PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SERIKALI YAFANYA TATHMINI YA VYETI VYA SHULE, NESI MOJA PEKEE AKUTWA NA VYETI HALALI

Hali ni mbaya, serikali imetangaza kuwa imekuta vyeti feki zaidi ya mia sita vilivyowakilishwa na watumishi wa serikali. Katika hali ya kushangaza katika hospitali moja mfanya kazi mmoja tu nae ni nesi  ndie pekee kakutwa na vyeti halali, yaani hata wagonjwa wamekutwa na vyeti feki vya hospitali.  We fikiria mpaka hata wagonjwa wamefoji vyeti vya matibabu kweli tunakokwenda kugumu, iko siku tutakuwa na rais feki kafoji matokeo ya uchaguzi.
Nesi huyu ambaye kajikuta ghafla akipewa wadhifa wa mganga mkuu wa hospitali ameshindwa kuficha furaha yake na kuanza kucheza Azonto mbele ya wakaguzi kutoka Wizarani. Hongera mnesi we peke yako sio feki.

Comments