PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

TIMU YA SOKA YA BONGO FLAVA IPEWE NAFASI YA TAIFA STARS MUONE KAZI

Mambo mengine yako wazi kabisa, yaani Waswahili wanasema hujui kusoma hata picha huoni? Blog hii kabambe inawatangazia rasmi kuwa imesoma alama za nyakati na kugundua kitu kikubwa kabisa. Nani anabisha kuwa Bongo Flava ndio habari ya mujini? Fungua radio, angalia TV full taim Bongo Flava, ni wazi hawa vijana wameweza kufanya makubwa kiasi cha kuweza kuteka nyoyo za wananchi wa Bongo na nchi jirani au siyo? Hata ukibisha habari ndio hiyo. Wiki iliyopita, vijana hawa walionyesha kitu kingine waliweza kuwatandika Bongo Movies 2 - 1 katika soka. Hili si jambo dogo, na ujue hapo walikuwa wametoka kupafom jana yake , je wangekuwa fresh si ingekuwa mvua ya magoli? Picha iliyo wazi hapa ni kuwa hawa vijana mahiri wapewe chans ya kuliwakilisha Taifa na kuteuliwa kuwa timu yetu ya Taifa. Wabishi watakuwepo tu si ndio kawaida, lakini wataalamu wetu wamebaini kuwa hawa kwa kuwa ni damu changa, ingekuwa wao ndio waliokipiga na Cranes jana, wangeweza kuichachafya ngome ya Waganda kwa muda wote wa dakika 90. Wahusika ambao najua huwa hamkosi kusoma blog hii chukueni uamuzi mgumu, vunjeni Taifa Stars na nafasi muwape Bongo Flava muone mambo ya ukweli.
Nawasilisha hoja. Tafadhali Mbunge husika tetea hoja hii

Comments