HATUPIMI BANDO

27 July 2013

KIUKWELI TUMECHEZA SANA, WENZETU WAMETUMIA UCHAWI

Kwa kweli leo tumecheza, lakini bahati haikuwa yetu. Kilichotuponza ni kuwa hatukuwa na watu wakitushangilia sana, wenzetu walipata sapot kubwa ya fanz wao na hiyo inachanganya sana. Kiukweli ni muhimu FIFA kuanzisha sistem timu ikiwa ugenini ishangiliwe. Mtu unacheza lakini uwanja mzima unapiga kelele , kwa hiyo mtu unakosa konseteshen. Pia uwanja ulikuwa mbovu sana una mabondemabonde hasa upande wa goli letu. Refa kwa kweli hakututendea haki kabisa nadhani wenyewe mliona ametoa ile penati ambayo angekuwa refa wa ligi ya Uingereza angepeta tu, maana ndugu yetu hakushika kwa makusudi. Pia kama mliona goli lilikuwa kwubwa zaidi ya saiz tuliozowea. Mi nadhani wananchi mtuunge mkono ili tuweze kujipanga upya kwa ajili ya kujitayarisha kwa ajili ya Kombe la Dunia. Kitu kimoja lazima tuseme, yaani kuna wakati tulikuwa tunacheza tukawa tunajiona pumzi zinajaa na miguu inakuwa kama tumebeba mifuko ya siment, hii ni wazi jamaa walitumia nguvu za ziada, hivyo na sisi next time lazima tutumie wataalamu wetu mbalimbali kukabiliana na tabia hii ya kuloga wachezaji.
KWA PAMOJA TUTAWEZA

No comments: