PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KAMA HUPENDI JOTO USIINGIE JIKONINdugu zangu najua mnasubiri kwa kuwa nilisema nitawataja, sasa ni kuwa limetokea tatizo la kiufundi, fundi mitambo kapata malaria sugu sasa baada ya kutafakari kwa kina ndio ikaonekana ni muhimu tujali afya ya mwenzetu kwanza na kwa  hiyo, tumechukua uamuzi mgumu na kupeleka Australia akatibiwe, atakaporudi ndio atafunga mitambo ya kutangazia halafu ndo ntawataja, laiv bila chenga.
Najua wengine mtaanza kuleta maneno, “Ohh si uwataje tu bila fundi mitambo”, Hapa lazima tuelewane, mambo haya lazima yafuate taratibu, kila kitu kinaenda kwa taratibu, hata ukitaka kulala kuna taratibu unaanza kukung’uta miguu ndio unapanda kwenye kitanda. Kwa hiyo nawaomba wasomaji wa chekanakitime, mvute subira najua nyinyi ni watu watulivu hamna fujo, mkidangwanywa sorry yaani samahani limeniponyoka, mkielezwa mnaelewa bila matatizo aksante saana. Kwanza hii si mara ya kwanza ilikuwa watajwe, na kwa muda wote huu mmeonyesha uvumilivu na uelewa wa hali ya juu na kutulia kusubiri watajwe ikiwa huu ni mwaka wa tano sasa mnasubiri kwa utulivu wa hali ya juu, tuendelee na hali hiyohiyo kwa hiyo nyinyi ni watu wema sana. Mtu mwema pepo ni yake

Comments