PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SWAGA ZA MAHAUZIGELO WANYALU

Kila kazi ina swaga zake, nimefanya utafiti wa swaga za mahauzigelo WANYALU, nimegundua yafuatayo;
1. Huwa hawaamini majina yao kama vile Kostanzia, Imakulata,Pelpetua, tena yakifuatiwa na jina la ukoo yana swaga, hivyo kitu cha kwanza huwa ni kubadili majina, na kuitwa Amina, Rozi, Mwajuma, nakadhalika
2. Wakirudi nyumbani likizo hata kama ni miezi sita tu toka wameondoka hapo kijijini ndipo swaga hizo hujitokeza zaidi kwa kuwa na maswali kama; Kile kilima pale kalibu na kanisani bado kipo? Au yale mawe kilimani yamewekwa na nani? Hivi nyie mbona hapa hakuna saluni? DSTV mnalipiaga wapi? Leo sijui nani katoka Big blaza?
3. Lafudhi yao inategemea walikuwa wanafanya kazi kwa nani, aliyekuwa anafanya kwa muhindi usishangae akikuuliza, 'veve naitwa nani?' Aliyefanya kazi kwa Mchaga utamjua kwa kihehe chake chenye lafudhi ya Kichaga.
4. Si ajabu akikaribishwa ugali kwa matembele akajidai eti hajazoea. UTAFITI UNAENDELEA...............

Comments