HATUPIMI BANDO

15 July 2013

VEVE LETA NYUMA VAGENI NATAKA

JOJI kaenda kuomba kazi ya uboi kwa muhindi, mambo hayakuwa mabaya kwa wiki mbili za kwanza mpaka siku ndugu za bosi walipokuja kula chakula cha mchana. Joji akaambiwa apange meza ya chakula, akaweka vizuri sahani, visu, vijiko lakini akasahau kuweka  uma. Wageni wote wakawa wamekaa kwenye viti vyao , Juma akiwa nje anapumzika, ghafla akasikia; BOSI: Hanee Jojiiii, vee Jojiiii,  lete nyuma..... Joji hakuamini alichosikia, JOJI: Umesemaje Bosi? BOSI: Ve apana sikia, lete nyuma vageni nataka...
Bosi hakujua na mpaka leo hajui ni kwanini Joji alimtandika kama vichwa sita vya mfululizo...............

No comments: