PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HAKUNA MJINGA ZAIDI

MULI: Mke wangu ananidharau sana
KIDOA: Kivipi?
MULI: Anasema eti hakuna mwanaume mjinga kama mimi
KIDOA: Huyo mama hajaona wajinga nini? Ona, ngoja nimuite yule dereva wa kibajaji ndio ujue duniani kuna wajinga. Kidoa akamuita yule dereva wa kibajaji
KIDOA: Aise hebu chukua hizi shilingi elfu mbili, nenda pale kwangu kaangalie kama nipo
KIBAJAJ: Ndio mzee.. Dereva akaondoka huyooo
KIDOA: Unaona Mudi sasa ndio ujue kuna watu wajinga bwana
MULI: Aise kweli yule mjinga, ningekuwa mimi ningechukua hela halafu ningekupigia simu nikuulize kama upo

Comments