HATUPIMI BANDO

25 July 2013

HUYO MBWA MUWONGO SANA MCHUKUE TU

Jamaa alikuwa anatafuta mbwa, akapita mtaa mmoja akakuta jamaa anauza mbwa kwa shilingi alfu 50 kila mmoja, lakini jamaa hakuwapenda,
JAMAA: Huna wengine? Hawa hawajanifurahisha
MUUZA MBWA: Ninae mmoja nyumbani namuuza alfu tano, ila huyo anajua kuongea
JAMAA: Duh twende ukanionyeshe....wakafika kwa jamaa, akaonyeshwa mbwa.
JAMAA: Umesema anajua kuongea?
MBWA:Ndio mi naongea, halafu ni poa ukininunua , nilishakuwa mbwa wa polisi nimekamata sana wezi mpaka nikapandishwa cheo nikawa mkuu wa intelijensia kanda maalumu
JAMAA: Mi sitaki mbwa wa polisi
MBWA: Naweza kufanya kazi nyingine kama kukuletea viatu, au kwenda kununulia vocha za simu
JAMAA: Okay ntakuchukua. Sasa Mzee inakuwaje wale mbwa wa kawaida unawauza shilingi alfu hamsini na huyu mbwa anaongea unamuuza  alfu tano?
MUUZA MBWA: Bwana tatizo la huyo mbwa muongo sana, hebu ondoka nae.

No comments: