PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UTUMBO WANGU WOTE UMETOKA

Jamaa fulani alikuwa na tabia ya kujamba kwa nguvu kila aamkapo asubuhi. Mkewe alikerwa sana na tabia hiyo, alimkataza akachoka, siku moja akamwonya kuwa iko siku badala ya ushuzi, utumbo utakuja kumtoka. Jamaa alicheka sana kusikia hilo. Siku moja mke alilazimika kuamka alfajiri awatengeze kuku kwa ajili ya sherehe, alipowatoa utumbo wale kuku akakumbuka alichowahi kumwambia mumewe akaamua kumtisha, akamnyatia mumewe ambaye alikuwa bado amelala na kumuwekea utumbo kwenye pajama lake na kurudi jikoni. Muda si mrefu mwanaume aliamka akajamba kwa nguvu kama kawaida yake, lakini akahisi kitu cha baridi ndani ya suruali, ile kuvuta si akakuta utumbo. Akapiga ukelele,’Mama yangu nimekufa’. Mke wake aliposikia akacheka peke yake, akajua jamaa kashaukuta ule utumbo. Kimya cha kama nusu saa kilipita. Hatimaye jamaa akamfuata mkewe jikoni akiwa amelowa jasho pajama nzima.
JAMAA: Mke wangu yale uliosema leo yametokea.
MKE: Yepi jamani?
JAMAA: Mke wangu ulisema nikiendelea kujamba utumbo utatoka, leo utumbo si umetoka kama ulivyosema
MKE: Pole mume wangu, sasa?
JAMAA: Namshukuru Mungu, nimejitahidi nimeusindilia na vidole na nimeweza kuurudisha ndani wote.
MKE: Mungu wangu umefanyaje?

Comments

Anonymous said…
Daaaah....!! Itabid ajizuie asiende haja kubwa manake "utumbo" utatoka tena..!!! Ha ha haaaaa...!!!