nikaamua kukojoa kabla ya kuanza kumkamua, ile namaliza kukojoa si mke wangu kaingia.
MKE:Heee mume wangu unamfanya nini ng'ombe?
Nimejaribu kumueleza kuwa nilikuwa namtayarisha ng'ombe kumkamua haelewi kitu

1 comment:

Itika Majivuno said...

Mke alikuwa sahihi, kwanini alimfunga na mkia? Na tabia ya kukojoa hovyo iachwe!