PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NDOTO YA KONDA

Konda alikuwa kakasirika sana, abiria alikuwa kagoma kulipa nauli akisisitiza eti yeye ni denti, wakati kila mtu alimuona ni mtu mzima. Konda akamkunja jamaa, wakapigana sana, abiria alipoona anapigwa akaanza kukimbia, konda akamfukuza abiria akaaingia kwenye shimo, konda alipofika pale akakuta yeye hawezi kuingia kwenye shimo, kwa kisirani akaamua amkojolee humohumo kwenye shimo, wananchi waliokuwa karibu wakamhamasisha konda, 'Mnyee huyo, konda mnyee', konda akavua suruali na kulenga lile shimo na kuachia kitu. Hapo ndipo sauti ya hasira ya  mkewe ikamuita, ikiambatana na makofi,'We mjinga unaona sasa matokeo ya bangi zako umekunya kitandani', Duh ndipo konda akazinduka toka usingizini, akagundua kumbe kila kitu alikuwa anaota ila kukojoa na kunya ilikuwa laiv bila chenga,  akajikuta kishaharibu mambo yote kitandani.........

Comments