PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

IRINGA WALIKUWA TAYARI KWA ZIARA YA OBAMA- SOMA RATIBA

Taarifa iliyopatikana katika blog hii ni kuwa wakazi wa Iringa walikuwa tayari kabisa kwa ziara ya Obama, na ifuatayo ni ratiba iliyopangwa ikapangika kutegemea ujaji wa ugeni huo.
Baada ya Air Force 1 kutua Nduli, msafara wa magari ungemchukua mpaka Miyomboni, ambapo angekuwa na dhifa ya chakula cha mchana na wazee wa Iringa pale Babanusa, baada ya hapo angetembelea mabanda ya kitimoto pale CCM na kuangalia jinsi yeye binafsi ambavyo angeweza kuwekeza katika biashara ile. Kisha angeelekea Tanangozi kuangalia mradi mubwa wa ugemaji wa ulanzi, ili kujifunza taaluma hiyo na kuona uwezekano wa kuleta wanafunzi toka Marekani kupata elimu hiyo hapo. Kisha angeenda kuangalia Fuvu la Mkwawa kwa kupitia Weluu , Lulanda hadi Kalenga. Ambako pia angezindua mradi mkubwa wa Bagia ambapo wananchi wameingia ubia na kampuni ya Symbion ili kupata umeme wa kutengenezea bagia. Jioni angepita Miami kwa chakula cha jion na kulala Kihesa tayari kwa safari ya kurudi Marekani kesho yake. LAKINI WATU WAMETIA MTIMA NYONGO WAMEFUTA ZIARA HIYO, MBIFILE SANA

Comments