HATUPIMI BANDO

10 July 2013

HAHAHAHA TEAM CHEKANAKITIME YAFIKISHA 400,000, blog inaangalia uwezekano wa kugawa bia bure kwa wasomaji

Yaani kuna mambo mengine ya ajabu sana, eti hii blog isiyo na maana kabisaa, haina breaking news, haina picha zile za 'ingia uwe wa kwanza kuona', haina ishu kabisaaa eti imetimiza waingiaji 400,000. Aise nyie jamaa mna roho ngumu sana  daaah, kwa heshima yenu utawala wa blog hii unafanya mpango wa kuajiri wafanya kazi wengine kama saba hivi ili mkija ofisini kwetu mkute ugali bure, konyagi kwa wingi bure, mibia bure yaani mnastahiri kula bata bure mmeonae. 
Bosi wetu kasema juzi alidiskasi na Rais wa dunia ishu ya kuwapeleka wote mhamie Marekani na kwa wale walioko huko tayari kupewa uraia fasta, so kusoma humu ni faida kubwa. Kwa walioko Marikani kesho ukiamka nenda tu Homeland office yoyote waambie, 'I am team Chekanakitime, so give me Citizenship' watanipigia simu mi ntakudhamini, basi kila kitu kitaenda sawa, hata nyie ambao mnaishi kimkandamkanda nendeni tu nimeshadiskasi ishu yenu na Mzee. Kwa wale walioko Bongo ambao wanataka kuhamia kule nendeni tu pale Ubalozini waambieni wale askari, kuwa "Mimi ni team Chekanakitime nimekuja kujaza fomu' watakuelekeza room 4 kule kuna kibao kimeandikwa Visa for Chekanakitime, huko utapewa fom utajaza , pia utapewa na nauli ya kwenda States(unaweza kuchagua usafiri kama ni meli au ndege).  Tumia vizuri nafasi hii adimu kubadilisha maisha yako.
 YES WE CAN NOT

No comments: