PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NDUGU YANGU KAPOTEZA DHAMBI ZAKE, UKIZIONA MRUDISHIE

NINA ndugu yangu mkazi wa hapa Sinza Mori, kanambia aliamua kwenda kuungama dhambi zake kwa padri , akaona ni heri aandike dhambi zake kwenye karatasi ili azikumbuke zote, sasa kapoteza karatasi, hajui kama imeokotwa na wanae au mkewe au majirani. Kifupi kapoteza dhambi zake.Tafadhali ukipita mitaa hii ukiona karatasi imeendikwa...
 -Nilisema uwongo kwa mke wangu mara kumi
 -Nilifanya uasherati mara mia
 -Sikwenda kanisani Jumapili nyingi
 -Nilizini na mke wa jirani yangu na kadhalika nitaarifu
 tumrudishie jamaa dhambi zake.

Comments