HATUPIMI BANDO

30 August 2013

WAHARIRI FEKI WACHAMBUA MAGAZETI YENU

 Ngumu kuelewa hii lugha ya gazeti hili kuhusu kitendo cha Msigwa. Hatuchambui chochote hapa tunataarifu tu, lakini mmhh

 Jamani madebe tena ya nini? Pigeni makofi itatosha, madebe ni kelele sana mjengoni..........

Enzi mhariri alipokuwa mdogo, watu walukuwa wanaanika unga, sasa wanaanikwa wauza unga, hiki kimbembe

29 August 2013

AUNTY TUNAOMBA MPIRA WETU


WENZIO WOTE TAYARI KWANINI WEWE HUTAKI?

Yaani naamulia kesi kubwa, jamaa yangu Mzambia kaja kushtaki, mke wake kamshikia bango leo kamuuliza swali swali ambalo ndio linaleta kesi kubwa.
MKE: Hivi mume wangu kwa nini hutaki kutahiriwa? rafiki zako wote wametahiriwa

23 August 2013

BAADA YA BODI KUJA JUU MHARIRI AANZE TENA KUCHAMBUA VICHWA VYA HABARI

 Huyu lazima kavalishwa sanda, jezi gani tena ya marehemu kuliko hiyo?

 Mkuu sijui alikuwa anawashwa maana hawa waandishi wanaleta utata

 Ngoja Jumamosi niende Njenje nikamuulize Waziri Ally Kisinja kama wameibuka Mawaziri feki au bado yuko peke yake

Ni kweli polisi wengine wana nywele ndefu sana, imeshakuwa tabu sasa

22 August 2013

NAKUMBUKA NILIPOKUWA MWANAUME

Mbongo kaenda Thailand, katika zunguka yake akapata mpenzi wakaenda hotelini kwake na kulala mpaka asubuhi. Asubuhi yake mdada wa KiThai akawa anaonekana hana furaha;
MBONGO: Vipi honey mbona unaonekana huna raha?
MTHAI: Nimekumbuka tu enzi kabla sijapata operesheni nilipokuwa mwanaume.

MKE WANGU WE VIPI?Jamaa alikuwa na mke wake akasimamishwa na trafiki,
TRAFIKI: Bosi mbona unaenda spidi 70 kwenye eneo la kwenda spidi 50?
JAMAA:Hapana mzee nilikuwa naendesha spidi 55 samahani
MKE: Mhh mume wangu si useme ukweli ulikuwa spidi 80.
TRAFIKI: Taa za breki za nyuma haziwaki pia
JAMAA: Dah hizo zitakuwa zimeungua leo leo
MKE: Jamani mume wangu si toka wiki iliyopita ulinambia zimeungua utatengeneza?
TRAFIKI: Halafu mkuu hujafunga mkanda
JAMAA: Nimeufungua sasa hivi uliponisimamisha
MKE: Mume wangu toka lini wewe ukavaa mkanda?
JAMAA: hebu kelele na we mjinga mkubwa
TRAFIKI: He huyu jamaa ndio huwa anakukaripia hivi kila mara?
MKE: Hapana huwa anakuwa mkorofi hivi kama amelewa tu.

I CAN BE PRESIDENT BISHA


KWELI SI KWELI?


20 August 2013

KUMBE KALE KAGIA NI KAKUWASHIA INDIKETA

Kirungu

steringi
Blogu yenu yakidijitali www.chekanakitime.blogspot.com imegundua siri kubwa itakayosaidia sana madereva wa Dar. Baada ya kufanya utafiti ambao umeikost blog fedha nyingi za kigeni, blog imegundua kitu mbacho kimekuwa kigumu kukigundua kwa madereva wengi wa Jiji la Dar. Utafiti wa hali ya juu umegundua siri kuwa katika magari yote pale kwenye steringi pana kama vigia vidogo viwili, kimoja kushoto kingine kulia. Vigia hivi kumbe vina kazi muhimu sana. Kwa magari ya Kijapani kale kagia ka kulia kanakazi ya kuwasha taa, halafu kumbe ukikaminya chini utagundua kuwa kumbe ndio kakuwashia indiketa za kulia, ukikapeleka juu kana washa indiketa za kushoto. Siri hii ambayo blog hii imeamua kuiweka wazi itawasaidia sana madereva wa Dar. Blog hii inawaomba madereva mjaribu muone mtashangaa kumbe gari linaindiketa zinafanya kazi. Kwa taarifa indiketa ina kazi ya kuonyesha unakata kulia au kushoto. mara nyingine inasaidia mwenzio anayekufuata nyuma ajitahadhari. Tunategemea Taifa litaizawadia blog hii kwa kugundua siri hii kubwa ambayo madereva wengi wa Dar walikuwa hawaijui.

MARUFUKU KUPATA AJALI HAPA

Kuna madereva wengine wakorofi wanapata ajali kila mahala, sasa ni vyema kuweka kibao kama hiki ili wasiwe wanapata ajali hovyo bila mpango. Blog hii inaishauri serikali yetu sikivu kuweka mabango haya kwenye barabara zetu ili kulinda maisha ya magari yetu.

ACHA KULIA HUJUI WAHENGA WALIKUWA NYANI?


YAANI MKE WANGU HAELEWI KABISAAA

Mfugaji mmoja kakutwa bar kalewa wakati kwa kawaida hanywi pombe.
RAFIKI:He vipi tena hata wewe leo umelewa
MFUGAJI: We acha bwana we acha, nimechanganyikiwa hapa
RAFIKI: Kuna nini nikusaidie?
MFUGAJI: Alfajiri nimeamka ili nikamkamue ng'ombe maziwa. Leo ng'ombe kawa mkorofi sana hataki kukamuliwa anatupa mateke hovyo, nikatafuta kamba nikatanua miguu nikamfunga kwenye  nguzo, kisha nikaunyanyua mkia nikaufunga kwenye kenchi, nilipomaliza kazi hii nikaamua kukojoa kabla ya kuanza kumkamua, ile namaliza kukojoa si mke wangu kaingia.
MKE:Heee mume wangu unamfanya nini ng'ombe?
Nimejaribu kumueleza kuwa nilikuwa namtayarisha ng'ombe kumkamua haelewi kitu

YULE MBONA HALII

Ilitokea bonge ya ajali. Jamaa mmoja alikuwa kakatika mkono na analia kwa kelele.
MJAMAA: We acha kulia bwana, ona yule jamaa pale kakatika kichwa kabisa halii

HOTUBA ILIYOTUKUKA YA BWANA HARUSI WETU

MC: Na sasa tupate maneno machache kutoka kwa bwana Harusi
BWANAHARUSI: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu. Pili nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii. Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii. Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa kuniazima  suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki kwa kutuazima keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana. Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu. MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa

SASA SI MUANDIKE KISWAHILI TU ANGALIENI MLICHOANDIKA


VIP TOILET CHEZEA WEWE


19 August 2013

AISE NI KWELI LAINI HIVIHIVI

Devi alikuwa anapenda sana kutania wenzie, siku hiyo kamkuta Gwalu kajiinamia kashika tama kwa mawazo makali, kwa uchokozi akamshika mwenzie mashavu;
DEVI: Vipi mshkaji mbona mawazo sana? , changamka bwana angalia mashavu yako laini kama tako la mke wangu
GWALU: Aise hapo nimechangamka, umenikumbusha matakao ya mkeo yalivyo laini.........
Devi haraka sana akakunja ngumi anataka kupigana

KICHWA CHA HABARI CHA LEO18 August 2013

BABA AMKA CHAKULA TAYARIDah mambo mengine bwana, juzi nilipita pale Sinza darajani nikielekea home nikaona mfuko umetupwa, kuuangalia ndani nimekuta dola 20,000. Niwe mkweli woga na furaha vyote  vilinishika nikaangalia kushoto na kulia nilipoona watu hawanioni nikachukua ule mfuko na kwenda haraka home. Nilipomwaga kila kitu nikakuta vitambulisho, kadi za ATM, makaratasi mengi na iphone, nilitaka kuzima simu nitoe sim kadi lakini nikaacha roho ikanisuta kuwa mwenye mali anaweza akanipigia. Na kweli baada ya muda si mrefu simu ililia na kwa maelezo ikawa wazi mali zile ni za aliyepiga simu, nikamuelekeza niliko akaja kuchukua mzigo wake akanipa dola 2000 nikakataa kistaarabu, akachukua namba yangu akaondoka. Jana akanipigia simu kuwa yuko nje ya nyumba yangu alikuwa kaja na NOAH mpya kabisa, akanipa ufunguo na kuniambia hiyo ni zawadi yangu kutokana na tabia niliyoonyesha. Nikamshukuru sana wala sikuamini macho yangu, ile nataka kuwasha gari nilitest si nikasikia,'Baba baba amka chakula tayari'

INJINIA WA UJENZI AGOMA KUZUNGUMZIA UBUNIFU WAKE

Baada ya kukutwa kagundua stail mpya kabisa ya ngazi, injinia moja wa ujenzi amegoma kabisa kuzungumza na blog hii feki kuhusu ubunifu wake ambao watu ambao wala sio mainjinia wameanza eti kuukosoa. Watu hawa wa ajabu ambao hawataki kabisa kumpa injinia 'natural justice' ajitetee kwa ubunifu wake wa hali ya juu wameanza kumlaani. Blog hii ambayo inategemea kuwa na ofisi ghoroya tatu ya jengo hili inapongeza ujenzi huu ambao utaweza kupunguza kasi ya wasumbufu katika maofisi.

TUMIA ATM WATAKUZIMIKIA

Jamaa kajiunga na GYM iliyokuwa na mashine kadhaa za mazoezi, na hapo ndani kukawa na madada kibao wanafanya mazoezi, jamaa kachanganyikiwa, akawa mara ahamie mashine hii mara ile ili wadada wamuone mkali, lakini yote ikawa bure. Hatimae akamuendea mwalimu wa GYM na kumuuliza; Jamaa: Aise mashine gani nikitumia hawa madada watanizimia? Mwalimu: Hebu jaribu kutumia mashine ya ATM hapo nje ya GYM, lazima watakuona we mkali.

KAMA HUPENDI JOTO USIINGIE JIKONINdugu zangu najua mnasubiri kwa kuwa nilisema nitawataja, sasa ni kuwa limetokea tatizo la kiufundi, fundi mitambo kapata malaria sugu sasa baada ya kutafakari kwa kina ndio ikaonekana ni muhimu tujali afya ya mwenzetu kwanza na kwa  hiyo, tumechukua uamuzi mgumu na kupeleka Australia akatibiwe, atakaporudi ndio atafunga mitambo ya kutangazia halafu ndo ntawataja, laiv bila chenga.
Najua wengine mtaanza kuleta maneno, “Ohh si uwataje tu bila fundi mitambo”, Hapa lazima tuelewane, mambo haya lazima yafuate taratibu, kila kitu kinaenda kwa taratibu, hata ukitaka kulala kuna taratibu unaanza kukung’uta miguu ndio unapanda kwenye kitanda. Kwa hiyo nawaomba wasomaji wa chekanakitime, mvute subira najua nyinyi ni watu watulivu hamna fujo, mkidangwanywa sorry yaani samahani limeniponyoka, mkielezwa mnaelewa bila matatizo aksante saana. Kwanza hii si mara ya kwanza ilikuwa watajwe, na kwa muda wote huu mmeonyesha uvumilivu na uelewa wa hali ya juu na kutulia kusubiri watajwe ikiwa huu ni mwaka wa tano sasa mnasubiri kwa utulivu wa hali ya juu, tuendelee na hali hiyohiyo kwa hiyo nyinyi ni watu wema sana. Mtu mwema pepo ni yake

16 August 2013

DINGI NIAZIME BUKU KUMI BASI

DOGO: Baba ingekuwa unanithaminisha na pesa, mimi thamani yangu shilingi ngapi kwako?
BABA: Dah mwanangu wewe sawasawa na mamilioni na mamilioni ya shilingi kwangu
DOGO: Baba niazime alfu kumi tu

BABA ETI MTU STUPID NDIO YUKOJE?

DOGO: Eti baba mtu stupid yuko je?  
DADDY: Hilo ni swali zuri sana, a very good kweshen kwa kweli I am praud of you,ni wazi kuwa kuna kila sababu ya kukiri kuwa elimu unayopata inaendana na mtizamo mzima wa big results now, you see mwanangu, mtu stupid ni yule ambaye akiulizwa just a simpo kweshen, yaani swali dogo sana basi huanza kulinyumbulisha na kuongeza mofimu na fonimu katika hilo swali, kuanza kutafuta, tena infact bila mantiki yoyote wala kufuata basis ya swali, na baada ya hapo kufanya mchanganuo usio na mashiko yoyote na hatimae kukam up na solushenz ambazo in prinsipo hazikuweko katika swali husika kiasi cha kwamba aliyeuliza swali anakuwa haelewi hata kitu, umeelewa  
DOGO: Hapana

NILIKUWA NAWAHI HARUSIJumamosi fulani Trafiki kamkamata jamaa aliyekuwa anaendesha gari spidi, kila jamaa alipojaribu kujitetea Trafiki hakusikiliza, ila akamwambia mhalifu , 'Kwanza twende kituoni sitaki kusikia chochote'. Walipofika kituoni askari aliendelea na shughuli zake akatokea baada ya masaa mawili na kumweleza mhalifu, 'Nyie madereva wakorofi sana, nikikuachia utadai eti nimechukua rushwa, kwa hiyo kesi yako italazimu tumsubiri Mkuu wa Kituo kaenda kwenye harusi ya binti yake akitoka huko na furaha zake labda atakuachia'. Mhalifu akajibu kwa upole, 'Afande sidhani kama atarudi na furaha maana mie ndie Bwana Harusi, hivi nilikuwa nakimbilia kanisani niwahi kuoa".

USIPATE TABU SIKUTOSI BAHARINI

Jamaa alimkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia, akamuuliza shida, yule mdada akasema maisha yamemshinda anaona heri ajiue, maana maisha hapa Bongo shida tupu, kazi hapati madeni yanazidi. Jamaa akamwambia kuwa yeye ni baharia kwa hiyo kama akikubali atamuweka kwenye boksi kisha atamficha kwenye meli yake na wataweza kusafiri mpaka Ulaya wakifika huko atamuoa. Bibie akaona heri hilo, akaingia kwenye boksi jamaa akambeba na kweli mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli, jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe analala huko kwenye hako kastoo, akimhakikishia mdada kuwa wanakaribia visiwa vya Komoro, na kisha hutoka na kuendelea na shughuli. Ilipita wiki ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo hicho, alipoulizwa anatafuta nini mle?, akalazimika kueleza kila kitu, na kuwa anamuomba nahodha asimtose baharini bali amlinde mpaka watakapofika Ulaya. Nahodha akaanza kucheka mpaka machozi yakamtoka, 'Wala usipate taabu mama, siwezi kukutupa baharini, ila jamaa yako kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni, tukifika huko shuka uende kwenu'

NAOMBA UNIUZIE TINDIKALI

Mdada kaingia duka la kemikali, kamkuta mfamasia mwanaume wa makamo hivi;
MDADA: Naomba tindikali kuna mshenzi mmoja nataka kumtia adabu. 

MFAMASIA: Mama mbona unataka kuniweka kitanzini , hiyo sitakuuzia, labda uje na cheti cha daktari hahahahaha....... (Mdada akatoa picha inamuonyesha mumewe yuko kitandani na mke wa huyo mfamasia.....)
MDADA: Cheti cha daktari hiki hapa
MFAMASIA: Kumbe una cheti, haya unataka kiasi gani cha dawa, na leo tunafanya promo dawa bure

AUNTY NISAIDIE

Duh nimeisoma barua hii kwenye gazeti moja jamaa anaomba ushauri, kaandika hivi;
Aunty Fatu, tafadhali nipe ushauri katika hili tatizo langu. Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi katikati ya jiji, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi na taxi, wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu alikuwa mkali kwelikweli. Ni kweli sijawahi kumuuliza kuhusu wasiwasi wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, wakapanda taxi nami nikawafuata  na wakaishia kuingia kwenye gest moja pale Kinondoni, nikaona ni vizuri niangalie saa nijue ni saa ngapi wameingia mle kwani itanisaidia katika ushahidi wakati wa kesi hapo baadae, si ndio nikagundua saa yangu imesimama, saa hii ni Rolex na nilipewa na bosi wangu mzungu kazini alinunua kwao huko Uswisi, na ni expensive sana, sasa je, unanishauri nimrudishie bosi akaitengeneze kwao? au ninunue nyingine?

TUANZE KULIPANA KWANZA

JAMAA: Dokta nisaidie nina tatizo kubwa la kusahau sahau
DOKTA: Nilipe kwanza halafu nikutibu

TRAFIKI WA KIONGOKIONGO AKUTWA TABATA

Trafiki feki akutwa kazini Tabata, trafiki huyu ambaye vyombo vya usalama vinamchunguza kama alitengenezwa Uchina amekuwa akifanya kila kazi yao hata kula vichwa.

14 August 2013

ROBERT MUGABE KIBOKO HATA CHEKANAKITIME HAWAONI NDANIMWANDISHI MUINGEREZA:Mr President don't you think 89 years old would have been a great time to rest and retire?

PRESIDA ROBERT MUGABE: Have you ever asked Queen Elizabeth this question or is it just for African leaders?

12 August 2013

NAFASI ZA KAZI


Part Time Stand-Up Comedians / Wachekeshaji
Do you think you have it? Are you funny? Come for auditioning for standup comedians Thursday 15th August 2013. Starting 5 o’clock at Mayfair Plaza Mikocheni.
Unadhani una kipaji cha kuchekesha? Basi njoo ujaribiwe kipaji chako ambacho kinaweza kukupatia ajira.
Fika Mayfair Plaza, Mikocheni . Alhamisi 15/08/2013 kuanzia saa kumi na moja jioni.


WANGEKUWA AKINA BI FULANI WANGESEPA ZAMANIIII


Wangekuwa akina Bi Fulani wale wa Whatsapp na Instagram wangesepa mapemaaaaa, nyumba zinazoonekana hapa wangeona  hazina swagaaa. Nilimsikia mmoja akisema yeye bila kuachiwa laki tano kwa wiki haelewi somo

NACHUKUA WOTE WAWILI

Mdada alienda super-market kununua kuku, bahati mbaya kwenye frij kulikuwa na kuku mmoja tu, muuzaji akamtoa akamuweka kwenye mzani, akaonekana ana kilo moja na robo. Mdada akamuuliza muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji akamchukua yule kuku na kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu akamtoa tena kwenye friji na kumrudisha kwenye mzani, safari hii akagandamiza mzani kwa gumba, kuku akaonekana ana kilo mbili. Mdada akasema ‘Duh afadhali huyu mkubwa kidogo, naomba unifungie nawachukua wote wawili’

WE MJUKUU MJINGA SANA

Babu kaenda kumtembeza mjukuu wake kwenye makaburi ya kijiji;
BABU: Unaona kaburi hili huyu jamaa alikuwa mtu, nilimkopesha fedha, akajitahidi sana kunilipa, kwa bahati mbaya alikufa huku namdai alfu hamsini. Nina uhakika huyu kaenda mbinguni alikuwa mtu mzuri sana.........wakaenda kaburi jingine
BABU: Sasa huyu alikuwa mshenzi sana alikopa laki yangu hakunilipa makusudi mpaka akafa na deni langu. Huyu lazima yuko motoni
MJUKUU: Dah babu ukifa una bahati kweli
BABU: Una maana gani na wewe?
MJUKUU: Yaani babu ukifa ukienda mbinguni kuna hela zako, ukienda motoni kuna hela zako
BABU: Mjinga mkubwa twende nyumbani

JAMANI HAPA NI DRY CLEANER TAFADHALI

Fulo na Gulo walipoingia mjini kwa mara ya kwanza, walipita sehemu fulani wakakuta tangazo, suruali 1,500/-, shati 500/-, suti 3,000. Wakakubaliana kuwa wakichukua mzigo wa nguo na kurudi nao Bombambili wakiuza watapata faida safi sana. Gulo akamwambia Fulo, " Kwa kuwa wewe kiswahili chako kibovu watatushtukia kuwa tumetoka kuliiii, wacha niingie nikaongee mimi". Basi Gulo akaingia kwa mbwembwe sana,
GULO: Nataka vitu kadhaa toka dukani kwako, suti 100, mashati 1000, suruali 1000. Nifungie vyote nasafiri navyo
Mfanyabiashara: He mzee umetoka kule nanihii?
GULO: Haa umejuaji?
Mfanyabiashara: Hii dry-cleaner bwana hatuuzi nguo hapa, tunafua na kupiga pasi tu.

11 August 2013

JANA WALA SIKUWEPO NYUMBANI HAHAHAHAHA

JIRANI: Hoyaa Devi wakati uko faragha na mkeo uwe unafunga mapazia, jana usiku mtaa mzima tulikuwa tunakucheka ulipokuwa na mkeo
DEVI: Hahahahahaha nyie ndio mnachekesha, jana wala mie sikuwepo nyumbani hahahahahaha

DIA INGLISH TISHER DUDU MONI


Umerudi na maksi mbovu toka shule, baba yako anaamua kumuandikia mwalimu barua ya kulaani ufundishaji wa siku hizi, ana muandikia mwalimu barua ifuatayo, Je utaipeleka kwa mwalimu…………………….
Dear  Inglish teasher,
please i not like how you gived my children 2 of 10 in ezam. I having look at the thing he is colect so why you gived him 2 of 10? What is the why for the little mark? Yours, hungry palent!!

FUTA DELETE KABISA ...OHOOO SHAURI ZAKO MI SIMO


7 August 2013

KAKA DEVI UNA ROHO NZURI SANA

Mdada mmoja mrembo sana alikuwa kapewa talaka na mumewe akahamia a watoto wake wawili nyumba aliyokuwa kapanga ndugu yetu  Devi. Bwana Devi alipomuona mpangaji mpya roho yote ikamtoka. Akajitahidi kila njia kumuonyesha kuwa nae yupo na ni bachela, mdada akawa anaendelea na shughuli zake bila hata kuonyesha dalili za kumwona Devi. Jioni moja Devi akiwa kapumzika akasikia hodi kwenye chumba chake, alipofungua akakutana uso kwa uso na mdada mpangaji, kapendeza sana na akiwa kavaa kimini cha nguvu;
MDADA: Samahani kaka Devi, yaani nimekaa muda mrefu mpweke nimeona leo lazima nitoke nikajirushe kidogo kisha nipate bwana niondoe uchovu. Vipi we uko free unisaidie?
DEVI: Mimi sana tu niko free sina kitu chochote ninachofanya jioni hii, yaani niko free kabisa si unaona mwenyewe niko free sina ishu kabisaaa
MDADA: Loh nakushukuru sana kaka yangu, basi ngoja nikuletee watoto wangu ushinde nao mpaka ntakaporudi

POMBE SI CHAI, SIKUKUU INAKUJA UKIKUTWA HIVI ITAKULA KWAKO


YAANI NIKIKUKAMATA UTANITAMBUA MIE NANI


MDADA AOMBA USHAURI KWA ANKO KWENYE FACEBOOK


Anko,
Vipi mzima? Naomba unisaidie. Huu ni mwezi wa nne toka nimeolewa, yaani tayari najilaumu sana kuhusu ndoa hii. Kabla ya kunioa mume wangu alikuwa anakuja kwangu kia siku na gari jingine, akanambia kazi yake ni dalali wa magari, baada ya miezi mitatu ya ndoa nimegundua kumbe kazi yake ni kuosha magari, hana udalali wala nini. Kwanini alinidanganya vile? Si angenieleza tu ukweli nijue? Ntaendeleaje kumuamini?  Mbaya zaidi mi ni graduate nimegundua kuwa jamaa hakumaliza hata form 4,  Anko what do I do? Wenzangu wameanza kunicheka, wananitumia txt za kejeli. Help me I am confused, sababu nilionywa nyumbani kuwa wanamuona jamaa tapeli nikagombana sana na ndugu zangu. Naomba ushauri
 Baby D

HALELUYA ALIKUWA KAZIMIA

MUME karudi alfajiri kusha anza kuwa kweupeeee
MKE: Jmani ndio unarudi saa hizi ulikuwa wapi?
MUME: Dizasta mke wangu, simu yangu iliisha chaji na tulikuwa tunakunywa na rafiki yangu Devi, akapigiwa simu dada yake kafariki, basi tukachanganyikiwa ikalazimika nikeshe huko mpaka asubuhi hii
MKE: Loh jamani poleni. Ngoja nikutengee maji na nikuweke chai harakaharaka maana ntalazimika nami nitoke asubuhi hii hii
MUME: Unaenda wapi?
MKE: Jamani si ntalazimika kwenda kwenye msiba wa mwenzetu?
MUME: Nilikuwa sijakumalizia, si asubuhi hii wamekwenda mochwari, haleluya Mungu mkubwa, kumbe yule dada alikuwa kazimia tu

6 August 2013

KWANI GLOVU SHILINGI NGAPI?

DOKTA: Unajisikiaje saa hizi?
MGONJWA: Kwa kweli najisikia vizuri sana baada ya opereshen asante dokta mmenirudishia uhai.
DOKTA : Nashukuru, ila kuna tatizo kidogo
MGONJWA: Nini tena?
DOKTA: Tutalazimika kufanya operesheni tena maana tumegundua tumesahau glov tumboni mwako
MGONJWA: Dokta hiyo kitu sahau kabisa, we sema glov shilingi ngapi nikupe hela ukanunue hatobolewi mtu hapa

5 August 2013

KATAKUWA KALE KAMWANAMKE KALOKOLE KALE

Jamaa karudi home na manundu katoka kupigana,
Wife: Kulikoni? Mbona hivyo?
Jamaa: Yule meneja wa kigrosari hapo kona mshenzi kanivunjia heshma imelazimika nipigane
Wife: Kwani vipi?
Jamaa: Eti bila aibu anajitapa kalala na wanawake wote mtaa huu kasoro mmoja tu. 

 Wife: He atakuwa nani huyo? Au katakuwa kale kamwanamke kalokole ka pale kona? Kanapenda sifa sana

BAADA YA SUGARMUMMY KUPATA KASERENGETI BOI....

Sugarmummy kakapata kaserengeti boi akaona kapata bwana, akakatoa out, akakapiga msosi wa nguvu na vijiwain kwa sana huku akikishushia mabusu sana tu, hatimae wakiwa hoi kwa ulevi wakarudi nyumbani kwa Sugarmummy. Wakiwa chumbani kitandani wamepumzika, AC inaguruma kwa mbali, flat screen ikionyesha Big Brother, Sugarmamy akiwa anakichezea kifua cha kaserengeti boi akapumua kwa nguvu kisha akasema kwa mahaba;
SUGARMUMMY: Ninachohitaji sasa ni mwananume tu
KASERENGETI: Hata mimi

HAYA NISUKUME

Ilikuwa usiku wa manane, mtu na mkewe walikuwa wamelala usingizi, ghafla wakasikia mtu anagonga mlango. Mume akaamka na kufungua mlango; MUME: Vipi tena usiku huu? MLEVI: Samahani mzee nina tatizo naomba ukanisukume. Mume akafunga mlango KWA HASIRA na kurudi kulala. Jamaa akaendelea kugonga.
MKE: Kwani anataka nini?
MUME: Mjinga huyo eti anasema nikamsukume
MKE: Si umsaidie mwenzako, hata wewe unaweza ukapata tatizo gari likakuzimikia usiku. Mume akaamka akavaa na kukubali kusindikizana na mlevi akamsaidie......
MUME: Mbona sioni gari?
MLEVI: Subiri, na hatimae wakafika mahala kuna mabembea, mlevi akapanda moja;
MLEVI: Haya nisukume

BINTI SIJAKUKASIRIKIA WEWE

Kigogo mmoja wa hishma alikwenda ziara ya kuhamasisha maendeleo katika mji fulani, akapangiwa hoteli nzuri, wenyeji wake ili kumfurahisha mzee wakakatangulizi kabinti kazuri chumbani kwa mzee. Kigogo ile kuingia kwenye chumba chake akakuta kabinti kazuri kamelala kitandani kwake. Akanyanyua simu na kumpigia mwenyeji wake;
KIGOGO: Aise ndiyo nini hii kuniwekea kabinti chumbani? Nyie mnanionaje mimi? Nimekasirika sana........ Kale kabinti kusikia hivyo kakaamka haraka na kuanza kukusanya vitu vyake ili kasepe'
KIGOGO: Binti unaenda wapi? Mi sijakukasirikia wewe, nimekasirikia hawa wahuni usiondoke

4 August 2013

BREAKING NEWWWWWSSSSSSSSSSSS

Waaandishi na wachunguzi makini wa blog hii wamefanya utafiti ambao umegharimu shilingi milioni tano na kugundua jambo la ajabu sana na ambalo ni muhimu na linaweza kubadilisha msimamo wa serikali kuhusu mambo mengi. Vijana wetu wakakamavu wamegundua kuwa miguu ya wadada inavutia kuliko ya wakaka. Katika uchunguzi huu uliopitia mikoa kama Mbeya Iringa na Bukoba, umeleta majibu haya ya kushtua ambayo yataleta mtizamo mwingine katika ulimwengu wa kisayansi. Kama hamuamini shauri zenu

WAHARIRI WA BLOG HII KIZUNGUMKUTI WAMEGOMA KUCHAMBUA VICHWA VYA MAGAZETI


3 August 2013

TANGAZO CHEKANAKITIME SASA TUNAFANYA KAZI ZA UKANDARASI

Baada ya kuona kuwa blog imefanya kazi ya kuchekesha weeeee lakini matangazo haipati, bodi ya wakurugenzi ya blog imeamua kuhamishia ubunifu wao uliotukuka katika kazi ambayo imeonekana inalipa sana na hii ni ile kazi ya ukandarasi. Hivyo basi blog hii inatangaza kama wewe una inshu ya ukandarasi kama vile kujenga nyumba, bafu , gorofa, choo, chumba cha kupanga, kibaraza na kadhalika tutaarifu, yale mambo yetu ya ten pasenti yako palepale, hakuna ubishi infact sisi tunatoa twenty pasenti kabisa mbele. Pichani ni kazi yetu moja ambayo tumeifanya ya vyoo vya kike vya club moja maarufu, ambavyo vimesifiwa sana na wateja wa kiume. Usipoteze muda wasiliana nasi mapema

CHAMBUACHAMBUA YA VICHWA VYA MAGAZETI

 KIZUNGUMKUTI HIKI....nyie acheni tu

 Leo Jumamosi hatutakiwa kuumiza vichwa

Kimsingi hiki kizungu ni tafsiri ya kile Kiswahili haya kwaherini

2 August 2013

iPEDI


DOGOOOOOO FANYA MABO DOGOOO


FACEBOOK YASABABISHA MAGONJWA MAPYA YA KIDIJITALI SOMA CHUKUA HATUA


Kutokana na matumizi makubwa ya Facebook tayari kumeanza kupatikana magonjwa ambayo yanatokana na hii kitu, katika semina niliyohudhuria jana niliweza kufahamishwa baadhi ya magonjwa mapya kabisa yafuatayo;

1.LIKOSIS.
Huu ni ugonjwa ambao mgonjwa huwa ana ‘like’ kila status na picha yoyote atakayoiona mbele yake. Ugonjwa huu huwapata hasa wale ambao ndio kwanza wanaanza kutumia FB

2.LIKOPHOBIA
Huu ni ugonjwa wa kutoku ‘like’ kitu chochote, ugonjwa huu wanao sana masupastaa wa bongo, maana huwa na tatizo la kisaikolojia kuwa waki’like’ watashuka hadhi na kuwa watu wa kawaida

3.AIBUMIASIS
Huu ni ugonjwa wa kuionea aibu FB. Mtumiaji huingia FB labda mara moja kwa mwezi halafu anaona aibu kuingia tena mpaka mwezi unaofuata.

4. TAG SYNDROME
Ni ugonjwa ambao mwana FB anataka umtag kila picha anayoiona hata isiyomuhusu

5. HATE SYNDROME
Huu ni ule ugonjwa wa mwana FB ambapo yeye huweka status za ‘hate’ tu. I hate life. I hate haters, I hate Dar, I hate CCM, I hate CDM

6. REQUEST SYNDROME
Hapa ni ule ugonjwa wa mwana FB kurequest marafiki bila hata kuwa anawajua anataka tu aonekane anao wengi.

7. COMMENTOLARIA
Mwenye ugonjwa huu, hu comment kwenye kila status itakayotokea mbele yake, yanayomhusu na yasiyomhusu, mradi ka comment

8.MBULULATOSIS
Mwenye ugonjwa huu hucomment utumbo tu kila mara, status na mazungumzo yanaweza kuwa ni ya kuhusu ujio wa Obama, yeye ataweka tangazo la duka lake la simu, au ataulizia Kofi Olomide ana umri gani

 9. ADICTOMIOLOGY
Mgonjwa anaweza kuhisi kufa kama katimiza masaa 24 bila kuingia FB


HERI AIBU KULIKO KIFO


Mke kasikia mumewe ambaye alikuwa safari akigonga mlango wa nyumba yao afunguliwe, naye alikuwa na bwana mbaya zaidi walikuwa wanaishi ghorofa ya kumi na nne, mdada mwasherati akamwambia bwana  waliekuwa nae, aise mume wangu karudi, hebu simama jifanye robot, niachie mie nizungumze; usitikise,
MKE: Karibu mume wangu. Mume akaingia akakuta mtu yuko uchi kasimama;
MUME: Huyu nani?
MKE: Hilo robot nilinunua linanisaidia kujiliwaza wakati wewe haupo.
MUME: Okay poa, sasa mwenyewe nimerudi na mimi nahamu sana na wewe, nipe halali yangu
MKE:Samahani mume wangu, niko siku mbaya pole kwa leo. Ngoja nikutengenezee chai...wakati mke yuko jikoni anatengeneza chai;
MUME: (Akawa anaongea peke yake) Dah mke wangu hawezi na mimi nataka, ngoja nilishughulikie hili robot la mke wangu...... jamaa mgoni kusikia vile akajua hatari inakuja, akaanza kuongea kwa sauti ya kirobot;
ROBOT: Robot bovu halifai, robot bovu halifai
MUME: Duh mi ninahamu  hata robot nalo bovu, upumbafu sasa silinajaza tu nafasi humu? kama bovu ngoja nilitupe nje....Jamaa Robot akajua kifo kinakuja, gorofa ya kumi na nne mchezo? akaona ajisevu; heri aibu kuliko kifo
ROBOT: Robot limepona, robot limepona halina matatizo, halina matatizo

NIMEOTA KANIBA...KANIBAKA KWELI

Mangi alikuwa mahakamani kashtakiwa kwa kosa la mauaji. Akaruhusiwa kuanza kujitetea; MANGI: Mheshimwa mi ninatatiso maku..makubwa kweli, kila nikiota ndoto inakuwa kwee.... inakuwa kweli. Niliota mke wangu kasaa mapacha ikawa kweli ikawa  kweli akasaa mapaa...mapacha. Nikaota duka langu wamefunja, nilipoamka nikakuta wamefu....wamefunja kweli. Mwesi uliopita sinikaota kari yangu mpya imeungu...imeungua, siku mbili badae si ikaungua. Sasa nililasimika kumuua Gody kwa kuwa usiku niliota ananiba....... ananibaka, msee hakimu inkekuwa wewe ungekubali?

SISI VAYANGA SIO SAVA NA VALE VASIMBA..soma na kusikiliza hapa laiv

Tatizo moja sie naona kuva sisivayanga iko kuba kuliko vale vasimba. Sisi iko na vatu vengi vao vako vatu dogo, so nani nasema vao na sisi vote napata ikwal shea? Sisi iko vakuba bana so sisi hapana kubali hii gao nyinyi nataka kumpa sisi. Hata kama naangalia kule UK vale Manchesta vakicheza na Asnal, ve naona Chelsi TV naonyesha vao? Haivezekani kwani vale taonyesha pale timu pinzani napigwa chenga apana naonyesha timu pinzani nafunga goli. Vi do not agree na hii. Halafu hava vatu namaliza piriod yao mezi jayo vasisain kitu oote vala vasipate shahara, vala vasicheke na sisi paka takapoingia ile wiongozi mupya, sava au sio sava? Ve naona iko sava? Sisi vayanga apana naona iko sava.

ETE LISTI NA SISI WABONGO KUNA KITU TUNAWEZAAAAA

YA ETE LISTI KUMBE JAPO KUWA TUNAWEZA KURUKA KAMBA KWA UFASAHA NA KIPAJI CHA HALI YA JUU. UMEONAEE

1 August 2013

KIZUNGUZUNGUUUUUUU


MABOSI WARUDI OFISINI BAADA YA KUKOSEKANA KWENYE SEMINA YA TCRA, WAANZA KUCHAMBUA VICHWA

 Sheshe tena bonge la sheshe, ishu ngumu hii, madenti itakuwaje sasa?

 Oyaa mshikaji umepata shilingi ngapi? Au wanakusingizia maana hii itakuwa ya kwanza duniani

 Dah sasa mambo magumu kweli Ticha kahamia toilet

 Sasa nani mkweli kati ya nyie wawili? Na huyo hapo juu?

  Kwa hiyo Yanga mida hii haina maini

Huu ni uwanja wa ndege madudu yanatafuta nini? Madudu yaende uwanja wa Madudu, siyo kuchanganya mambo, maana ndege lazima wataanza kula madudu

ILE RUSHWA ULIYONIPA IMESAIDIA SANA

Jamaa alikuwa na kesi nzito ya mauaji, ikafikia karibu na wakati wa kutoa hukumu, akahisi wazee wa baraza watamuona ana hatiana na anaweza akanyongwa, basi akampata mzee mmoja wa baraza akamhonga ili ashawishi wenzie wasimpate na kosa la mauaji ya kukusudia, ila japo liwe kosa la mauaji bila kukusudia ili afungwe tu. Kweli baada ya siku tatu wazee wa baraza wakakubaliana kuwa jamaa aliua bila kukusudia, Jaji akampa adhabu ya kifungo cha  miaka saba, akashukuru. Alipopata nafasi ya kuongea na mzee aliyemhonga;
MFUNGWA: Mzee nashukuru sana nategemea sikukupa kazi nzito
MZEE: Loh ilikuwa kazi nzito sana, wenzangu wote walikuwa wameona huna hatia hivyo kuwabembeleza wakubali kuwa umeua bila kukusudia ilikuwa ngumu sana, nimelazimika ile hela yako kugawana na wengine waniunge mkono.

UNATAKA NIUWAWE? UNATAKA NIWE WA 20?

Waifu wa jamaa mmoja alikuwa akisumbuliwa sana na njemba fulani iliyokuwa ikimtaka kila siku, hatimae waif akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, "Unajua watu kama hawa dawa yao ndogo tu,we mkubali tu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu". 
Mamaa akafuata masharti ya mumewe na hatimae akaweza kuirubuni njemba hadi wakaingia chumbani, mume akawa tayari na panga uvunguni mwa kitanda anangojea signo.
 Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona njemba ina makovu makubwa kifuani na mgongoni akaamua kuuliza, "Hee jamani mbona una makovu hivyo?", Njemba huku ikiendelea kuvua suruali ikajibu," Niwe mkweli mie nina pepo la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nimeshafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania nimewaua". Mamaa akbaki kuduwaa tu. Jamaa alipomaliza kuvua nguo mdada akaanza kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni, mume kabana kimya, kila jitihada za mdada kupunga mkono hazikupata majibu,  mpaka njemba ikamaliza shughuli zake akatokomea.Ndipo mume akatoka uvunguni jasho linamtoka,"Sasa ndio umefanya nini mume wangu? Umeacha nimeshindwa kufanya lolote, kwanini hukutoka jamanii?" . Mume akajibu kwa ukali," We we we, mwenyewe umesikia kasha ua 19 unataka niwe wa ishirini? nauliza unataka niwe wa 20 kusudi muendelee na uasherati wenu?"