HATUPIMI BANDO

18 July 2013

KUMRADHI...KUTOKANA NA WAHARIRI KUCHELEWA KAZINI, MFAGIZI WA OFISI ATACHAMBUA VICHWA VYA HABARI LEO

 Siamini kabisa, hifi mtu unawesa kununua tleni? Tena tleni yenyewe ya golofa? Yaani akija bosi ndamchekesa mbaka acheke, eti tleni ya golofa, wacha nijichekee mimi

 Jamani si wawage wanasema JK yupi? inawesa kuwa John Kitime au John Komba, sasa hawa watampa kasi gani laisi msima, watamlipaga silingi ngapi?

Wanaijelia hatali, pale Tandale wameweka kibao wanawesa kukuongesa akili sa dalasani, kama ngufu za kiume simekwisha wanaludisa, halafu hata siku moja sijaona wanaludisa ngufu sa kike, sasa huyu sijui kafanya nini huko Yanga, labda kawafanya wapate magoli mengi. Mi naondoka kabla wabosi hawajaja.

No comments: