PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KIZUNGUMKUTI NDIO HICHOOO

BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Arusha kwenye mkutano, hivyo jitayarishe.
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Arusha kwenye mkutano wa  wiki nzima
MUME (anampigia nyumba ndogo): Mambo safi, wife anaenda kikazi Arusha jitayarishekujirusha wiki nzima
SMALL HOUSE (anamwambia mwanafunzi wake wa twisheni): wiki hii nina kazi fulani hakuna twishen mpaka wiki ijayo
MWANAFUNZI (anampigia simu babu yake,ambaye kumbe ndie Bosi aliyepanga safari ): Babu hakuna twisheni wiki hii nakuja kwako
BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Arusha mjukuu wangu kapata nafasi ya kunitembelea
SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Arusha
MUME: Aise mpenzi jamaa haendi mipango imeharibika
SMALL HOUSE (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida
MWANAFUNZI: Babu twisheni iko, ntakuja wiki ijayo
BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Arusha iko palepale mjukuu wangu hawezi kuja wiki hii

Comments