PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UTAINGIA CHINI YA KITI? AU YEYE ATAINGIA CHINI YA KITI

Baada ya kushinda machana kutwa na mdada mkila bata, ukimununulia mibia ile ya bei kuanzia 2,500/-, mishkaki kwa sanaaa, mara ya samaki, mara ya nundu, hatimae kama saa mbili ya usiku hivi, unampa hela ya taxi akapumzike, kwa maelezo kuwa gari yako alichukua mjomba wako amekupigia simu atakupitia akiwa na shangazi yako, mdada anaondoka kwenda kupanda taxi kituo cha jirani, baada ya dakika tatu na wewe unaenda barabarani na alfu yako iliyobaki mfukoni unapanda daladala uelekee kwenu, kituo cha pili, macho yenu yanakutana na demu wako katulia kiti cha mwisho kwenye daladala hilo hilo.

Comments