PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HALELUYA ALIKUWA KAZIMIA

MUME karudi alfajiri kusha anza kuwa kweupeeee
MKE: Jmani ndio unarudi saa hizi ulikuwa wapi?
MUME: Dizasta mke wangu, simu yangu iliisha chaji na tulikuwa tunakunywa na rafiki yangu Devi, akapigiwa simu dada yake kafariki, basi tukachanganyikiwa ikalazimika nikeshe huko mpaka asubuhi hii
MKE: Loh jamani poleni. Ngoja nikutengee maji na nikuweke chai harakaharaka maana ntalazimika nami nitoke asubuhi hii hii
MUME: Unaenda wapi?
MKE: Jamani si ntalazimika kwenda kwenye msiba wa mwenzetu?
MUME: Nilikuwa sijakumalizia, si asubuhi hii wamekwenda mochwari, haleluya Mungu mkubwa, kumbe yule dada alikuwa kazimia tu

Comments

Anonymous said…
Ha ha haaa!! Itabid Mke akamuone na kumpa Hongera huyo aliefufuka! Kimbembe hicho.