PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HATIMAE WATU WANAFIKIA KUKOPI NA KUPESTI UTENGENEZAJI WA WATOTO

Baada ya miaka michache watoto wengi watazaliwa wanafanana kila kitu. Hii ni sentensi ya kwanza iliyomo katika ripoti ya kurasa 70 iliyotengenezwa na watafiti feki waliolipwa pesa feki na hii blog yenye utata. Watafiti hawa wamekuja na maelezo kuwa kwa kuwa kizazi cha sasa kimeanza kubobea kwenye kopi endi pesti kwa karibu kila jambo, karibuni wataanza kukopi na kupesti hata kutengeneza watoto na hivyo watoto wao watafanana na kule waliko kopi na kupesti.
Wachunguzi hawa ambao wameomba majina yao yasijulikane ili watu wasiyakopi na kupesti wamekuja na ripoti hii na kumkabidhi mkurugenzi wa blog ambaye amesema karibuni ataiweka wazi ili watu waikopi na kuipesti.

Comments