PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UGANDA 1 -TANZANIA 0, UNAJUA SABABU? MASOGANGE ANAHUSIKA, KUWA WA KWANZA KUSOMA HAPA

Mcheza soka wetu alipokuwa mdogo.


Watafiti makini wa blog hii waliingia kazini ili kujua kwanini tumefungwa leo na Uganda, kwa kweli timu hii makini ya wapelelezi imekuja na majibu makini yasiyo na mantiki yoyote ya  kisayansi kwanini tumefungwa.
1. Ugeni wa Rais Obama umegundulika kuwa ni sababu kubwa sana. Waganda walikuwa wamekasirika kwanini Obama hakwenda kwao , hivyo wakapanga njama za siri kuwa lazima waifunge timu yetu. Masikin vijana wetu wakakamavu na wapole,  bila kujua kuwa wenzao wamekuja na njama ya kuwafunga, tena  kwao wamepigana kishujaa lakini hizi njama za kifisadi na za kisiri zimeweza kufanikiwa. Tunaishauri serikali yetu sikivu iwachongee Uganda kwa Obama, kwanini wameifunga timu ya nchi aliyotembelewa na yeye? Huku ni kumdhalilisha mgeni wetu
2. Mganga aliyetumiwa na timu yetu  kumbe ana vyeti feki vya darasa la saba. Yaleyale ambayo watu walijua yatatokea kutokana na kuzagaa kwa vyeti feki, sasa ona kuna waganga wa kienyeji feki. Viongozi wetu wamemuaproch huyu mganga akaihakikishia timu yetu kuwa itawafunga Waganda 20 - 0, matokeo ndio hayo, na ile pesa ya tenda ya utaalamu ndio imeshaliwa tena. Serikali iangalie na vyeti vya wachawi wetu wa timu, ili kitu hiki kisitokee tena.
3. Kitendo cha watu kusema Masogange kasafirisha mzigo wa kilo 150 wa madawa, kimewashtua wachezaji wetu, wamepata shock wameshindwa kucheza kabisa kwa mawazo

Comments