PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

USHAURI WA BLOG HII FEKI KUHUSU BONGOFLEVA KUOKOA SOKA WACHUKULIWA NA KLABU KONGWE YA YA SIMBA

Hatimae timu kongwe hapa nchini imeanza kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na blog hii siku chache zilizopita ukielekeza jinsi ilivyo muhimu kuwatumia Bongofleva kuendeleza soka la Tanzania, hasa kutokana na wacheza soka wenyewe kuonekana wanapwaya sana katika taaluma yao ukilinganisha na ile timu iliyoongozwa na H Baba,  katika makala yanayopatikana HAPA blog hii ilieleza umuhimu wa kubadilisha utaratibu katika soka,  leo hii uongozi wa juu wa club kongwe ya Simba umetangaza rasmi nia inayorandana sana na mawazo hasi ya blog hii kwa kupanga kuanzisha kundi la Bongoflava. Wahariri wa blog hii leo watalala wanachekelea kwa kugundua kuwa kuna watu muhimu wanafuata ushauri wao uliotukuka haya wote tuimbee.....blogu blogu, blogu, blogu hiyo, blogu blogu hiyo, blogu blogu hiyo bloguuuuuuu.

Comments